Google Yaonya Watumiaji wa Gmail Kuhusu Mashambulizi ya Wadukuzi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,096
Reaction score
7,128
Kampuni ya Google imewataka watumaji wa huduma ya baruapepe ya mtandao ya Gmail kuwa makini kwani kuna kundi la wadukuzi wanaozilenga akaunti hizo baada ya kufanikiwa kuiba taarifa.

Google imesema watumiaji wa huduma hiyo wanaofika zaidi ya bilioni mbili duniani kote wasijibu ujumbe zinazowataka kutoa nywila za (Password), za akaunti zao Gmail.

Google imesema kuwa ni asilimia 36 pekee ya watumiaji huboresha nywila mara kwa mara. Hii inamaanisha wengi wako hatarini. Hivyo kutokana na hilo Google imewataka watumiaji wa huduma hiyo kubadili nywila zao (Password), ili kuwa salama zaidi.

Kupitia taarifa zilizochapishwa kwenye akaunti za mitandao ya Forbes, Google Cloud na MSN, Google imethibitisha wadukuzi walifanikiwa kuingia kwenye akaunti za Gmail na kwamba nywila walizoiba ndiyo chanzo kikuu cha uvamizi wa kimtandao unaoendelea.

Shambulio hilo la kundi la wadukuzi la ShinyHunters, pia wanaojulikana kama UNC6040 lilianza Juni 2025 likitumia mbinu kadha wa kadha. Kwa mujibu wa Google Threat Intelligence Group (GTIG), wadukuzi walijifanya wafanyakazi wa IT ambapo walipiga simu kumshawishi mfanyakazi wa Google akubali programu hasidi iliyounganishwa na Salesforce hatua iliyowapa uwezo wa kunakili maelezo ya mawasiliano, majina ya biashara na taarifa husika.
 
Wamejiwahi hapo ma engineer wako site kuhakikisha hakuna upenyo 😂😂
 
Kwaiyo unashauri tubadilishe password kw mara nyingine
 
Back
Top Bottom