salimkabora
JF-Expert Member
- Nov 10, 2012
- 2,441
- 651
Wana jf kuna kituko nimekutana nacho leo hii ingefaa mnijuze kama na nyie mnakutana nacho na pia tushauriane kuhusu dawa ya jambo husika. Ishu ni kuwa mwanangu anasoma darasa la pili shule binafsi VIBE kinyerezi na tegemeo ni kuingia darasa la tatu wakifungua; cha ajabu nimekabidhiwa ripoti ya mtoto inayosema shule ikifunguliwa atarudia darasa na kusoma hilo hilo la pili kwa kuwa hakufikisha wastani wa marks 70 walizojipangia. Imeonyeshwa nafasi yake darasani ni wa 16 na kwa maana hiyo nusu ya darasa watakuwa wanarudia kwa kuwa darasa lina wanafunzi karibia ya thelasini. Sasa hii maana yake nini ni kwamba sasa tujiandae kuona watoto wanamaliza la saba wakiwa na miaka 20 au 21 umri sawa na ule wa wale wanaokaribia kumaliza chuo kikuu. Hapo sasa na umri huo apate bahati ya kuingia sekondari na hizo rudiarudia atapoteza miaka mingine 12 hapo umri utakuwa miaka 33; sasa aende chuo aje kuingia kwenye maisha atakuwa ameshakuwa m-babu wa miaka 50. Hivi hii wizara ya elimu kazi yake nini hadi kila mjinga mwenye vijihela vya kufungua shule anaanzisha ujinga anaoujua yeye? Hivi hawa kina MULUGO na elimu zao za kuungaunga ndio wamekuwa majanga kiasi hiki? huyu mtoto wangu yuko bright na namkubali hata faili lake lina marks kuanzia 80 kwenda juu lakini sizo zilizowekwa kwenye ripoti; na hapa nyumbani anategemewa na watoto wenzake tena wa darasa la tano wa shule za serikali anawafanyia hesabu, na kuwajibia masomo mengine pia lakini yeye arudie mwaka wakati wanafunzi wake wanasonga mbele kuingia la sita. Hivi hapo darasa la saba si wanafanya mitihani ileile ya kwenda sekondari? na utaratibu wa kurudia madarasa si ni darasa la nne na form two? hii ya kurudishwa nyuma darasa lolote ili watu wavune pesa imeidhinishwa na nani? MULUGO? hebu nijuzeni wenzangu!