Marais wa Tanzania wajutia kuwadhulumu Watanzania

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Hakika kila anayedhulumu, kamwe hatayamaliza maisha yake ya hapa Duniani kwa amani, na wala pepo hatairithi, bila ya toba iliyo kuu. Laana hata siku moja haikupi amani. Wote waliodhulumu mali, haki na uhai wa watu, wanaishi kwa majuto makubwa mioyoni mwao. Wanahangaika, wasijue watue vipi mizigo yao.

Mwalimu katika kujutia, alisema, "katiba ya Tanzania hii iliyopo ni mbaya, inamfanya Rais kuwa dikteta", maana yake ni kwamba alikuwa anajutia udikteta wowote alioufanya, na akaeleza kuwa chanzo chake ni katiba. Alikuwa akijuta, kwa nini hakuweza kufanya mabadiliko ya katiba, na kuifanya Tanzania kuwa na katiba bora yenye kuwapa haki Watanzania. Mwalimu, pamoja na kujua kuwa Katiba yetu ni mbaya, hakuibadili. Hili ndiyo kosa alilolijutia. Katika kupunguza simanzi moyoni mwake, aliamua kuweka wazi kuwa Katiba ambayo yeye alishiriki kuiandaa, na ambayo aliitumia kuongoza nchi, ilikuwa katiba mbaya kwa sababu inamfanya Rais kuwa dikteta na mungu mtu.

Akaja Mwinyi, alijua katiba ni mbaya, na mtangulizi wake alishuhudia hilo kwa kauli yake, lakini Mwinyi hakusimamia uanzishaji wa katiba mpya. Alifurahia kuwa Rais dikteta, japo katika kutenda, aliamua kuwa muungwana wa kiasi fulani, lakini hakuwahi kuonesha dhamira ya kuwataka Watanzania waongozwe kwa misingi ya haki inayosimamiwa na katiba bora. Laana itamwandama.

Akaja Mkapa, akaitumia vyema katiba inayomfanya Rais kuwa dikteta. Akafurahia. Akaitumia katiba hiyo hiyo, kuminya haki za kikatiba kwa wapinzani. Akawanyima Watanzania haki ya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi. Akawaua Wazanzibari, bila ya kuhojiwa na yeyote. Laana haikumwacha. Hakuyamalizia maisha yake kwa amani Duniani. Dhamira ilimtesa na kumsuta. Akaona aheri akiri na kuwaomba msamaha Watanzania. Kwenye kitabu chake, akasema, mauaji ya Wazanzibari, yaliutesa moyo wake. Pia akasema, anapenda nchi iwe na Tume huru ya uchaguzi. Wakati wa uongozo wake hakufanya, lakini baadaye dhamira yake iliendelea kumshtaki na kumtesa. Baada ya majuto na toba, Mungu akampumzisha.

Jakaya aliyafurahia mamlaka ya kidikteta. Akamaliza awamu yake ya kwanza bila ya kuandaa katiba bora. Mwishoni mwa muhula wake wa pili, akataka kujikosha, akanzisha mchakato wa katiba. Kwa vile Mungu hataki unafiki, hakufanikiwa. Ulikiwa na miaka 10, kwa nini ukasubirie mwaka wa 9 ndiyo uanzishe mchakato wa katiba mpya? Yaani wewe ulifurahia Urais wa kidikteta halafu unajikosha na kutaka katiba mpya mwishoni mwa muhula wako, katiba ambayo wewe hutaiishi kwa sababu hutakuwa madarakani! Mungu hataki unafiki, mchakato haukukamilika ili katika kumbukumbu ibakie kuwa ulifurahia kuwa Rais dikteta.

Akaja Magufuli, hakuwa mnafiki, yeye alinena wazi kuwa hataki Watanzania waongozwe kwa haki, hataki katiba mpya, hataki Watanzania wachague viongozi, wa kuchagua ni yeye tu. Akahakikisha kila mahali, si bungeni, si mahakamani, kote, ni yeye ndiye mwamuzi. Akasema kwamba muhimili wake, wa Urais, ndiyo una mizizi mirefu. Mingine yote au haina miziz au miziz yake inaelea hewani. Akataka afurahie mamlaka yasiyo na mipaka wala yasiyo hojiwa. Pamoja na kufanikiwa kuzima sauti za watu wote, pamoja na kuwafanyia uovu wa kila aina wanaohoji mamlaka yake, hakupata amani. Japo hakuna kipimo, lakini ukweli ni kuwa huyu ndiye Rais aliyeishi kwa kukosa amani kuliko kiongozi yeyote. Na mwisho Mungu akawapelekea injili wale wote walioamini kuwa wanaweza kutenda uovu wowote alimrudi Rais amewaruhusu, akawaonesha kuwa hakuna mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ambaye mamlaka yake hayana mipaka, ukiiondoa mipaka inayowekwa na wanadamu wenzako, utakutana na mamlaka ya aliyetuba. Akamwondoa Duniani mapema, akiwa hajafanikisha mambo mengi aliyoamini yangeweza kumwongezea utukufu.

Kule Zanzibar, Komandoo mwisho umekuwa wa majuto. Karume hana ani moyoni. Na sasa ameelezea jinsi CCM, kupitia Jecha, walivyopora ushindi wa Maalim Seif. Anasema , aliwaambia viongozi wenzake wa CCM kuwa, mboba hata wapinzani ni Wazanzibari? Kwa nini wananyimwa haki ya kuongoza. Akawaambia kuwa Maalim Seif ni mtu muungwana sana, tofauti na CCM walivypkuwa wakimpaka matope. Karume hana amani wala furaha kwa kushiriki dhuluma dhidi ya Seif. Jecha, ndiyo usiseme. Hawa wote wanatafuta njia ya kupungiza simanzi mioyoni mwao.

Sasa tunaye Samia, huyu naye kwa mwelekeo uliopo, anataka kutenda kama Kikwete, kuuleta mchakato wa katiba mpya mwishoni mwa awamu yake ya pili. Yaani hiyo katiba mpya ikambane Rais mwingine, na siyo yeye. Hakika naye hatafanikiwa maana Mungu hataki unafiki. Anayetaka Watanzania waongpzwe kwa haki, ni yule atakayeleta mchakato wa katiba mpya, mara tu baada ya yeye kushika madaraka ili yeye mwenyewe akawe mtu wa kwanza wa kuongoza kwa kutumia katiba hiyo inayotoa mamlaka makubwa kwa wananchi na siyo Rais. Hakika, na Samia, kama mchakato wa kupata katiba mpya, hautakuja kwenye awamu yake hii ya kwanza, laana ijuu yake, atajutia, na mwisho wake hautakuja kuwa na amani.

Watu kama Siro, Kingai, Mahita, na wengineo, wafiatilieni, kamwe hawataufurahia uzee wao hapa Duniani, na wala hawataonja furaha huko ahera. Hawa hata kama watapata mali na vyeo, lakini kamwe mioyo yao haitaionja furaha ili mateso yao ya ndani yakayazidi ya wale wadhulumiwa.

Ujumbe wa Jumla:

Kubambikia watu kesi za uongo, kutesa na kusababsha watu wafungwe bila hatia, ni matendo ya dhuluma. Dhuluma huleta laana kuanzia wewe mpaka kizazi chako cha 4.

Huu ni ujumbe maalum wa kitume kwa watu wenye Roho wa Mungu.

Msisitizo: Yafurahie maisha yako ya ujanani kwa kutenda haki, ili uzee wako ujae neema, matumaini na furaha.
 
Watu kama Siro, Kingai, Mahita, na wengineo, wafiatilieni, kamwe hawataufurahia uzee wao hapa Duniani, na wala hawataonja furaha huko ahera. Hawa hata kama watapata mali na vyeo, lakini kamwe mioyo yao haitaionja furaha ili mateso yao ya ndani yakayazidi ya wale wadhulumiwa.
Watapata stroke na kisukari na watakosa hata walezi. Watakua na mwisho mbaya sana
 
Basi gombea uraisi 2025 ukishinda utuletee katiba mpya
Wananchi tuandae ilani yetu. Ni ilani ya wananchi. Wananchi tuseme kuwa, tutampa kura mgombea ambaye anaahidi kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya ndani ya siku zake 100 za mwanzo.
 
Hao ni marais wa CCM wanaojutia kuwadhulumu wapinzani.
Wanajutia hasa. Bahati mbaya ni kuwa Muumba wetu huwachoma nafsini mwao ili waune uovu walioutenda nyakati ambazo walikuwa na uwezo wa kutenda kitu.
 

Gambo: Ulikuwa uporaji shughuli ya kufunga maduka ya kubadilisha fedha za kigeni​

Tuesday June 15 2021​

Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo amesema shughuli ya kufunga maduka ya kubadilishia fedha za kigeni iliyofanyika nchini takribani miwili iliyopita, ilikuwa ni uporaji wa kuumiza watu.



By Habel Chidawali
More by this Author

IN SUMMARY​

  • Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo amesema shughuli ya kufunga maduka ya kubadilishia fedha za kigeni iliyofanyika nchini takribani miwili iliyopita, ilikuwa ni uporaji wa kuumiza watu.


Advertisement
Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo amesema shughuli ya kufunga maduka ya kubadilishia fedha za kigeni iliyofanyika nchini takribani miwili iliyopita, ilikuwa ni uporaji wa kuumiza watu.

Akizungumza jana Jumatatu Juni 14, 2021 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa bajeti kuu ya Serikali, Gambo amedai mchakato huo ulikuwa kama nia ya baadhi ya watumishi wa Serikali kutaka wafanye wao biashara hiyo.

Novemba 20, 2018 maduka zaidi ya 20 yalifungwa jijini Arusha baada ya ukaguzi uliofanywa na maofisa wa Serikali wakishirikiana na vyombo vingine vya dola.

Aprili, 2021 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga alisema kati ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni 87 yaliyofanyiwa ukaguzi jijini Dar es Salaam, 82 yalikutwa na viashiria vya utakatishaji wa fedha.

Katika maelezo yake, Gambo ambaye amewahi kuwa mkuu wa Mkoa Arusha amedai Serikali ilikuwa ikipandisha viwango vya mitaji kwa lengo la kutaka wafanyabiashara washindwe lakini walipoendelea kufanya biashara zao waliona hakuna namna zaidi ya kuvamia.

"Mlichukua fedha zao, magari, viwanja vyao na mali nyingine watu wakabaki hawana kitu hivi lengo la Serikali ilikuwa nini," amesema Gambo.

Gambo amezungumzia pia sekta ya Utalii akisema imeachwa kabisa bila kuwekewa mkakati katika bajeti jambo ambalo ni hatari kwa uchumi wa nchi.

Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imeshindwa kubuni mbinu ya kuvutia ili kuongeza watalii badala yake imefikiria kuongeza tozo inayoweza kusababisha watalii kupungua nchini.

"Hii bajeti imeacha kabisa kutaja sekta ya utalii, wenzetu wanafikiria kuvutia watalii sisi tunawaza kuongeza tozo, mnawaza nini nyie," amehoji Gambo.

Ametolea mfano wa kupungua kwa watalii kwamba kumesababisha baadhi ya wawekezaji kupunguza gharama kwenye mahoteli yao kutoka Dola 200 za Marekani hadi Dola 100.
 
Kanuni au utaratibu wa kutubia ni hivi...
Unaacha dhambi kisha unajutia kwanini umefanya dhambi halafu unanuia kutorudia tena dhambi hiyo na mwishowe...

Kama dhambi hiyo ilihusika na kuzuia au kukatili haki ya mtu basi sharti haki hiyo irejeshwe

Mambo matatu hayo na hilo la mwisho yanakuwa manne, ndiyo yanahesabika sasa mtu amejutia makosa yake

Sasa tujiulize wewe na mimi, ni nani ametimiza hilo sharti la nne tangu uanze kusikia wakijutia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom