Mapungufu ya zoezi la ukaguzi wa vyeti vya kugushi

Aurora

JF-Expert Member
May 25, 2014
7,308
5,270
Natumaini ni wazima humu ndani,
Naomba Mungu taarifa nilizozisikia zisiwe za kweli maana hadi moyo unaenda mbio, eti hili zoezi la ukaguzi wa vyeti feki, wanaitisha cheti cha muhusika original na copy alafu wana verify ile copy kwa kuangalia ile original na kui sign/ ku stamp.

Kwanini wasichukue vyeti husika na kuwasiliana na chuo/shule aliyosoma muhusika, wahakikishiwe kweli alisoma pale,kipindi hicho na taaluma hiyo, bila kumuhusisha muhisika kwenye hiyo process.

Mungu ibariki Tanzania
Muwe na siku njema
 
Kuna shida gani akihusika mwenye cheti, ili akibainika hapo hapo alambe adhabu yake on the spot!
 
Mkuu usijali ata viongozi wako wanavyo piga kazi ila badilika Fanya kazi kama unafukuzwa kesho jijenge kiuchumi
 
Zoezi linavyoenda kama una cheti fake hiyo siku utatokeza,uliza wakuambie waliokaguliwa jinsi zoezi lilivyo kali.Nafikiri awamu ya kwanza ni mahali pa kazi awamu ya pili nafikiri itakuwa nikupitia taarifa ya chuo na tasisi aliyosoma muhusika kulinganisha alichowasilishia wakati wa kukaguliwa na chuo alichosoma,kuanzia elimu ya form four mpaka chuo cha muhusika kwa walio foji ukigusa tarifa za form four na chuo unamdaka hapo hapo maana majina yatakuwa ayafanani najaribu kuwaza tu nakuota itakuwa hivyo.Nafikiri umefika wakati sasa TCU na NACTE wawe na tarifa za graduate wa vyuo vyote vya Tanzania vile vinavyotambuliwa.
 
Nchi nyingine ukiomba kazi either kwenye application form au CV ukiwawekea elimu yako na mwaka uliohitimu, baada ya short listing HR wanawasiliana na chuo ulichowaambia. Siku ya internteriview unaona copy ya result transcript iko mbele yako.
 
Natumaini ni wazima humu ndani,
Naomba Mungu taarifa nilizozisikia zisiwe za kweli maana hadi moyo unaenda mbio, eti hili zoezi la ukaguzi wa vyeti feki, wanaitisha cheti cha muhusika original na copy alafu wana verify ile copy kwa kuangalia ile original na kui sign/ ku stamp.

Kwanini wasichukue vyeti husika na kuwasiliana na chuo/shule aliyosoma muhusika, wahakikishiwe kweli alisoma pale,kipindi hicho na taaluma hiyo, bila kumuhusisha muhisika kwenye hiyo process.

Mungu ibariki Tanzania
Muwe na siku njema
Ajira nyingi niza Degree na Diploma, Je unaweza kuwa na vyeti fake kuanzia O-level hadi Diploma au Chuo kukuu na vikafana kwa kila kitu? Sijui. Lakini nafikiri wakiangalia taarifa zako na wakiona kuna mashaka ndio wanafuatilia vizuri kwenda NECTA na kwenye vyuo husika.
 
Hapa nilipo presha inapanda na kushuka,naomba anayejua sangoma alipo ili anitengenezee matunguli niepukane kuangukiwa na hil jumba bovu.
 
Kuna shida gani akihusika mwenye cheti, ili akibainika hapo hapo alambe adhabu yake on the spot!
Mmmmmhhhh hili nalo ni tatizo. Hapo mwaka 1993 kuna mtu mmoja aliomba vyeti vyangu vyote viwili vya sekondari na kwenda kulambia ajira katika moja ya taasisi nyeti hapa Tz, mpaka muda huu sijui nini itakuwa hatima yangu. Bhati nzuri mimi si mwajiriwa wa ofisi yyote, niko self employee. What my sake will be.
 
Kuna mtu aliona nachelewa kupata ajira,eti akaja kutaka nimuuzie cheti akapate ajira.Mambo yanaibuliwa,ole wake ningempa aulizwe majina ya walimu na masomo walionifundisha ashindwe kujibu.
 
Ni vema kuthibitisha chuo alichosoma au watu wawili aliyosoma nao maana vyeti feki hutengenezwa Buguruni na sehemu nyingine mfano ni waliyokamatwa Buguruni
 
Ni vizuri watunga sera za elimu wakasoma maoni humu kujua ukubwa wa tatizo na jinsi ya kulitatua.Ukisikia watu wanaitwa majina ya kejeli na dharau kama haya KANJANJA,KISHOKA na K...Z. ujue wana elimu ambazo hazikuendelezwa.Ndiyo hawa wanaoachwa bila muongozo ni wapi wapeleke ujuzi na maarifa waliyoyapata.Mfano utakuta kijana kasoma FIZIKIA kuna shughuli za umeme atakuwa anaweza tu.Mwingine kasoma lugha,zipo shughuli anazoziweza.Watu wanafanya shughuli kulingana na maarifa waliyonayo.Elimu haina mwisho.
 
Ajira nyingi niza Degree na Diploma, Je unaweza kuwa na vyeti fake kuanzia O-level hadi Diploma au Chuo kukuu na vikafana kwa kila kitu? Sijui. Lakini nafikiri wakiangalia taarifa zako na wakiona kuna mashaka ndio wanafuatilia vizuri kwenda NECTA na kwenye vyuo husika.

Usiogope mkuu hutakamatwa kamwe

tatizo ni kutokuwa na mifumo ya taarifa (database) iliyojitosheleza.

taasisi zote za serikali zingekuwa na mifumo ya taarifa zilizojitosheleza ingesaidia.

mf. NIDA, RITA, BRELA, TRA, NECTA, polisi, na Posta (mfumo wa makazi) na taasisi zingne.

NIDA - kutambua makazi na taarifa za raia
wote.

RITA - taarifa za vizazi na vifo

POSTA - anuani na mawasiliano kwa raia wote

POLISI - taarifa za watuhumiwa na wahalifu wote (pamoja na alama za vidole, macho nk)

taarifa zote kwa taasisi hizo zingeweza kuchujwa(sort) ktk idara maalum. ingeleta ufanisi kwa kutumia teknolijia za kisasa.
 
Back
Top Bottom