Mara ya mwisho kusema neno 'I love you'

Mara ya mwisho kusema neno 'I love you'

KORBOTO

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2014
Posts
1,848
Reaction score
2,447
Wanaume walikuwa kwenye semina wakaulizwa,mara ya mwisho kumwambia mkeo unampenda ni lini? Wengine wakasema leo asubuhi,wengine muda sio mrefu.Muwezeshaji akawaambia kila mmoja sasa hivi amuandikie mkewe sms amwambie nakupenda mke wangu halafu badilishaneni simu kila mmoja asome majibu ya mwenzake.

Majibu yalikuwa hivi:

1. Unaota au?❓❓

2. Umekumbwa na nini?❓❓

3. ??!! Makubwa!❗❗❗

4. Utanieleza hii sms ulikuwa unamtumia nani❗❗

5. Leo sikusamehi najua kuna kitu.

6. Huyo ulienae ndo kakwambia unitumie hii sms?❗❓❓

7. Najua tu tayari kuna kitu umeharibu.

8. Wewe sema unachotaka.

9. Leo hunipati ng'o!❗❗

10. Nani mwenzangu❓❓

Mwanamke yupi alitisha hapo?Mi nimecopy pahala nikaona si vibaya nanyi mtoe maoni yenu.
 
hiyo ya 11 kabla ya kuisoma ya 13 kuna namba 12 na 14 zimenivunja mbavu zangu kweli....hahahahahaha!!!
 
4 na 10 zinaniachaga hoi sana,, by the way ni human nature kukinai
 
mi kwangu na7 ndo iliua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom