Marafiki!!!

Asante Lizzy, Rafiki ni mtu wa thamani sana na ndio maana tunatakiwa kuwa makini na mtu tunayemwita rafiki na kumtambulisha kama rafiki. Kwani kuna watu wanatumia loop ya kutambulishwa marafiki baadae wanakuchafua na unaonekana na wewe ni hivyoulivyo. Utasikia aah, kwanza yule jamaa nimejuana naye juzijuzi tu! Why tunawatambulisha kama marafiki while we don't know them? A real Friends are always there for you .
 
well said lizzy, wakati mwingine marafiki ni wa msaada kuliko hata ndugu. tatizo linakuja kama mkijakorofishana halafu akawa hana busara na uvumilivu kama ulivyosema, anatumia siri zako zote kuwa silaha za kukuangamiza.

Hapo pabaya sana!Inabidi watu tujifunze kutokua na visasi vya kitoto!Hapo ndo ukomavu wa akili unapohitajika!
 
Hivi inakuwaje wakati mwingine inatokea mtu unakuwa na marafiki unawathamini sana,ukisikia anaumwa unaenda kumwona , kama wana shughuli kama harusi unachanga, matatizo kama unaweza kumsaidia unamsaidia, ila inapokuja wewe unahitaji rafiki yako hawakufanyii kama wewe unavyowafanyi? haya yananipata mimi kwa marafiki zangu wa kike karibu wote. au ndio mambo ya tenda wema uende zako
 
Hapo ndo unajua wanakujali kiasi gani....but then kuna watu wamejaliwa ubinafsi kwao kumfikiria mtu mwingine ni mwiko!!Kwahiyo wanaweza kua hivyo.
 
Mkuu sana Lizzy! Urafiki ni must uwe proportion na muda na terms za urafiki ziwe wazi unless otherwise tuna tafsiri tofauti za urafiki...kumeet na mtu na kushabihiana vitu viwili vitatu hakutoshi kumfanya mtu kuwa rafiki..muda wa kufahamiana na chimbuko la wahusika vinamatter as well
 
Huo nao unatafsiriwa kama urafiki na sio kosa kwasababu hiyo nayo ni level moja wapo.
Ndo maana unakuta mtu anakwambia ahhh yule rafiki yangu tu...yule ni rafiki yangu wa kawaida na huyu ni rafiki yangu haswa.
Nwyz tatizo linakuwepo pale mtu ambae hujawahi kukaa nae chini akitegemea umfanyie kitu ambacho ni sahihi kwa rafiki haswa ila sio rafiki wa mambo...poa!!!

Labda kama tungekua na maneno mengine yanayoweza kutumika kama ambavyo unasikia mtaani watu wakiitana washkaji and the likes maana yale yanatofautiana kulingana na level!!!
 
Lizzy,umegusa pazuri sana!..ila honestly when it cam e to friends,i gave my all!too bad i was not that lucky kwakua wengi hawakua waaminifu and did not treat me right!..but i thank God for the ones i have,especially my mum!..ubarikiwe dear!
 
Asante mpendwa!!!Mara nyingi kweli inatokea wewe uko tayari kwa lolote kwa rafiki yako wakati yeye haoni umuhimu wako!!!Pole mwaya....but atleast you got your mama!!!
 
Nimesema labda ni kichwa changu kigumu ama vipi...maana in fact mimi binafsi kununa si moja ya tabia yangu,najua kukaa na watu ktk moments tofauti tofauti na marika as well...tabia hii imenifanya kuwa na so called marafiki wengi sana! Of whom kwao nimejifunza mengi kuliko wao walivyojifunza kwangu(nina ushahidi)...kwa uzoefu nilionao kwenye elimu ya mtaani nasoma viashiria tofauti vichwani mwa hawa 'marafiki' zangu! Kuna walioenda beyond scope (kimtazamo wangu) hawa ni wale km si kuwa mseminari mmmh em ngoja kwanza! ndo maana nadhani ili mtu kukidhi urafiki ni must kuwe na terms na conditions of which km si kushuka sign basi msome terms husika na ziwe mwongozo kwenu! Hii itasaidia pale mmoja atakapoipua jambo ambalo halikua kwenye mkataba tokea kwanza...yes! Kwako mkuu Lizzy
 
Lizzy asante sana kwa hii topic umenikumbusha mbali sana nilikuwa na marafiki baadae tuligombana kwa mambo ya kijinga nasema ya kijanga kwa sababu unapokuwa na wivu kwa ajili ya maendeleo ya mwenzako na kuaanza kuzusha maneno ya uongo sio vizuri
umeniongezea uelewa zaidi wa kuchagua marafiki
BE BLESSED
 
Ushauri mzuri sana Lizzy....ila nakubaliana na Miss Judith kuwa marafiki hawachaguliwi....mara nyingi unakuwa na urafiki na mtu kutokana na circumstances/situations/interests au kufanana kwa tabia fulani fulani,umri,mawazo,hobbies au ukaribu etc.
 
Michelle, natafuta marafiki sasa....
 
Asante sana Lizzy,

Hivi siku hizi wewe una upako? Naona kila mara unapakua vitu vyenye kuletA afya mu-kichwa!
 
I love you Lizzy ..
Hii Topic yako imenifanya nitafakari mengi sana be blessed ,Nimemkumbuka rafiki yangu ambaye mungu alimpenda zaidi ya mie nilivyompenda
Kila nikiwaza chozi linanitoka .
Pole sana FirstLady1. Kama ulivyosema, Mungu alimpenda zaidi. Yeye hutoa na Yeye huchukua.
 
Urafiki unakuwa na "hatua", zinazoanza tangu siku mnakutana hadi mnafika wakati kila mmoja wenu anahisi moyoni kuwa "huyu ni rafiki yangu wa kweli". Tusichanganye baina ya watu tunaowajua kwa sababu ni majirani, tunafanyakazi nao pamoja, tunakutana nao vilabuni, mikutanoni, mitaani na marafiki wa kweli. Wote hawa mnakutana, mnaulizana, na wote wana umuhimu wao ingawa hatuchangiani nao kila kitu. Ikifika hatua ya kuchangiana naye mambo muhimu kwa mfano anakuwepo wakati unamhitaji japo kwa mawazo au kukusikiliza, anakusaidia unamsaidia, anakuliwaza unamliwaza bila ya kudai kurejeshewa fadhila, huyu ndie rafiki wa kweli. Kwa rafiki wa kweli hakuna "commitment" wala makubaliano, bali ushindani wa kutendeana mema.

Inaemekana, rafiki wa kweli anakuwa kama kioo chako. Unajiangalia na unajirekebisha ufane naye, na yeye ndio hivyo hivyo. Ndio mana katika kundi la wahuni si rahisi kumkuta asiyekuwa mhuni, na kama yumo, anajifunza kuwa kama wao kwani ndivyo anavyotaka awe.

Pamoja na yote, urafiki kama mapenzi vinabaki kuwa vitu vya mjadala kwani ni mahusiano baina ya mtu na mtu.
 
Ushauri mzuri sana Lizzy....ila nakubaliana na Miss Judith kuwa marafiki hawachaguliwi....mara nyingi unakuwa na urafiki na mtu kutokana na circumstances/situations/interests au kufanana kwa tabia fulani fulani,umri,mawazo,hobbies au ukaribu etc.

Dearest you can always choose who you want around and who you don't!!Inawezekana kabisa kwamba we normally don't choose from the begining ila baadae hua inatokea unaamua kutokua rafiki na mtu tena kutokana na kutofautiana.Ndo maana kuna watu hata wewe unaweza kusema yule alikuaga rafiki yangu....au wakasema wewe ulikuaga rafiki yao.Binafsi marafiki niliokua nao mwanzo wa mwaka huu sio wote wanaendelea kua marafiki zangu....kweli unakutana na mtu mnaanza kua marafiki ila ikitokea ukaona tofauti zenu haziwezi kua pamoja unampotezea au anakupotezea!!!Hapo unakua umechagua kutokua rafiki na mtu au unachagua kuendelea baada ya kuona mnafaana!!!
 
Hapo pabaya sana!Inabidi watu tujifunze kutokua na visasi vya kitoto!Hapo ndo ukomavu wa akili unapohitajika!

Nakubaliana na wewe kabisa. Naona ile sredi ya michelle inachambua behavior pattern, which may compliment with this one of yours.
 
Back
Top Bottom