Mapya yaibuka kuungua kwa soko la Samunge Arusha

Waziri2025

Senior Member
Joined
Sep 2, 2019
Posts
149
Reaction score
380
Mapya yaibuka kuungua kwa soko la Samunge Arusha.

Na, Mwandishi wetu, Arusha

Siku chache mara baada ya soko la Samunge lililopo jijini Arusha kuteketea kwa moto taarifa za ndani zimebainisha ya kwamba soko hilo lilichomwa maksudi kwa sababu za kisiasa.

Ingawa mpaka sasa jeshi la polisi mkoani Arusha limedai kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme lakini taarifa za uhakika zinaeleza kwamba kiongozi mmoja wa serikali mkoani Arusha kwa kushirikiana na vijana walipanga kuchoma moto huo kwa sababu za kisiasa.

Hatahivyo, mfanyabiashara ambaye chanzo cha moto huo unaotajwa kuanzia kibandani kwake inasemekana haijulikani mahali alipo mpaka sasa pamoja na kusakwa na vyombo vya dola.

Taarifa za uhakika zinantaja mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwamba ndiye mhusika aliyepanga njama mwanzo mwisho kuchoma soko hilo kwasababu za kisiasa.

Gambo anayetajwa kuwania ubunge wa jimbo la Arusha Mjini katika uchaguzi mkuu mwaka huu anadaiwa kuwatumia baadhi ya vijana wa CCM (majina yanehifadhiwa) kwa lengo la kuchoma moto kwenye soko hilo.

Gambo, ambaye alifanya ziara ya kutembelea soko hilo jana na leo ambapo ameonekana akilakiwa na wananchi mbalimbali anadaiwa kuandaa mpango kabambe wa kuhakikisha anashangiliwa kwa nderemo katika soko hilo.

Baadhi ya vijana wanaodaiwa kuandaa mpango wa kuhakikisha kiongozi huyo anashangiliwa katika ziara hiyo ni pamoja na katibu Tarafa kata ya Elerai, Tito Cholobhi sanjari na katibu hamasa wa Uvccm Wilayani Arusha Mjini, Abraham Mollel ambao wanadaiwa kuwapanga wananchi katika eneo hilo muda mfupi kabla ya Gambo kutinga eneo hilo.

Vijana hao wanadaiwa kumwaga fedha kiasi cha sh, 2000 kwa kwa wananchi mbalimbali huku lengo likiwa ni kuhakikisha mkuu huyo wa mkoa anashangiliwa pindi akiwasili katika eneo hilo.

Licha ya serikali kupiga marufuku mikusanyiko Kama njia mojawapo ya kupambana na ugonjwa hatari wa Corona lakini Gambo Jana alionekana akiwa na wananchi mbalimbali huku akipena mikono kitendo ambacho kimelaaniwa vikali na watu mbalimbali.

Huku akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM mkoani hapa akiwemo Mwenyekiti wa mkoa Stephen Zelothe mkuu huyo wa mkoa alionekana akisindikizwa na wakinamama huku wakimwita "Mbunge "Mbunge "jambo ambalo linatajwa kama kampeni za ubunge wa jimbo la Arusha Mjini.

Katika eneo hilo Gambo aligawa jumla ya Mabati 700 na kuwahaidi kuwasaidia wakinamama ambao watajenga vibanda vyao katika soko hilo kama njia mojawapo ya kujisafishia njia ya ubunge mwaka huu.

Hatahivyo, taarifa za ndani zinadai ziara hiyo ililenga kumhujumu mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni na mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro ambao amekuwa na tofauti nao kwa nyakati tofauti kwa lengo la kuwafanya waonekane hawafanyi kazi jijini hapa.

Katika ziara yake Gambo alitamka kwamba kuna baadhi ya viongozi jiijini Arusha wana mpango wa kuwaleta matajiri wachukue eneo la soko hilo huku akiwalenga Dk Madeni na Daqaro ambao walifika awali mara baada ya moto huo kuibuka na kutangaza mkakati wa kuliboresha kwa kiwango soko hilo ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu rafiki kwa watumiaji wa soko hilo kama vyoo, njia za kupita na mitaro ya maji.

Hatahivyo, cha kushangaza katika ziara aliyoifanya Gambo Jana na Leo hakuambatana na Dk Madeni na Daqaro jambo ambalo limeibua sintofahamu kubwa jijini Arusha.

Gambo akiambatana na Zelothe Leo walifika katika eneo hilo na kuanza shughuli ya kugawa maeneo kwa wafanyabiashara hao huku wakishangiliwa kama njia mojawapo ya kujijenga kisiasa bila kuzingatia usalama wa eneo hilo.

Mwisho.
IMG-20200403-WA0077.jpeg
IMG-20200402-WA0019.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli anaujua Mungu LAKINI:
Leo nilikuwa naongea na mtumishi wa manispaa na aliniambia haya;
1. Tangu soko liungue wao kama watumishi waneteseka sana kwa kupokea masgizo yanayopingana kutoka kwa watendaji wakuu.
2. Walipewa maelekezo kuaandaa michoro na hatimaye gharama ya ujenzi, wajenge sawa na soko lavKrokoni.
3. Jana mkuu wa mkoa alisitisha kila kitu na kutaka soko lifunguliwe muda ulele bila kujengwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Yaani muandishi was hii habari ameweza kutaja live Nina LA Mkuu was Mkoa lakini majina ya Vijana anaosemekana kushirikiana kuchoma solo Majina yao Yamehifadhiwa..! Upuuzi Mtupu...!
 
Mapya yaibuka kuungua kwa soko la Samunge Arusha.

Na, Mwandishi wetu, Arusha

Siku chache mara baada ya soko la Samunge lililopo jijini Arusha kuteketea kwa moto taarifa za ndani zimebainisha ya kwamba soko hilo lilichomwa maksudi kwa sababu za kisiasa.

Ingawa mpaka sasa jeshi la polisi mkoani Arusha limedai kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme lakini taarifa za uhakika zinaeleza kwamba kiongozi mmoja wa serikali mkoani Arusha kwa kushirikiana na vijana walipanga kuchoma moto huo kwa sababu za kisiasa.

Hatahivyo, mfanyabiashara ambaye chanzo cha moto huo unaotajwa kuanzia kibandani kwake inasemekana haijulikani mahali alipo mpaka sasa pamoja na kusakwa na vyombo vya dola.

Taarifa za uhakika zinantaja mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwamba ndiye mhusika aliyepanga njama mwanzo mwisho kuchoma soko hilo kwasababu za kisiasa.

Gambo anayetajwa kuwania ubunge wa jimbo la Arusha Mjini katika uchaguzi mkuu mwaka huu anadaiwa kuwatumia baadhi ya vijana wa CCM (majina yanehifadhiwa) kwa lengo la kuchoma moto kwenye soko hilo.

Gambo, ambaye alifanya ziara ya kutembelea soko hilo jana na leo ambapo ameonekana akilakiwa na wananchi mbalimbali anadaiwa kuandaa mpango kabambe wa kuhakikisha anashangiliwa kwa nderemo katika soko hilo.

Baadhi ya vijana wanaodaiwa kuandaa mpango wa kuhakikisha kiongozi huyo anashangiliwa katika ziara hiyo ni pamoja na katibu Tarafa kata ya Elerai, Tito Cholobhi sanjari na katibu hamasa wa Uvccm Wilayani Arusha Mjini, Abraham Mollel ambao wanadaiwa kuwapanga wananchi katika eneo hilo muda mfupi kabla ya Gambo kutinga eneo hilo.

Vijana hao wanadaiwa kumwaga fedha kiasi cha sh, 2000 kwa kwa wananchi mbalimbali huku lengo likiwa ni kuhakikisha mkuu huyo wa mkoa anashangiliwa pindi akiwasili katika eneo hilo.

Licha ya serikali kupiga marufuku mikusanyiko Kama njia mojawapo ya kupambana na ugonjwa hatari wa Corona lakini Gambo Jana alionekana akiwa na wananchi mbalimbali huku akipena mikono kitendo ambacho kimelaaniwa vikali na watu mbalimbali.

Huku akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM mkoani hapa akiwemo Mwenyekiti wa mkoa Stephen Zelothe mkuu huyo wa mkoa alionekana akisindikizwa na wakinamama huku wakimwita "Mbunge "Mbunge "jambo ambalo linatajwa kama kampeni za ubunge wa jimbo la Arusha Mjini.

Katika eneo hilo Gambo aligawa jumla ya Mabati 700 na kuwahaidi kuwasaidia wakinamama ambao watajenga vibanda vyao katika soko hilo kama njia mojawapo ya kujisafishia njia ya ubunge mwaka huu.

Hatahivyo, taarifa za ndani zinadai ziara hiyo ililenga kumhujumu mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni na mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro ambao amekuwa na tofauti nao kwa nyakati tofauti kwa lengo la kuwafanya waonekane hawafanyi kazi jijini hapa.

Katika ziara yake Gambo alitamka kwamba kuna baadhi ya viongozi jiijini Arusha wana mpango wa kuwaleta matajiri wachukue eneo la soko hilo huku akiwalenga Dk Madeni na Daqaro ambao walifika awali mara baada ya moto huo kuibuka na kutangaza mkakati wa kuliboresha kwa kiwango soko hilo ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu rafiki kwa watumiaji wa soko hilo kama vyoo, njia za kupita na mitaro ya maji.

Hatahivyo, cha kushangaza katika ziara aliyoifanya Gambo Jana na Leo hakuambatana na Dk Madeni na Daqaro jambo ambalo limeibua sintofahamu kubwa jijini Arusha.

Gambo akiambatana na Zelothe Leo walifika katika eneo hilo na kuanza shughuli ya kugawa maeneo kwa wafanyabiashara hao huku wakishangiliwa kama njia mojawapo ya kujijenga kisiasa bila kuzingatia usalama wa eneo hilo.

Mwisho.View attachment 1408032View attachment 1408033

Sent using Jamii Forums mobile app
Ubunge kwa Arusha asahau..
 
yaani wanapewa sh.2000 kushangilia?!
Waarusha wamekuja kuwaje aisee!
 
Dah!.. haya madaraka haya......

Kama ni kweli kama mwandishi anavyodai yaani mkuu wa Mkoa anatofautiana na DC wake na mkurugenzi wa jiji, je huo Mkoa wanauendeshaje?
 
Tabu tupu best kwa kifupi uroho wa madaraka itawatokea puani hawa maccm🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻
 
Back
Top Bottom