Marais Wastaafu Mwinyi na Kikwete kama mnavyoshangaa Ujasiri wa Hayati Rais Magufuli, nasi pia tunawashangaa kwanini hamkufanya nyie

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Rais Mstaafu Mzee Mwinyi..' Yanayoendelea hapa katika Ujenzi wa hili Bwawa la Nyerere ni Maajabu makubwa Watanzania karibuni mjionee jinsi Hayati Rais Dkt. Magufuli alivyokuwa kweli anatimiza ndoto za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere '

Rais Mstaafu Mzee Kikwete..' Kwa hiki kinachoendelea hapa Katika huu Ujenzi wa Bwawa la Nyerere siamini macho yangu na najiuliza huu Ujasiri wa Kupongezwa kabisa Hayati Rais Dkt. Magufuli aliutoa wapi kwani ameonyesha Uthubutu na kutimiza Ndoto njema za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere '

Mwana JamiiForums Krav Maga..' Kiukweli nawashangaa sana Marais Wastaafu akina Mzee Mwinyi na Kikwete kwa Unafiki wao mkubwa usiovumilika wa Kusifia zilizokuwa Juhudi za Hayati Rais Dkt. Magufuli wakati hata Wao katika Awamu zao wangeyafanya haya ili Hayati alipokuwa Rais aendelee na mambo mengine ya Msingi kwa Watanzania hasa Ajira, Afya, Maji na Elimu ya hovyo hovyo iliyopo Tanzania kwa sasa '

Ushauri wa bure tu kwa Wastaafu hawa ni bora wanyamaze tu kuliko kuendelea Kujichoresha na Kuendeleza Utamaduni ule ule wa Unafiki ulioota Mizizi ndani ya Chama Tawala CCM ulioenda mpaka kwa Watendaji wa Serikali yao.

Halafu Rais Mstaafu Kikwete utaanzaje Kumsifia sana Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Juhudi zake huku ukisahau Kumpongeza sana Rais Mstaafu Hayati Mkapa ambaye aliweka Rekodi ya Ukusanyaji wa Mapato makubwa na baadhi ya Pesa hizo pia zilikusaidia hata Wewe kuja kuwa Rais wa Tanzania na zingine kuanza Kukusaidia kuendesha nchi japo vyanzo vya ndani vinasema ulipoondoka hukuacha Kitu pale Hazina na Hayati Dkt. Magufuli alikulaumu na Kuchukizwa mno na hili?

Na Wewe Rais Mstaafu Mzee Mwinyi nadhani tena ndiyo ungekuwa tu Mpole kwani ni katika Awamu yako ya Utawala / Uongozi nadhani ndiyo Uchumi wa nchi ya Tanzania uliharibika na kuzalisha Mafisadi Papa wengi, Rushwa kushamiri hadi Rais Mstaafu na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akawa anakusema tena hadharani. Na sijui ni kwanini katika Kitabu chako hukutueleza Watanzania kwanini wale Tausi walitoweka na kwenda mno nchi za Uarabuni na hukusema nani katika Familia yako alikuwa akiratibu huko Kutoweka Kwao.

Mnazeeka vibaya nyamazeni mnatuboa!
 
Nashangaa kwa nini watu wanamsifia mkapa..

Ufisadi na mikataba mibovu nchii hii imefanyika kipindi cha mkapa..

Wananchi tuliambiwa tule nyasi.

Mawaziri wa awamu ya Mkapa walitajirika vya kutosha

Nyumba za serikali ziliuzwa kwa bei ya boda boda

Mashirika ya uma yaliuzwa kwa bei za ajabu..

Mfano NBC iliuzwa yenyewe na asset zake nchi nzima kwa bei ambayo haitoshi hata kununua ghorofa lao 1 pale posta mpya kwa bei halali

Mkapa na mwanasheria wake mkuu Chenge wameirudisha sana nyuma hii nchi
 
Rais Mstaafu ni mmoja wa washauri wa yule anayekuwa ikulu hivyo moja kwa moja ana haki ya kuongelea kinachofanywa na serikali.

Mama Samia alimwomba JK akamuwakilishe kule kwenye msiba wa Kaunda, anaweza kumwomba Mwinyi akamuwakilishe kwenye tukio fulani ulaya.

Wanakuwa wamestaafu urais lakini ni sehemu ya serikali mpaka wanapokufa.

Na hakuna rais anayeweza kufanya kila kitu katika ujenzi wa nchi kila mmoja anaishia pale anapoweza na kumkabidhi ofisi mwingine.
 
Umeongelea upande mbaya wa Mkapa anao mzuri tena ni wa kuenziwa.

Mkapa alijenga mamlaka zote za kiuchumi ambazo ndizo zinafanya miradi ya kuendeleza nchi iweze kuwa na tija.

Hakuna mamlaka aliyojenga Mkapa.. alifata tu maelekezo ya wahisani.. mwaka ambao TRA ilianzishwa, Kenya ilianzishwa KRA Zambia ZRA na Uganda URA na nchi zingine..

Usidanganye Mkapa alibuni yeye.. ilikuwa ni lazima nchi zote zianzishe mamlaka hizo kwa kufata maelezo ya wahisani
 
Wanaboa mno Ndugu. Bora wanyamaze.

Hivi ukisikia wanashangaa unaamini wanashangaa kweli au ndio mambo ya kuvikana vilemba vya ukoka? JK alianzisha umeme wa gas, na matarajio ilikuwa kuzalisha 5,000m atashangaa nini kwenye umeme wa 2,115mg? Huyo Mwinyi kwa umri wake hapo alipo hata akiona mshumaa unawaka atashangaa. Hivi ulitegemea waseme tofauti na walichokisema wakati wamepewa picnic ya bure na imprest juu?
 
Hakuna mamlaka aliyojenga mkapa.. alifata tu maelekezo ya wahisani.. mwaka ambao TRA ilianzishwa, kenya ilianzishwa KRA zambia ZRA na uganda URA na nchi zingine..

Usidanganye mkapa alibuni yeye.. ilikuwa ni lazima nchi zote zianzishe mamlaka hizo kwa kufata maelezo ya wahisani
Hawa kina ewura na wengineo ni kazi ya Mkapa.

Unataka kusema Mkapa hajafanya lolote!!. Watanzania shukrani zetu ndogo sana.
 
Huu ni uungwana tu wa kumsema mtu vizuri.

Kila rais kafanya yake mazuri kulingana na wakati wake

Ulitaka Mkapa ajenge stieglers kabla ya kusimika mfumo wa TRA?

Ulitaka Kikwete ajenge Stieglers huku wananchi wa Kagera wakitaka kwenda Kagera kwanza lazima wazunguukie Kenya?
Kupanga ni kuchagua
 
Hizo mamlaka zilikuwa ni masharti ya wahisani lazima uzianzishe nchini mwako utake usitake..
Kutekeleza masharti ya wahisani kulienda pamoja na ongezeko la pato la taifa kwa njia ya kodi.

Usiseme hiyo sio kazi nzuri ya Mkapa. Mama Samia nae anapigana uwekezaji ubadili hali ya uchumi wa watu.

Na yeye baadae ataambiwa hakufanya chochote bali ni wageni ndio walichangia kukuza uchumi.
 
Rais Mstaafu Mzee Mwinyi..' Yanayoendelea hapa katika Ujenzi wa hili Bwawa la Nyerere ni Maajabu makubwa Watanzania karibuni mjionee jinsi Hayati Rais Dkt. Magufuli alivyokuwa kweli anatimiza ndoto za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere '

Rais Mstaafu Mzee Kikwete..' Kwa hiki kinachoendelea hapa Katika huu Ujenzi wa Bwawa la Nyerere siamini macho yangu na najiuliza huu Ujasiri wa Kupongezwa kabisa Hayati Rais Dkt. Magufuli aliutoa wapi kwani ameonyesha Uthubutu na kutimiza Ndoto njema za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere '

Mwana JamiiForums Krav Maga..' Kiukweli nawashangaa sana Marais Wastaafu akina Mzee Mwinyi na Kikwete kwa Unafiki wao mkubwa usiovumilika wa Kusifia zilizokuwa Juhudi za Hayati Rais Dkt. Magufuli wakati hata Wao katika Awamu zao wangeyafanya haya ili Hayati alipokuwa Rais aendelee na mambo mengine ya Msingi kwa Watanzania hasa Ajira, Afya, Maji na Elimu ya hovyo hovyo iliyopo Tanzania kwa sasa '

Ushauri wa bure tu kwa Wastaafu hawa ni bora wanyamaze tu kuliko kuendelea Kujichoresha na Kuendeleza Utamaduni ule ule wa Unafiki ulioota Mizizi ndani ya Chama Tawala CCM ulioenda mpaka kwa Watendaji wa Serikali yao.

Halafu Rais Mstaafu Kikwete utaanzaje Kumsifia sana Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Juhudi zake huku ukisahau Kumpongeza sana Rais Mstaafu Hayati Mkapa ambaye aliweka Rekodi ya Ukusanyaji wa Mapato makubwa na baadhi ya Pesa hizo pia zilikusaidia hata Wewe kuja kuwa Rais wa Tanzania na zingine kuanza Kukusaidia kuendesha nchi japo vyanzo vya ndani vinasema ulipoondoka hukuacha Kitu pale Hazina na Hayati Dkt. Magufuli alikulaumu na Kuchukizwa mno na hili?

Na Wewe Rais Mstaafu Mzee Mwinyi nadhani tena ndiyo ungekuwa tu Mpole kwani ni katika Awamu yako ya Utawala / Uongozi nadhani ndiyo Uchumi wa nchi ya Tanzania uliharibika na kuzalisha Mafisadi Papa wengi, Rushwa kushamiri hadi Rais Mstaafu na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akawa anakusema tena hadharani. Na sijui ni kwanini katika Kitabu chako hukutueleza Watanzania kwanini wale Tausi walitoweka na kwenda mno nchi za Uarabuni na hukusema nani katika Familia yako alikuwa akiratibu huko Kutoweka Kwao.

Mnazeeka vibaya nyamazeni mnatuboa!
Kubali, kataa: Magufuli hayupo keshaondoka na kamwe hatarudi tena!

Mimi namkumbuka kwa mabaya mengi yaliyotokea wakati wake, na yeye ' aliyabariki': Watu kupotea- Azori, Ben Saa8 etc; T. A. M. Lissu kupigwa risasi; Watu kuuliwa kiholela na maiti kuokotwa kwny fukwe; Viongozi kudhalilishwa majukwaani; Biashara ya kununua binadamu- wabunge na madiwani wa upinzani; Kunajisi uchaguzi s/mitaa na uchaguzi mkuu 2020; Kuwanyima watumishi wa umma stahiki zao kwa miaka 5; Lugha chafu ambazo hazistahili kutoka kwa kiongozi- aseweza kulipa nauli apige mbizi, matajiri wataishi kama shetani, laleni na mavi yenu ndani etc; Kukiuka taratibu za manunuzi ya umma na kumfukuza cag aliyebaini upotevu wa 1.5T etc etc.

Mabaya ni mengi, hata kuteua watu wa hovyo na katili- Bashite, Sabaya etc. Naomba msaada anaeweza kuendeleza hii orodha.

Sasa: TUNATAKA KATIBA MPYA ambayo itahakikisha hatuwezi kupta viongozi wa hovyo, bali wanaoheshim haki za raia, watakaoheshimu na kulinda raia.
 
Rais Mstaafu ni mmoja wa washauri wa yule anayekuwa ikulu hivyo moja kwa moja ana haki ya kuongelea kinachofanywa na serikali.

Mama Samia alimwomba JK akamuwakilishe kule kwenye msiba wa Kaunda, anaweza kumwomba Mwinyi akamuwakilishe kwenye tukio fulani ulaya.

Wanakuwa wamestaafu urais lakini ni sehemu ya serikali mpaka wanapokufa.

Na hakuna rais anayeweza kufanya kila kitu katika ujenzi wa nchi kila mmoja anaishia pale anapoweza na kumkabidhi ofisi mwingine.
At least mimi sidanganyiki. Hiyo ziara ina lengo la kuondoa upinzani wa kujenga bandari ya Bagamoyo. Kivipi: Watakuja kufanya tena ziara sehemu inapotakiwa kujengwa bandari halafu wasifie.... Just wait...
 
Huu ni uungwana tu wa kumsema mtu vizuri.

Kila rais kafanya yake mazuri kulingana na wakati wake

Ulitaka Mkapa ajenge stieglers kabla ya kusimika mfumo wa TRA?

Ulitaka Kikwete ajenge Stieglers huku wananchi wa Kagera wakitaka kwenda Kagera kwanza lazima wazunguukie Kenya?
Kupanga ni kuchagua
Nimesikia fununu lengo la ziara ni kuweka mazingira sawa ili baadae waje wafanye ziara kama hiyo panopokusudiwa kujengwa bandari ya Bagamoyo na kutoa sifa kemkem ili kuondoa upinzani unaoonekana kushamiri. Sijui kama kuna ukweli katika hii tetesi.
 
Back
Top Bottom