EEX
JF-Expert Member
- Oct 19, 2014
- 4,130
- 13,380
Nimezaliwa katika familia duni mkoani Shinyanga.Nilifeli darasa la saba,mbaya zaidi nikafeli vibaya mno kidato cha nne (Elimu ya watu wazima, alimaarufu masomo ya jioni). Wakati nikisubiri matokeo, bibi yangu anayekaa Mwanza aliniomba nikamtembelee wakati nikisubiri matokeo.
Niliondoka na salfeti langu kama la Ommy Dimpoz,lenye fulana niloyamalizia shule, Kasuruali pamoja na lifulana lingine jeusi lililopauka ambalo lilikuwa na shingo pana yakutosha kupitisha vichwa vya watu watatu (nilikuwa nikiipenda sana nguo hii). Nilipokelewa vizuri sana na baada ya kufika nyumbani, niliandaliwa maji ya kuoga, kisha nikaambiwa nijongee sebuleni kupata chakula.
Kufika mezani nilikuta hotpot tatu, sahani za udongo na vibakuli, 1 Ilikuwa na ugali laini mkubwa kiasi, 2 ilikua na nyama iliyokuwa inanukia vizuri mno, 3 ilikuwa na mchicha wenye mapambo (karoti).
Nilichofanya nilichukua mchicha nikachanganya na nyama, nikauchungulia ule ugali nikuona naumudu peke yangu bila usaidizi. Nikautwanga wotee, nikabuguia nyama zotee na mchicha. Vikabaki vimchuzi mchuzi nikainua hotpot nikavinywa.
Kabla sijaweka hotpot chini,mjukuu wa kike wa yule bibi akaingia,nikasikia akiambiwa "P chakula kiko mezani muachieni mjomba na dada".
Jicho lilinitutumka kama kitenesi, chakula cha mtu tatu nimekiteketeza alone, aibu gani hii. Nililoa jasho la fedheha, nikawa mdogo kama punje ya ufuta.
Je wewe ni masahibu yapi yalikukuta ugenini?