Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,110
Hodi hapa jamvini! Nimepita pita mara nyingi jukwaani MMU,nimegundua kuna watu wanateswa na mapenzi lakini majuto mengi sana hutoka jinsia ya kike. Mara nyingi nimeshuhudia wanawake wakitulaumu wanaume eti, "Wanaume hawatulii, wanaume hawaaminiki, wanaume wana tamaa sana n.k" Na wanaume nao vivyo hivyo wanalaumu, "Wanawake wanapenda vidumu, wanapenda pesa, wanapenda nywele kuliko mume n.k" Leo nataka nipate reflections za wanawake na wanaume walio na experience kuhusu polygamy. Je, umewahi kujaribu kuchunguza japo kidogo moyo wa mwanamke (mwanamke mwenza) anapokabiliwa na polygamy? (Mume mmoja, wake wengi). Je, umejaribu kufikiri kinachotokea moyoni kwa mke mmoja pindi mumewe anapolala na mke mwenza? Nani amepata kujiuliza hisia za mwanamke alipata menopause pale Mumewe anapoamua kuoa under 23 yrs old? Kwanini ni rahisi kwa Mwanamke kuvumilia haya?
Last edited by a moderator: