Marais nane Afrika kuhudhuria miaka 50 ya uhuru Desemba 9 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marais nane Afrika kuhudhuria miaka 50 ya uhuru Desemba 9

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Dec 2, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  02 DECEMBER 2011  Na Rachel Balama

  MARAIS nane kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), na Makamu wa Rais wa tatu, wamethibitisha kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 9 mwaka huu.

  Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari na Waziri Mkuu Bw.
  Mizengo Pinda, ilisema maadhimisho hayo yatafanyika katika Uwanja wa Uhuru ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.

  Alisema alitoa mialiko kwa viongozi haoili kujumuika na Watanzania kusherehekea
  miaka 50 ya uhuru ambapo mbali ya viongozi hao, pia kutakuwa na makamu watatu wa Rais pamoja na wawakilishi 16.

  Taarifa hiyo iliongeza kuwa, Rais Kikwete pia ametoa mialiko kwa viongozi wa kitaifa waliopo madarakani, wastaafu na vyama vya siasa kwa Wenyeviti na Makatibu Wakuu.

  Alisema mialiko maalumu imetolewa kwa wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Taifa, wazee mashuhuri kutoka mikoa mbalimbali, baadhi ya Wenyeviti na Makatibu wa chama tawala.

  Akizungumzia mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2011, Bw. Pinda alisema zimetumika kama sehemu ya maadhimisho hayo kuelezea mafanikio ya Serikali baada ya kuwashwa na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kijiji cha Butiama, mkoani Mara.

  Alisema ujumbe wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka huu unasema "Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi Kusonga Mbele" na kusisitiza kuwa mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, dawa za kulevya na rushwa pia ni sehemu ya ujumbe huo.

  Mkesha wa maadhimisho hayo utakuwa Desemba 8 mwaka huu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.Pamoja na shughuli mbalimbali zitakazofanyika siku hiyo, pia kutakuwa na gwaride ambalo limeandaliwa na Vikosi ya Ulinzi na Usalama pamoja na onesho la zana mbalimbali za kivita.

  Alisema pia kumeandaliwa halaiki maalumu ya wanafunzi wa shule
  za msingi 4,550 na wanafunzi wa shule za sekondari na wahamasishaji 2,000.

  Sherehe hizo pia zitapambwa na ngoma za asili za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 9 mwaka huu.

  Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari na Waziri Mkuu Bw.
  Mizengo Pinda, ilisema maadhimisho hayo yatafanyika katika Uwanja wa Uhuru ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.

  Alisema alitoa mialiko kwa viongozi hao ili kujumuika na Watanzania kusherehekea
  miaka 50 ya uhuru ambapo mbali ya viongozi hao, pia kutakuwa na makamu watatu wa Rais pamoja na wawakilishi 16.

  Taarifa hiyo iliongeza kuwa, Rais Kikwete pia ametoa mialiko kwa viongozi wa kitaifa waliopo madarakani, wastaafu na vyama vya siasa kwa Wenyeviti na Makatibu Wakuu.

  Alisema mialiko maalumu imetolewa kwa wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Taifa, wazee mashuhuri kutoka mikoa mbalimbali, baadhi ya Wenyeviti na Makatibu wa chama tawala.

  Akizungumzia mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2011, Bw. Pinda alisema zimetumika kama sehemu ya maadhimisho hayo kuelezea mafanikio ya Serikali baada ya kuwashwa na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kijiji cha Butiama, mkoani Mara.

  Alisema ujumbe wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka huu unasema "Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi Kusonga Mbele" na kusisitiza kuwa mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, dawa za kulevya na rushwa pia ni sehemu ya ujumbe huo.

  Mkesha wa maadhimisho hayo utakuwa Desemba 8 mwaka huu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.Pamoja na shughuli mbalimbali zitakazofanyika siku hiyo, pia kutakuwa na gwaride ambalo limeandaliwa na Vikosi ya Ulinzi na Usalama pamoja na onesho la zana mbalimbali za kivita.

  Alisema pia kumeandaliwa halaiki maalumu ya wanafunzi wa shule
  za msingi 4,550 na wanafunzi wa shule za sekondari na wahamasishaji
  2,000. Sherehe hizo pia zitapambwa na ngoma za asili.   
 2. HT

  HT JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  uhuru wa taifa non existent!
  Wasting resources!
   
 3. J

  John W. Mlacha Verified User

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  uhuru wa taifa gani?
   
 4. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  sherehe ya siku moja, matayarisho Billioni 50 TSH. Tanzania ni nchi ya ajabu kweli
   
 5. R CHUGGA

  R CHUGGA Senior Member

  #5
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Haya mi napita tu!nikielewa unachozungumzia nitarudi kujumuika nanyi
   
 6. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Haya ni matumizi ya hovyo ya fedha za walipa kodi. Nawapongeza Marais 16 (?) waliotuma wawakilshi badala ya kupotteza muda wao kuja kwenye usanii.

  Nataraji baada ya shughuli zote hizi Serikali (kwa hiari au kwa kulazimishwa na Wabunge waadilifu) itatoa taarifa ya matumizi ya fedha (gharama za maadhimisho) zote zilizotumika na nini maana yake.

  Haya mambo ya kukosa vipaumbele yanatufanya kitu mbaya!
   
 7. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,159
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye RED, Mkesha Mnazi mmoja, hapa sio uhamasishaji wa Mapambano ya Ukimwi bali uhamasishaji wa KUENEZA UKIMWI. Kuna haja gani ya kuwakusanya watu usiku kucha. HAMASISHENI WATU KUCHUKIA UFISADI NA KUJENGA NCHI YAO, Sio kukesha kwa matukio ya miaka 50. Watu wakusanyike mchana Uwanja wa Uhuru na sio kuhamasisha mikusanyiko ya usiku.

  Halafu hapo kwenye BLUE. Inaelekea ajira ya watoto mnaiendekeza sana nyie. Mnawezaje kupambana nayo?

  Kwa ujumla mipango yenu sio mizuri na ni UFISADI mwingine kwa rasilimali za Taifa
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa rais mwenye akili zake timamu hawezi kuja kusheherekea miaka 50 isiyokuwa na hata chembe ya maendeleo huku tukiwa na resources kibao. Pia kutumika garama kibao huku walim na wafanyakazi kibao wakiwemo wazee EAC hawajalipwa huku serikali ikifanya matumizi makubwa kwa vitu visivyokuwa na msingi
   
 9. Kisiya Jr.

  Kisiya Jr. Senior Member

  #9
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna mengi tumefanikiwa jamani,pamoja na mapungufu yote ila ni vema tukajipongeza japo kwa kidogo tulichopata. We were not static in 50 yrz there iz a considerable stage. Natambua ufisadi uliopo,embazlement,un proportionate of resource,poor education, infrastructure and dependance we face in time. Tujipongoze kwa miaka 50 ya uhuru umepata vyama vingi ikiwepo CHADEMA ambacho ni tumaini la WATZ wengi kwasasa. MOTO YETU IWE ; TUMEJARIBU, TUFANYE NINI TUSONGE MBELE.
   
 10. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Tatizo langu ukiondoa gharama kubwa inayotumika kwaajili ya tukio hili la mara moja,ninatatizwa na kitendo cha serikali kualika kwenye sherehe hizo wajumbe wote wa Halmashauri kuu ya CCM kwa gharama ya nani? Sherehe za miaka 50 ya Uhuru wala si ya CCM bali ni ya Tanganyika. Lazima tutofautishe shughuli za chama na za serikali na si sahihi kualika wajumbe wote wa CCM na kuwahudumia kwa malazi na posho as if wanakuja kwenye kikao cha NEC.

  Lakini naamini kwa dhamira njema kabisa kama 50 billion ndiyo iliyotengwa kwa shughuli hii basi hatujui vipaumbele vyetu.Ingekuwaje kama sherehe hizi zingefanyika kwa say kuzindua Meli ya Kisasa katika Ziwa Nyasa iliyonunuliwa kwa sehemu ya pesa hiyo!
   
Loading...