Mapya kwenye gmail | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapya kwenye gmail

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kilongwe, Aug 4, 2010.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Source: AfroIT

  Je una akaunti ngapi za google? Inakuwaje endapo mtoto,mke au rafiki yako anataka kutumia google
  akaunti yake kwenye kompyuta yako bila kutoka kwenye akaunti yako? Google imesikiliza kilio
  chetu. Na sasa ipo njiani kukamilisha moja ya feature ambayo itamuwezesha mtumiaji kusign in kwenye
  akaunti zaidi ya moja kwa pamoja. Binafsi nimeipenda sana hii feature kwani itaokoa muda
  sana,fikiria zamani ulitakiwa kusign out kwenye akaunti moja kabla ya kusign in akaunti nyingine
  pindi utumiapo kompyuta moja.


  Kulingana na mfumo wa sasa,unaweza kusign in kwa kutumia akaunti mbili tu,moja ni akaunti ya
  google na nyingine ni akaunti ya Google Apps.Hii ya kwanza mfano ni gmail na hii ya pili ni kama
  kwa wale wanaotumia google applications kama google ads,madevelopers nk.

  Utata ambao upo ni kuwa hadi sasa huwezi kusign in kwenye akaunti binafsi zaidi ya moja,kwa mfano
  kuna mtu wana akaunti za gmail zaidi ya moja,pindi atumapo e mail anataka kuchagua atume hiyo e
  mail kutumia akaunti ipi.Kuna sababu nyingi za kutumia akaunti zaidi ya moja,kwa mfano unaweza
  kutumia moja kwa ajili ya mambo ya kikazi na nyingine ikawa kwa ajili ya mambo ya kifamilia
  vilevile nyingine kwa ajili ya kazi za online,kwani kama tulivyowahi kudokeza umuhimu wa
  kutofautisha akaunti kulingana na matumizi husika.

  Baada ya kusikiliza malalamiko toka kwa wateja wake,google wameamua kuja na hii kitu mpya ambacho
  kwasasa kipo kwenye makamilisho na majaribio,kazi ikikamilika,baada ya kusign in kwenye akaunti yako utakuwa
  na uwezo wa kuchagua akaunti mbalimbali kulingana na matumizi yako binafsi hivyo kazi itakuwa
  rahisi zaidi.

  Binafsi bado haijatokea kwenye akaunti yangu ingawa kwenye mitandao wameshatuma picha ya jinsi
  itakavyokuwa,inafanana sana na ilivyo kwenye qq(mtandao mkubwa na wenye watumiaji wengi
  China),kwani hawa jamaa wa qq walishakuwa na hii feature miaka kibao huko nyuma kama
  inavyoonekana kwenye picha.

  [​IMG]


  Ili kuweza kufaidi , unatakiwa kwenda kwenye Google Account page, halafu ukubali kulogin kwenye
  akaunti zaidi ya moja - Kwa sasa hii feature bado ipo njiani. Google wanasema mambo mazuri zaidi
  yaja.
  Usikose kutembelea AfroIT kwa mada mbalimbali za ICT zinazowalenga waswahili kwa 100%.
   
 2. A

  Audax JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  itatusaidia saana hii wadau. Alafu naomba mnisaidie -kuhusu kupost thread wakuu
   
 3. T

  Taso JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Technical information flawed.

  Kwanza, si kweli kwamba huwezi kufungua multiple accounts za gmail kwenye computer moja, ila kwenye browser moja. Ukifungua, kwa mfano, account moja kwenye mozilla, nyingine kwenye google chrome, itapeta.

  Pili, si lazima kusubiri gmail walete hiyo service au hilo kampuni la kichina la qq. Service tayari ipo kwa Microsoft Exchange, ambayo ndio ina lion's share kwenye soko la mail handling kwenye corporate environment.

  Tatu, hiyo feature itakuwa na udhaifu muhimu. Kwanza, haifanyi kazi kwenye mobile devices, a major dissapointmet kwa sababu e-mailing nyingi siku hizi, personal and business-related, zinafanywa kwenye mobile devices kama smartphones na tablet gadgets. Pili hata kwenye PC ukiiwasha ina disable google services offline, kama google calender and gmail.
   
Loading...