Marafiki wanavyoweza kukuzuia usifanikiwe

Marafiki wanavyoweza kukuzuia usifanikiwe

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,956
TAFITI za kitaalamu zinaonesha kuwa, tabia za watu hujengwa na ndugu, marafiki au mazingira yanayowazunguka kila siku. Hii ina maana kwamba kama tutakuwa na marafiki au ndugu walikata tamaa ya maisha upo uwezekano mkubwa wa kuathirika kisaikolojia.
Imebainika kwamba hata wanaume na wanawake wanaojiingiza kwenye uhusiano wa mapenzi wengi wao ni wale ‘walioathirika’ na kukutana kwao kila siku kwenye mazingira wanayoishi.

Bila shaka wewe msomaji wangu unaweza kufanya utafiti wako na kugundua kuwa asilimia 80-90 ya wanandoa uhusiano wao ulianza wakati wakiwa pamoja shuleni, kazini au mtaani. Ukweli huu unaweza kuwa msingi wa somo hili juu ya athari za marafiki kwenye maisha yetu.


Ikumbukwe kuwa maisha ni mipango lakini si kila kitu tunachopanga kinakuwa kimetokana na juhudi zetu za kufikiri. Wajuzi wa elimu ya maisha wanasema, asilimia kubwa ya mipango na tabia ya mwanadamu ni ya kuambukizwa kutoka upande wa pili unaomzunguka.


Wengi wetu tunaambukizwa kutumia vinywaji fulani si kwa sababu tulipanga kuvitumia, lakini mawazo yetu yalitekwa na matangazo kwenye runinga na redio yaliyokuwa yanatushawishi bila sisi wenyewe kujua na tukajikuta siku moja tunaamua kunywa.


Hii ina maana kwamba, mtu mmoja tu mwenye mawazo ya kushindwa, aliyekata tamaa anatosha kabisa kutuondolea shauku ya kufanikiwa, endapo atapata nafasi ya kutueleza kila mawazo yake ya kukata tamaa.


Naamini ndoa nyingi zinavunjika siku hizi kwa sababu, baadhi ya wanawake/wanaume wanatoa nafasi kwa marafiki zao kuwapandikizia udhaifu.

“Mumeo hafai ni mhuni sana, anakutesa. Mkeo mbaya hamuendani naye mkitembea hampendezi.”


Kwenye maisha haya tunaishi na marafiki hatari sana wanaotuambia kuwa hatuwezi kufanikiwa kwa sababu hatujasoma, hatuna mitaji ya biashara au serikali haijaweka fursa za vijana kuendelea. Watu wa aina hii tupo nao kila siku kazini na huko kwenye makazi yetu, wanatulisha hali ya kukata tamaa bila sisi wenyewe kujitambua.


Wengine wanatuvunja moyo wa kufanya kazi kwa bidii kwa kutuambia: “Kwenye kampuni yetu tunafanya kazi sana, halafu mshahara mdogo.” Kwa kuwa tumewapa nafasi ya kutuambia na sisi tunawasikiliza taratibu tunajikuta tunachukia kazi na kuona ni bora kuacha.


Naamini vijana wenzangu mmeacha kufanya vitu vingi kwenye maisha yenu kwa sababu rafiki zenu waliwavunja moyo. Tumeacha wapenzi wetu kwa ushawishi wa wengine, tumeuza viwanja, tumejiingiza kwenye tabia mbaya, tumekata tamaa kimaisha kwa sababu ya ndugu zetu.

Kwa msingi huu, natoa ushauri kuwa kila mtu anatakiwa kuwa makini na rafiki aliyekata tamaa.
 
date mtu nayemfahamu? No way! Strangers for Life

sema kusikiliza maneno ya watu juu ya mtu uliye na mahusiano naye inaweza kukukata stimu kabisa.
 
Kweli uliyosema ktk topic hii maneno ya vijuweni ukiyafuata una lost kweli
 
hiyo ni kweli maana kunawengine kwa vile maisha yao ni magum basi waja kwako kukukatisha tamaa wewe
 
Naamini vijana wenzangu mmeacha kufanya vitu vingi kwenye maisha yenu kwa sababu rafiki zenu waliwavunja moyo. Tumeacha wapenzi wetu kwa ushawishi wa wengine, tumeuza viwanja, tumejiingiza kwenye tabia mbaya, tumekata tamaa kimaisha kwa sababu ya ndugu zetu.
Kwa msingi huu, natoa ushauri kuwa kila mtu anatakiwa kuwa makini na rafiki aliyekata tamaa.

MziziMkavu leo umelonga................si waswahili husema.........."Kikuumacho ki nguoni kwako?" Chwa kamwe hawezi kukung'ata kama hayumo ndani ya nguo zako mwenyewe.............it is so obvious.....
 
kwa kweli!!! wanaopenda wenzao wasifanikiwe ni wengi haswa kama wao yao hayaendi!
marafiki watoa ushauri ni wengi, inabaki kuwa juu yako kufanya maamuzi. kwa maisha yetu ya sasa ni bora kujifunza kuwa na masimamo.
 
usiombe ukutane (dating) mwanamke aliyeumizwa ujanan au aliyeteswa na mumewe anamaneno machungu kama nyoka mwenye sumu!!
 
Ikumbukwe pia ndege hao hawapendi kuona mwenzao anawazidi mbio so inatakiwa kuwa makini sna na hawa marafiki na ndugu,nakumbuka rafiki yangu kipenzi aliacha kuongea nami kisa nimepata kazi nzuri yeye bado ,mpaka na leo hii tangu2009 wafananao huruka pamoja na hamna mtu anataka
 
Back
Top Bottom