Marais Wastaafu Mwinyi na Kikwete kama mnavyoshangaa Ujasiri wa Hayati Rais Magufuli, nasi pia tunawashangaa kwanini hamkufanya nyie

Hawa maraisi walifanya makubwa sana tena sana tofauti na makufuli wenu amini hilo!
tatizo la hawa wazee hawakuwa;
watu wa kijimwambafai
kupenda sifa
kupenda kujionyesha
walikuwa na mifumo ya kufanya kazi tofauti na makufuli hakuwa na mfumo alikuwa akitaka aonekane yeye tu.
Kupenda kusifiwa ktk kila kitu.
hawakuwa waongo kama makuful;i wako.
 
Mleta mada umezaliwa lini mwenzetu..Siko hapa kumtetea Rais Mwinyi lakini nakushangaa sana unavyosema aliharibu uchumi. Kabla yake uchumi ulikuwaje?!
Nakuuliza kama mdau ambaye nilikuwepo wakati wa maduka ya kaya na unga wa ugali wa njano (Yanga).
 
Rais Mstaafu Mzee Mwinyi..' Yanayoendelea hapa katika Ujenzi wa hili Bwawa la Nyerere ni Maajabu makubwa Watanzania karibuni mjionee jinsi Hayati Rais Dkt. Magufuli alivyokuwa kweli anatimiza ndoto za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere '

Rais Mstaafu Mzee Kikwete..' Kwa hiki kinachoendelea hapa Katika huu Ujenzi wa Bwawa la Nyerere siamini macho yangu na najiuliza huu Ujasiri wa Kupongezwa kabisa Hayati Rais Dkt. Magufuli aliutoa wapi kwani ameonyesha Uthubutu na kutimiza Ndoto njema za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere '

Mwana JamiiForums Krav Maga..' Kiukweli nawashangaa sana Marais Wastaafu akina Mzee Mwinyi na Kikwete kwa Unafiki wao mkubwa usiovumilika wa Kusifia zilizokuwa Juhudi za Hayati Rais Dkt. Magufuli wakati hata Wao katika Awamu zao wangeyafanya haya ili Hayati alipokuwa Rais aendelee na mambo mengine ya Msingi kwa Watanzania hasa Ajira, Afya, Maji na Elimu ya hovyo hovyo iliyopo Tanzania kwa sasa '

Ushauri wa bure tu kwa Wastaafu hawa ni bora wanyamaze tu kuliko kuendelea Kujichoresha na Kuendeleza Utamaduni ule ule wa Unafiki ulioota Mizizi ndani ya Chama Tawala CCM ulioenda mpaka kwa Watendaji wa Serikali yao.

Halafu Rais Mstaafu Kikwete utaanzaje Kumsifia sana Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Juhudi zake huku ukisahau Kumpongeza sana Rais Mstaafu Hayati Mkapa ambaye aliweka Rekodi ya Ukusanyaji wa Mapato makubwa na baadhi ya Pesa hizo pia zilikusaidia hata Wewe kuja kuwa Rais wa Tanzania na zingine kuanza Kukusaidia kuendesha nchi japo vyanzo vya ndani vinasema ulipoondoka hukuacha Kitu pale Hazina na Hayati Dkt. Magufuli alikulaumu na Kuchukizwa mno na hili?

Na Wewe Rais Mstaafu Mzee Mwinyi nadhani tena ndiyo ungekuwa tu Mpole kwani ni katika Awamu yako ya Utawala / Uongozi nadhani ndiyo Uchumi wa nchi ya Tanzania uliharibika na kuzalisha Mafisadi Papa wengi, Rushwa kushamiri hadi Rais Mstaafu na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akawa anakusema tena hadharani. Na sijui ni kwanini katika Kitabu chako hukutueleza Watanzania kwanini wale Tausi walitoweka na kwenda mno nchi za Uarabuni na hukusema nani katika Familia yako alikuwa akiratibu huko Kutoweka Kwao.

Mnazeeka vibaya nyamazeni mnatuboa!
Wote ni CCM Na mwendazake wao. Wameifisidi nchi yote. Wameuwa watu wabaki madarakani. Mungu atawalipa
 
Hivi ukisikia wanashangaa unaamini wanashangaa kweli au ndio mambo ya kuvikana vilemba vya ukoka? JK alianzisha umeme wa gas, na matarajio ilikuwa kuzalisha 5,000m atashangaa nini kwenye umeme wa 2,115mg? Huyo Mwinyi kwa umri wake hapo alipo hata akiona mshumaa unawaka atashangaa. Hivi ulitegemea waseme tofauti na walichokisema wakati wamepewa picnic ya bure na imprest juu?
Alipoanzisha halafu ikawaje?
 
Hawa maraisi walifanya makubwa sana tena sana tofauti na makufuli wenu amini hilo!
tatizo la hawa wazee hawakuwa;
watu wa kijimwambafai
kupenda sifa
kupenda kujionyesha
walikuwa na mifumo ya kufanya kazi tofauti na makufuli hakuwa na mfumo alikuwa akitaka aonekane yeye tu.
Kupenda kusifiwa ktk kila kitu.
hawakuwa waongo kama makuful;i wako.
Umemaliza kila kitu….Hoja ifungwe
 
Rais Mstaafu Mzee Mwinyi..' Yanayoendelea hapa katika Ujenzi wa hili Bwawa la Nyerere ni Maajabu makubwa Watanzania karibuni mjionee jinsi Hayati Rais Dkt. Magufuli alivyokuwa kweli anatimiza ndoto za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere '

Rais Mstaafu Mzee Kikwete..' Kwa hiki kinachoendelea hapa Katika huu Ujenzi wa Bwawa la Nyerere siamini macho yangu na najiuliza huu Ujasiri wa Kupongezwa kabisa Hayati Rais Dkt. Magufuli aliutoa wapi kwani ameonyesha Uthubutu na kutimiza Ndoto njema za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere '

Mwana JamiiForums Krav Maga..' Kiukweli nawashangaa sana Marais Wastaafu akina Mzee Mwinyi na Kikwete kwa Unafiki wao mkubwa usiovumilika wa Kusifia zilizokuwa Juhudi za Hayati Rais Dkt. Magufuli wakati hata Wao katika Awamu zao wangeyafanya haya ili Hayati alipokuwa Rais aendelee na mambo mengine ya Msingi kwa Watanzania hasa Ajira, Afya, Maji na Elimu ya hovyo hovyo iliyopo Tanzania kwa sasa '

Ushauri wa bure tu kwa Wastaafu hawa ni bora wanyamaze tu kuliko kuendelea Kujichoresha na Kuendeleza Utamaduni ule ule wa Unafiki ulioota Mizizi ndani ya Chama Tawala CCM ulioenda mpaka kwa Watendaji wa Serikali yao.

Halafu Rais Mstaafu Kikwete utaanzaje Kumsifia sana Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Juhudi zake huku ukisahau Kumpongeza sana Rais Mstaafu Hayati Mkapa ambaye aliweka Rekodi ya Ukusanyaji wa Mapato makubwa na baadhi ya Pesa hizo pia zilikusaidia hata Wewe kuja kuwa Rais wa Tanzania na zingine kuanza Kukusaidia kuendesha nchi japo vyanzo vya ndani vinasema ulipoondoka hukuacha Kitu pale Hazina na Hayati Dkt. Magufuli alikulaumu na Kuchukizwa mno na hili?

Na Wewe Rais Mstaafu Mzee Mwinyi nadhani tena ndiyo ungekuwa tu Mpole kwani ni katika Awamu yako ya Utawala / Uongozi nadhani ndiyo Uchumi wa nchi ya Tanzania uliharibika na kuzalisha Mafisadi Papa wengi, Rushwa kushamiri hadi Rais Mstaafu na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akawa anakusema tena hadharani. Na sijui ni kwanini katika Kitabu chako hukutueleza Watanzania kwanini wale Tausi walitoweka na kwenda mno nchi za Uarabuni na hukusema nani katika Familia yako alikuwa akiratibu huko Kutoweka Kwao.

Mnazeeka vibaya nyamazeni mnatuboa!
Unashangaa kwa kuwa hujui kuwa kila jamabo linawakati wake, najua utashangaa kwa ni nyerere aliazimia Dodoma iwe makao makuu lakini hakwenda wakati huo.Utashangaa kwa nini nyerere alisema baadhi ya madini yasichimbwe kwa kuwa muda wake haujafika kuyachimba,utashangaa kwanini nyerere ndiye aliyetoa wazo la kujenga bwawa la umeme lakini haakujenga wakati huo.

Utashangaa pia kwanini Hayati magufuli alikimbia kuendelea na mradi wa Mchuchuma na Liganga.Basi ukiwa unashangaa nikuambie kuwa mazingira aliyoachiwa Hayati Magufuli yalikua mazuri kuanzisha Mradi wa Hydro Power,ukiwa bado hujamaliza kushangaa nitakuambia kua Mazingira aliyochiwa Kikwete na Mzee mkapa ndiyo yaliyo mwezesha kujenga zaidi kilomita 10000 za barabara na kuunganisha mikoa mingi kwa barabara za Lami.Ukimaliza kushangaa untuambie.​
 
Huu ni uungwana tu wa kumsema mtu vizuri.

Kila rais kafanya yake mazuri kulingana na wakati wake

Ulitaka Mkapa ajenge stieglers kabla ya kusimika mfumo wa TRA?

Ulitaka Kikwete ajenge Stieglers huku wananchi wa Kagera wakitaka kwenda Kagera kwanza lazima wazunguukie Kenya?
Kupanga ni kuchagua
Economic point of view. No qn bro.
 
Waziri gani alisimamia uuzwaji wa Nyumba za serikali?
Nashangaa kwa nini watu wanamsifia mkapa..

Ufisadi na mikataba mibovu nchii hii imefanyika kipindi cha mkapa..

Wananchi tuliambiwa tule nyasi.

Mawaziri wa awamu ya mkapa walitajirika vya kutosha

Nyumba za serikali ziliuzwa kwa bei ya boda boda

Mashirika ya uma yaliuzwa kwa bei za ajabu..

Mfano Nbc iliuzwa yenyewe na asset zake nchi nzima kwa bei ambayo haitoshi hata kununua ghorofa lao 1 pale posta mpya kwa bei halali

Mkapa na mwanasheria wake mkuu chenge wameirudisha sana nyuma hii nchi
 
Wanaboa mno Ndugu. Bora wanyamaze.
Kila raisi ana vipaumbele vyake kama siku zote tunavyoambiana humu kutoweka mkazo katika mradi huo kwa maraisi waliopita haifanyi kupoteza Legacy zao walizoziacha katika nchi hii...kuna mambo Kikwete kafanya na Magufuli hajayafanya lakini Magu hakuacha kuyasifia katika utawala wake wa miaka mitano..hivyohivyo kuna vipaumbele aliviweka Mbele mheshimiwa Mwinyi lakini wengine walivitupilia mbali
 
katika Marais ambao wamelichakaza hili taifa wa kwanza ni jk,wapili mkapa huyu aliuza takribani 75% ya asset za nchi,migodi ,mashirika,makampuni ,taasisi n.k ,ziliuzwa zote kwa watu binafsi nchi ikabaki haina kitu. Mkapa &jk ,wametughalimisha Sana aise.
 
Wadau ugumu wa kazi kuitenda. Nadhani wengi humu hamuijui historia ya nchi hii kisiasa na kiuchumi. Wadau kiufupi nilikuwapo enzi za mwalimu, tumekuwa tukisifia Sana kwamba

Enzi za mwalimu kulikuwa na viwanda kibao vikifanya kazi na kuajiri watu lukuki. Sawa watu waliajiriwa wakapata mishahara kwa Ruzuku toka serikalini wakaishi vizuri lkn sio kwa tija ya vile viwanda Bali kwa RUZUKU.

Maana yake ni kwamba viwanda havikuzalisha kwa tija, hakukuwa na faida itokanayo na uzalishaji wa bidhaa zikauzwa kwa wingi na viwanda vikaneemeka. Sababu kwa wakati ule viwanda vilikuwepo lkn bidhaa madukani hakuna. Imagine sukari hakuna, unga hakuna, mafuta hakuna, nguo hakuna.

Sasa mnachofanya mnapangishwa foleni weekly Mara moja linakuja gari lina hizo bidhaa mnapangiwa kiwango Cha kununua. Mwalimu aliweza kutuunganisha kisiasa lkn kwa uchumi alishindwa.

Mwinyi aliipokea nchi ikiwa hoi Sana, kwa waliokuwepo watashuhudia nchi ilikuwa haikopesheki, siasa ya ujamaa mabeberu hawakuipenda, Nyerere alipewa masharti na imf ashushe thamani ya pesa yetu lkn alikataa.

Hi Sasa Mwinyi alipoingia ndo akaanza mazungumzo na imf wakakubaliana tukashusha thamani ya pesa yetu, tukaanza kukopesheka. Sasa wadau Mwinyi hakukuta investment yeyote yenye uwezo wa kulipa Kodi, wananchi wako hoi mifukoni, serikali haina pesa!

Mzee wetu alijitahidi Sana kukopa nje mipaka ilikuwa imefungwa bidhaa za nje haziingii, wakati wake mipaka ikafunguliwa km mnakumbuka vitu vya mwanzo kuingia vilikuwa toka Taiwan, plastics shoes zile, vyombo vyombo vya plastics. Kwa hali Kama hiyo huwezi fanya lolote, pale kariakoo barabara kibao zilikuwa vumbi tupu. Ile ya uhuru ndo ilikuwa na lami.

Kwa mantiki hiyo hakuweza fanya lolote kubwa sababu alikuta nchi iko hoi, kazi kubwa aliyoifanya ni kujenga trust kwa taasisi za kifedha za nje na nchi zenye kutoa misaada na mikopo na kujenga uhusiano mpya na nchi zenye nguvu za kiuchumi na kidogo kidogo wageni wakaanza kuja Tanzania.

Mkapa alipoingia aliona serikali haiwezi fanya biashara na kutawala wakati mmoja, akaamua kubinafsisha viwanda na kuuza baadhi ya assets za serikali ili kujitoa kwenye biashara na kuiachia sekta binafsi. Wadau tuliokwepo hivyo vitu mnavyosema leo viliuzwa kwa bei Chee vilikuwa ni mizigo kwa serikali.

Serikali ilikuwa inajitekenya na kucheka yenyewe! Benki serikali ilikuwa inatoa Ruzuku hakukuwa na faida. Noambie km mwaka 2010 takwimu zilionesha watanzanua milioni 2;tu ndo wanna akaunti benki, na wakati ile nilikuwa na account tatu, Sasa imagine 1995 huko ni wateja wangapi walikiwepo bank, wafanyabiashara wangapi walikuwa wakikopesheka wakati huo? Ilikuwa hasara tupu.

Viwanda vilikuwa na mitambo ya teknolojia ya 60s na 70s huko wakati na zimekufa haIfanyi kazi tena, au kwa sababu ya wear and tear production cost no kubwa Sana! Serikali haina fedha za kujiendesha yenyewe sembuse kufufua viwanda.

Akaamua abinafsishe viwanda na sekta nyi gine ili apate fedha za kujiendesha serikali na kupeleka uchumi kwenye uhalisia. Akaanzisha TRA akaunda mfumo wa kodi ambao haukwepo na Kodi zikaanza kulipwa. Term yake ya kwanza ilikuwa ngumu kama hi ya Magu, watu waliita ukosefu was pesa Ukapa. Maana walikuwa wametoka kwenye ruksa! Mwinyi hakukusanya Kodi, misamaha ilikuwa kibao watu walijichotea kivyao serikalini huko.

Mkapa alifaulu kupata fedha za kutosha akaanza Sasa kujenga majengo ya kisasa ya ofisi za serikali, maana ilikuwa ofisi za serikali hali ni mbaya Sana. Nakumbuka ilipojengwa Mwenge TRA pale watu walikuwa wakienda kushangaa ofisi nzuri za serikali Zina mpaka AC. Posta kule majengo yakakarabatiwa vizuri AC zikawekwa, barabara zikaanza wekwa lami Sasa.

Kwa sababu aliweza kusanya Kodi basi akaanza kurekebisha Mambo ya muhimu ambayo baajeti yake si kubwa mind you wawekezaji bado walikuwa wachache Sana. Kipindi Cha pili Cha Mkapa kikawa na mafanikio makubwa Sana lkn kila Rais anapokuja anakuwa na vipaumbele vyake tokana na uchumi unavyomruhusu. Kwa bajeti ya trilioni Saba kujenga kitu kimoja tungekula nyasi.

Kikwete alikuja nchi iko vizuri kidogo lkn na yeye alikuwa na priorities zake! Kajenga barabara nyingi bila majisifu Sana, mipango mingi ya maendeleo na miradi tunayoiona ikitekelezwa Sasa ilipangwa na kuratibiwa wakati wake, aliwaachia wabongo fursa wakazitumia kujineemesha, wakala, wakasaza wakaanza kumlaumu kwa kuwaneemesha, akawaachia mumtusi kwenye vyombo vya habari, fursa zikawa kila Kona, baba huyu wa demokrasia aliwaangalia km baba anavyomsanifu mtoto wake akihangaika na balehe iliyokuja bila taarifa.

Mlisafiri nje kama mnaenda kibaha, miradi ya serikali mkahamishia nyumbani kwenu, mkajiona mmemaliza, mkaona shibe mwana malevya mkadai mnataka dikteka huyu baba hafai ni dhaifu, Mungu si athumani akawapa ombi lenu!!
Jiwe akaingia madarakani akakuta Mambo swaafi walipakodi wa kutosha nchi inaweza kufanya miradi mikubwa, lkn tuondoe hii shibe iliyowalevya Hawa watanzania.

Jiwe aliweza na kuthubutu kufanya hiyo miradi sababu alikuta watangulizi wake washatengeneza njia! Yeye akaboresha mifumo ya Kodi na ukusanyaji wake, na miradi aliisimamia yeye mwenyewe kwa karibu Sana na kwa kutumia mkono was chuma miradi imekwenda.

Hakuwa muoga wa kukopa nje anajua nchi ina uwezo wa kulipa.
Point yangu ni kwamba msiwalaumu waliotangulia, nchi haikuwa na uwezo kifedha kugharamia miradi hiyo. Tulikotoka siasa yetu km nchi ilitufanya tisiaminike Sana na mashirika ya kimataifa na wawekezaji.

Sisi tunaaminishwa kuhusu usahihi was azimio la Arusha lkn kiuchumi limetucost Sana, mwekezaji Hana uhakika wa kesho. Mnaweza amka mkasema hii ni Mali ya Taifa. Akina Mzee Mwinyi muda was mwingi ulikuwa ni kujenga uaminifu wa siasa na uchumi I'll kuvutia mwekezaji.

Hata wewee ulianza kazi ukikaa kwenu, ulipopita muda Fulani ukahamia geto, mafanikio yalipokuja ukahamia nyumba kubwa, ukaoa, ukapata watoto, ukaanza ujenzi, ukahamia kwako. Hapo si chini ya 10yrs. Mafanikio no Safari ndefu tusiwabeze wastaafu wetu!!!
 
Kila awamu ilifanya yake,mwinyi aliipokea nchi ikiwa taabani,mkapa akaendelea kuitibu akaifikisha pahala,akaishika kikwete akaisogeza wewe akaona sasa aiunganishe kwa mabarabara maana nchi bila barabara haiwesekaniki,ndipo akaitwaa mwendazake naye akatusogeza pahala fulani,TAIFA LETU LIMEFIKA HAPA KWA MTIRIRIKO WA VIONGOZI WOTE WASTAFU KUFANYA KAZI ILIYOTUKUKA.
N.B-Ni mpumbuvu pekee ndiye atambeza kiongozi yeyote mstaafu.
 
Mleta mada umezaliwa lini mwenzetu..Siko hapa kumtetea Rais Mwinyi lakini nakushangaa sana unavyosema aliharibu uchumi. Kabla yake uchumi ulikuwaje?!
Nakuuliza kama mdau ambaye nilikuwepo wakati wa maduka ya kaya na unga wa ugali wa njano (Yanga).
Vijukuu vya juzi juzi havina hata ufahamu wa kujua tulipotoka na tunapoelekea.
 
At least mimi sidanganyiki. Hiyo ziara ina lengo la kuondoa upinzani wa kujenga bandari ya Bagamoyo. Kivipi: Watakuja kufanya tena ziara sehemu inapotakiwa kujengwa bandari halafu wasifie.... Just wait...
Sema mi naona hii ziara ina lengo la kututoa kwenye mjadala wa Katiba mpya! CCM nawajuwa Wajanja sana! Ona Sasa tumeshasahau kujadili Katiba,eti tuko tunajadili ziara ya Wastaafu!!
 
Sema mi naona hii ziara ina lengo la kututoa kwenye mjadala wa Katiba mpya! CCM nawajuwa Wajanja sana! Ona Sasa tumeshasahau kujadili Katiba,eti tuko tunajadili ziara ya Wastaafu!!
Hawana wasiwasi hata kidogo na jambo la katiba. Wanajua watanzania wengi ni waoga na hawataweza kukinukisha hasa ukizingatia hali ya sasa i.e. watu bado wako kwenye honeymoon ya kufurahia kuondoka kwa utawala katili na kuingia kwa rais mpole tena mwanamke. Nakuhakikishia washinikiza katiba mpya wamefanya timing mbaya sana. Wangesubiri kwanza rais Samia achokwe, jambo ambalo llazima litatokea kwa sababu hakuna kipya anachofanya.
 
Hakuna mamlaka aliyojenga mkapa.. alifata tu maelekezo ya wahisani.. mwaka ambao TRA ilianzishwa, kenya ilianzishwa KRA zambia ZRA na uganda URA na nchi zingine..

Usidanganye mkapa alibuni yeye.. ilikuwa ni lazima nchi zote zianzishe mamlaka hizo kwa kufata maelezo ya wahisani

kwa hiyo?
 
Back
Top Bottom