Marafiki wana msaada kuliko ndugu

Maisha yako ni jukumu
👉Kila kitu katika maisha yako ni jukumu lako
👉changamoto zinazokukabili ni jukumu lako kulitatua

💥umaskini usiwe chanzo cha makasrikiko na kukataa ndugu.

Epuka kua tegemezi kwa maana hata marafiki nao wanahitaji marafiki
Ndugu watabaki kua ndugu marafiki watabaki kua marafiki

kutoa au kupokea msaada sio sheria bali ni huruma na imani ya mwanadamu na ni optional

Ahsante🙏
 
Mkuu marafiki wameset future za watu wengi sana hivo kusema wanasaidia shida ndogo ndogo ni uongo.

Imagine mtu anakupambania upate mchongo fulani akati unao ndugu wenye nafasi za kukupatia michongo kirahisi bt kila ukiwacheki wanakupanga tu.

Binafsi ktk zama hizi umuhimu wa ndugu upo nyakati za misiba na magonjwa pekee.
 
Kwani Ndugu hawezi kuwa rafiki na Rafiki akawa ndugu ?

Nadhani tatizo ni sense of entitlement kuna mambo akikufanyie ndugu unachukulia poa (kama vile ni haki yako) ila mshikaji wa kawaida unaona ni zaidi sababu sio obligation...

By the way hao marafiki waliokusaidia wewe hawana ndugu ? Na je wanasaidia ndugu zao au waliacha kuwasaidia ndugu wakakusaidia wewe ?

Just trying to show you a different perspective
 
Kuna huu mfano nilisimliwa nikiwa mdogo. Kwamba jamaa mmoja alitaka kujua ndugu yake na rafiki nani anaweza kuwa naye wakati wa shida. Hivyo, siku moja alimchinja mbuzi, kisha akamfunika shuka nyeupe. Ilipofika usiku, akaenda kwa rafiki yake, akamwambia "nimeua mtu na naogopa muda wowote naweza kukamatwa." Akamwambia kwamba anamwomba waende kuvuta mwili wa yule aliyeuliwa na kuutupa porini ili polisi wasije wakamhusisha kwamba amemuua mtu. Baada ya kusikiliza simulizi zima, rafiki yake akaona hilo ni kosa la ninai, hivyo akishiriki kuuvuta mwli wa huyo aliyeuliwa kwenda kuuficha porini, mambo yakifichuka naye atakuwa kwenye hatia. Kwa kuona hivyo, akamwambia huyo rafiki yake kwamba huo ni msalaba wake mwenyewe, asimwingize kwenye matatizo maana familia yake inamtegemea. Jamaa baada ya kuona hivyo, akaenda kwa ndugu yake (brother) akasimulia kisa kizima cha kuua kama alivyofanya kwa rafiki yake. Ndugu yake akamwambia hilo ni tatizo kubwa, na kwamba asingeweza kumwacha ndugu yake kwenye tatizo kama hilo alibebe peke yake. Hivyo, alikubali kwenda kumsaidia kubeba maiti kwenda kutupa porini. Walipofika sehemu husika huyo ndugu mtu akafunua shuka na ndugu yake huyu akakuta siyo mtu, bali ni mbuzi. Yule aliyedai kamuua mtu akamwambia "sasa naamini damu ni nzito kuliko maji, na kwamba ndugu yako hawezi kukuacha uingie kwenye matatizo." Ni simulizi linalofikirisha, lakini halitoi jibu linalofanana kwa watu/ndugu wote.
 
Uongo ,marafiki watakuwepo kama wananufaika au wana mategemeo ya kunufaika na wewe,
Ndugu atakiwa na wewe kwa hali zote,kuwa makini hakuna watu wanafki kama marafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…