Mapya kuhusu Bashe: Masha anatumikia rais gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapya kuhusu Bashe: Masha anatumikia rais gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Sep 15, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]Ndugu Wana-JF: katika gazeti la Mwanahalisi la leo kuna hii makala ya Saed Kubenea (Uk wa 10) ambayo nimejaribu kuweka hapa sehemi yake kubwa tu. Makala inaibua mapya kuhusu namna wajumbe wa Baraza la Mawaziri (cabinet) ya JK walivyokuwa na utii (loyalty) katika sehemu mbili. Kwa maneno mengine kuna ‘cabinet' nyingine kivulini (isiyo rasmi) ambao inachota utii kutoka kwa baadhi ya mawaziri wa JK. Nimejaribu ku-highlight sehemu husika:[/FONT]

  Kitendawili cha uraia wa Hussein Bashe, mgombea ubunge Nzega (CCM) aliyoenguliwa kimeibua mapya.

  Wiki iliyopita, Waziri wa mambo ya Ndani, Lawrence Masha aliutangazia ulimwengu kuwa Bashe ni raia halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Akahoji, "nani mwenye mamlaka ya kusema Bashe si raia? Nikiwa waziri mwenye dhamana nasema, Bashe ni raia halali na hakuna atakayebadilisha uamuzi huu."

  Aliyesema kuna utata katika uraia wa Bashe ni Rais Jakaya Kikwete, tena ndani ya vikao halali vya chama chake.

  Taarifa zinasema, ndani ya ukumbi wa mkutano Kikwete alisimama kidete kutetea hoja yake kwamba Bashe si raia. Alisema amepata ‘taarifa za vyombo vya usalama' zinazothibitisha utata wa uraia wa Bashe.

  Wengine walioendeleza kauli ya rais ni viongozi wakuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Katibu Mkuu Yusuf Makamba na Katibu Mwenezi John Chiligati.

  Masha amenukuu vifungu kadhaa vya sheria ya uhamiaji akisema vinahalalisha uraia wa Bashe.

  Kwa mfano, ananukuu vifungu Na. 5(1) na Na. 7(8) vya Sheria Na. 7 ya uraia ya mwaka 1995 na kusema, "Bashe ni raia halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tena kwa kuzaliwa." Anasema tayari amemjulisha Bashe kuhusu uamuzi huo.

  Je, Masha hakushauriana na Kikwete, Makamba na Chiligati kabla ya kutoa uamuzi waliofikia? Kama walishauiriana, kwa nini wanaanika ngua zao za ndani hadharani?

  Kama walishauriana, kipi kinachompa ujasiri Masha hadi kuamua kupigana na mwamba? Nani aliyemhakikishia usalama wake kisiasa na kimasilahi?

  Akiongea kwa kujiamini, Masha alisema kwa mujibu wa nyaraka zilizopo na taarifa zilizofikia wizara yake. "….suala la uraia wa Bashe halina utata."

  Katika maelezo yake, Masha anasema Bashe ni raia halali wa Tanzania, tena wa kuzaliwa. Hili nalo lina utata. Hata Bashe anajua hilo; kwamba si raia wa kuzaliwa.

  Masha anajua kuwa wakati Bashe anazaliwa, baba yake mzazi alikuwa hajaomba uraia. Alikuwa raia wa Somalia. Alipoomba uraia wa Tanzania, hakumuingiza Bashe katika maombi aliyowasilisha katika fomu zake za kuomba uraia.

  Aidha, Bashe mwenyewe amekana uraia wa Somalia akiwa na miaka 25.

  Kama haya ndiyo maelezo ya Bashe, kwamba baba yake alipoomba uraia hakumuingiza yeye katika maombi yake; hiki ambacho Masha anaita "Bashe raia wa kuzaliwa" kinatoka wapi? Kinalenga nini?

  Kama Bashe hakuzaliwa Tanzania, na baba yake hakuzaliwa nchini na hata wakati anaomba uraia, Bashe akiwa na miaka kumi; nani basi raia wa kuzaliwa? Je, Masha amelenga nani na kwa faida ya nani?

  Kama Kikwete anasema Bashe si raia, huku Masha anasema tofauti, nani aaminike na yupi apuuzwe? Inawezekana Masha anajua vema nani anamtumikia, lakini siyo rais Jakaya Mrisho Kikwete na serikali yake.

  Ingekuwa Masha anamtumikia Kikwete, waziri na rais wasingepanda gari moja, lakini wakaelekea tofauti. Ama watateremka na kila mmoja aende zake, au mmoja atabaki kwenye gari.

  Lakini ukiyatafsiri vema haya utayafupisha kwa kauli hii: Kikwete ana serikali mbili. Zipi? Serikali anayozunguka nayo na nyingine iliyo kivulini.

  Katika nchi zote ambako rushwa imekomaa na ufisadi umekuwa dini, dola linakuwa na sura mbili. Serikali mbili, mabunge mawili na mahakama mbili.

  Kunakuwa na waasi wasioonekana kama majini ya Sheikh Yahya Hussein. Wanabaki kivulini.

  Watatenda bila kuafikiana na wanaishi kwa kuviziana na kuzomeana. Hatimaye aliyeko kivulini anaangusha serikali iliyo wazi na iliyochaguliwa.

  Wakati siyo rahisi kujua Masha yumo katika serikali ya dola lipi, katika hali ya kawaida, asingeweza kwenda kinyume na Kikwete, kama asingeweza kuwa na uhakika wa usalama wake kisiasa………..

  ……..Uamuzi wa masha wa kujitosa kumtetea Bashe, hata kwa kauli zenye utata, unachukuliwa na wengi kuwa njia ya kuonyesha kuwa ana msuli wa nje kuliko wa ndani ya serikali ya Kikwete…….
   
 2. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Ningeongeza na "Idara za Usalama mbili"
   
 3. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  hachana na kubenea ameishiwa siku hizi, sasa alitaka masha awe mnafiki kwa kutimiza matakwa ya mkuu wake wa kazi kwa kunyanganya haki ya uraia wa mtu
   
 4. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #4
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Anawatumikia RA and EL + Mzee wa Meli
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hili lisisiemu bana! mautumboo tuuu!!
   
 6. K

  Kijana Mkweli Member

  #6
  Sep 15, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha umbumbu ndugu yangu...ni ukweli ulio dhahiri kwamba Kikwete alidanganywa(misinformed) at first hand kuhusu uraia wa bashe...na masha kama waziri wa mambo ya ndani yeye ndie mwenye mamlaka ya kutoa 'confirmation' kuhusu uraia wa bashe...post yako hapo juu haina kichwa wala miguu...tafadhali usiharibu dhana ya jamii forums kua ni home of great thinkers...ACHA UMBUMBU NA MAJUNGU...LOOSER
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kutokana na makala hiyo, picha inayojitokeza ni kwamba Masha anatumikia 'cabinet' ya EL na RA. Na ndiyo wanaompa nguvu, hasa ikizingatiwa kuwa Bashe ni mtu wa RA. Sioni picha nyingine hapa.
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,346
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  pamoja na hayo bashe hawezi kwenda mahakamani kwani anajua ulikuwa ni mradi wa kikwete kutekeleza mamlaka ya mwanae rtiziwani ambaye alikuwa na bifu na bashe.............hii ndiyo tz.......mtoto wa rais naye ni rais...........mke wa rais halikadharika pia ni rais........tumeisha km tusipobadili uongozi na kumkana kikwete
   
 9. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,784
  Likes Received: 6,269
  Trophy Points: 280
  Masha na Kikwete wanajua kinachoendelea.

  Masha alikuwa wapi siku zote? siku ile walipomvua uraia Bashe kwa nini Masha ahkuja juu siki hiyo hiyo na kusema anayoyasema sasa, kama kweli yeye ndie mwenye dhamana ya kuhalalisha uraia wa mtu
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Siafiki hivyo. Masha sasa ni project ya kumuingiza EL mjengoni mwaka 2015. Huo mradi wa vitambulisho ilikuwa uwaingizie mabilioni kufanikisha azma hiyo ingawa hii sasa inaonekana kukwama.
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nchi imeuzwa
  kila kitu holela mpaka maisha yetu yapo kwa DALALI akisubiri wateja
   
 12. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2010
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  (1) Masha Kapinga kauli ya Chairman wa CCM sio Rais
  (2) Wote hawajui Sheria: hata bila kukana Uraia Bashe ni Raia as he was Born in TZ, kama angetaka Uraia wa Somalia ndo angeukana wa TZ, au kama wazazi wake wangekuwa wabongo then yeye akazaliwa somalia alipaswa kuukana wa somalia ili apate uraia wa TZ.hivi kama angekaa kimya ina maana angekuwa hana Uraia wa nchi yoyote??
  (3)Bashe wa Rostam vs Ridhwan Kikwete wote "dugu moja" na sote tunajua ndugu wakigombana shika jembe ukalime.
  (4) Huo ni mtindo wa CCM KUTUFANYA tujadili minor issues na kuacha issue muhimu

  (5) Kubenea ameanza "kutia Tembo maji " awe anafanya uchunguzi, Bashe ni mzaliwa wa Tanzania.
   
 13. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mie naona wa kulaumiwa hapa ni Rais Kikwete kwa umbumbu wa kutojua ni wapi apate taarifa sahihi iwapo Bashe ni raia ama la sasa ile Wizara aliiunda ya nini kama haitumii kupata uhalali wa uraia wa Bashe.....Tangu lini Makamba na Chiligati wakawa ndio wanaothibitisha uraia wa mtu nani kawapa mamlaka hayo ? Kupotoshwa kwingine ni kwa uzuzu tu.
   
 14. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Toka kadhia hii ianze mie bado najiuliza Masha anapata wapi balls za kuelezea kitu ambacho bosi wake kasema...Big Noooooooo,haiingii akilina hata kama wewe ni waziri bado unabaki mdogo kwa Rais wako na kuna dipolomasia ya kujibu endapo unaona mkuu wako kakosea lakini sio hadharani kama anavyofanya Masha, jambo hili nafikiri JK kashika makali na jamaa wameshika mpini hivyo wanafanya wanavyotaka, fikiria kama angekuwa Nyerere kweli angethubutu kuropoka ujinga ule, No naona kuna namna ambayo sisi wengine hatuioni lakini time will tell us,
   
 15. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Hayo yalikuwa ni masuala ya CCM na Makamba alikuwa akifanya kazi yake kama katibu wa CCM, kama ulidhani hii ni umbumbu basi nina wasiwasi na uelewa wako maana kwa mtu makini masuala yote haya ni mipangilio na kwa wanaomfahamu Bashe na historia yake CCM waliona hili kabla ya kura za maoni.
   
 16. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180

  It sounds & makes sense!
   
 17. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 512
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Nadhani hukuchukua muda kusoma vizuri hoja. Ni nini basi maana ya raia wa kuzaliwa ili kuondoa utata?Au hujui kuwa kuna aina mbalimbali za uraia? Make Masha anadai Bashe ni raia wa kuzaliwa na wakati huohuo Bashe anakubali kuwa wakati baba yake anaomba uraia wakati huo akiwa na miaka 10 hakumjumuisha yeye. Sasa sijui ilo neno (highlighted one) ulilo lituia litamrudia nani?
   
 18. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #18
  Sep 15, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwako unaejiita Kijana Mkeli. Wewe ndio Mbumbu ndugu yangu, Hiyo post kama alivyo anza amekwambia ame quote kutoka kwenye gazet la Mwanahalisi na emetushirikisha kama member, wewe hukua na mamlaka ya kumuhukumu kuwa ni mbumbumbu kuliko wewe. Pia dhana yetu nyingine ni KUFICHA UJINGA NA KUONYESHA HEKIMA ZETU. swali kwako sasa, Wewe una uhakika gani kwamba kikwete alikua misinformed?!.
   
 19. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Chili-gati + Makamba + Masha wote ni ma-spin dokta wa CCM wakiwa chini ya mkulu JK.!

  Huo mchezo mchafu ulichezwa ili kutimiza adhma yao ya kumng'oa huyo Bwashe lawama baadaye. Sasa Masha anafanya coverup tu ya tukio zima wadanganyika wengi hawawezi kuelewa kirahisi mambo haya, lakini ndio siasa zilivyo..:sleepy:
   
 20. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Mkuu Songoro,

  Angalia vizuri tafsiri yako juu ya kipengere no. 2 hapo juu. Kwa tafsiri yangu sio lazima uzaliwe kwenye nchi husika ili uwe na uraia wa nchi hiyo. Kwa mfano kama mtoto akizaliwa na raia wa Somalia na yeye anakuwa na uraia basi Bashe alikuwa na uraia wa Somalia hata kama yeye hakuwahi kukanyaga kule hata siku moja. Na ilikuwa sawa kwa yeye kuukana uraia wa Somalia baada ya kufikisha miaka 18.

  Ila Kubenea naye anachemsha, huyo babake Bashe angemwingiza kwenye maombi yake wakati Bashe tayari alikuwa ni raia? Bashe ni raia wa kuzaliwa kupitia upande wa mamake. Hivyo wakati babake anaomba uraia Bashe alikuwa tayari ni raia.

  Labda mjadala pekee hapa ni lini unaruhusiwa kuukana uraia mwingine baada ya miaka 18? Je ni siku hiyo hiyo unafikisha miaka 18 au kuna muda maalumu? Kama upo ni siku/miezi/miaka mingapi baada ya kufikisha miaka 18?

  Huko mbeleni hii sheria itakamata watu wengi sana.
   
Loading...