Mapungufu ya Taarifa ya Utendaji wa siku 78 za Rais Samia Ikulu

Write your reply. Hujatoa ushauri, bali umetoa ukosoaji usio na mantiki.

Hujasoma vizuri kwani kwenye uzi huo kuna hoja na ushauri wa kila lililochunguzwa!! Nakubaliana nae kwa mara 100% kuwa muelekeo wa kutaka kuijenga nchi kwa kutegemea wajomba kutoka nje kutaweka uhuru wa nchi hatarini. Nchi ilikuwa inasisitiza kutumia rasilimali zetu vizuri na kutoka kwenye kutegemea madeni ya benki ya Dunia na IMF; lakini sasa inaelekea msimamo ule umeanza kuyumba na kuendekeza mikopo toka nje kwa maendeleo ya nchi. Tusipokuwa waangalifu muda si mrefu tunaweza kujikuta tunaomba misaada toka nje kulipa mishahara ya wafanyakazi wetu!!!!
 
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa taarifa ya utendaji wa Serikali kwa siku 78 za Rais Samia Suluhu ofisini-Ikulu. Pamoja na mambo mengi mazuri, taarifa hiyo ina mapungufu kadhaa kwa maoni yangu, kama ifuatavyo:

Pia Gerson Msigwa wakati anatoa taarifa hizo akutane na wahariri wa media watendaji (editors in chief au associate editors) na special correspondents, news anchors, feature journalists mahiri na siyo waandishi uchwara wasio na weledi mkubwa zaidi ya habari za udaku ili Msemaji Mkuu wa Setikali ajiandae vizuri kuulizwa maswali kama haya au vipengele hivyo na habari za serikali hatimaye kuandika , kurushwa, kunukuliwa kwa ubora hapa nyumbani na kimataifa pia.

.......................................................

Streamed live on 5 Jun 2021
Ghorofa ya 5, PSSSF House
Dodoma, Tanzania

Msemaji Mkuu wa Serikali na Vyombo vya Habari



Source: MAELEZO TV
 
6 Juni 2021

James Mbatia mwenyekiti wa NCCR - MAGEUZI azungumza na waandishi wa habari


Mkutano wa mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI unazungumzia bajeti itakayosomwa na serikali kwa ajili ya matumizi ya mwaka 2021 /2022 na utaangazia maeneo haya yafuatayo
  1. Uchumi
  2. Deni la Taifa
  3. Ripoti ya CAG 2019/2020
  4. Matukio ya hujuma dhidi ya matumaini mapya ktk taifa letu baada ya awamu ya sita kuingia serikalini.
Source : MwanaHALISI TV
 
Yesu naye akamwambia nenda kavue samaki na mtoe shekeli ulipe kodi kwa ajili yako Petro na mimi pia !
Hivyo!

Sikuwahi kulijuwa hili. Yesu naye alidaiwa kodi?

Lakini itakuwaje amtumikishe Petro, si angeamua tu pesa ipatikane bila jasho?
 
hapa umepatia kabisa; linapokuja suala la ulipaji kodi uhusiano kati ya serikali na mlipa kodi huwa na wa kimabavu, na hiyo ndiyo nature ya uhusiano wenyewe. Mwulize Wesley Snipes, Lauryn Hill, james Brown na cerebrities wengine waliokiuka uhusiano huo baina yao na serikali wakuambie ni nini kilichowapta. Sasa hi Rais wa zamani wa marekani Donald Trump yuko kwenye kiti cha moto kwa sababu ya kushukiwa kuvunja uhusiano huo unaohusu kodi, ni swala la muda tu ataweza kuwaunga mkono akina wesley Snipes.
 
huwezi jitegemea kama huzalishi, huna viwanda, huna bidhaa za kuuza nje, hiyo sahau, Kenya bajeti yao inajitegemea lakipn ni mabingwa wa kukopa
 
huwezi jitegemea kama huzalishi, huna viwanda, huna bidhaa za kuuza nje, hiyo sahau, Kenya bajeti yao inajitegemea lakipn ni mabingwa wa kukopa

Kukopa hakukatazwi lakini kuwe kwa akili!!! Sio kukopa mradi unaambiwa kuna fedha pahala[ IMF au World Banak] wewe unakubali tu kwenda kuchukua!! Kumbuka hizo fecha lazima zilipwe at one point hata kama waliokopa watakuwa wamekufa. Mikopo lazima ichukuliwe strategically kwa shuhuri ambazo zitaelekezwa kuweza kurudisha huo mkopo!!

SELF RELIANCE should be the backbone of our economic policies!!
 
Mama yeye anafikiria kutotoza kodi sahihi ndio unaleta unafuu kwa wafanyabiashara Ila kiukweli ni anakaribisha tu rushwa kwa TRA maana hao ndio watakuwa Miungu watu ili wafanyabiashara wasilipe kodi stahili.
 
Hakuna Kodi ya kulazimishwa, ni wajibu wa kila mfanyabiashara kulipa Kodi kwa maendeleo ya nchi yake, usipotii sheria lazima nguvu itumike, Serikali isiyokusanya kodi ni serikali mfu na hakuna mfanyabiashara anayelipa kodi kwa kubebembelezwa.
Mkuu, huo WAJIBU ndo LAZIMA yenyewe kama vile mfanyakazi wa serikali anavolipa PAYE.
 

Samia unadhan ana akili nzuri yule mama? Akili zKe sio nzuri , ye anataka kuongoza Tanzania kama anaongoza familia yake
 
Kwenye Corona mama awe makini Uganda wimbi limeibuka kwa nguvu na wamechanjwa, shule,vyuo kufungwa.
Atuache tuishi hivyi hivyi tu,hiyo kamati imekopi na kupaste tu.
Hicho walicho pendekeza hata huko Ulaya walisha achana nayo mambo hayo,eti lockdown kulingana na utamaduni wa eneo husika.
Ajabu.
 
huwezi jitegemea kama huzalishi, huna viwanda, huna bidhaa za kuuza nje, hiyo sahau, Kenya bajeti yao inajitegemea lakipn ni mabingwa wa kukopa

Issue hapa ni kuendekeza kukopa wakati nchi ina kila rasilimali ambazo if harnessed intelligently hakutakuwa na sababu ya kukopa!!! Tuliwakamata Barrick kuwa wanatuibia na wataalam wetu wakafanya hesabu na kugundua kuwa tunawadai us$191billion; kitu cha ajabu ni kwamba wajanja wakalipunguza deni mpaka wakakubali kulipwa us$300million!!! Sasa huo ndio ujinga wa watawala wetu; na hiyo ni kwa kampuni moja ya dhahabu, je huko kwingine tunaibiwa kiasi gani?
 
Kwani hizo kodi za kibabe za kukusanya matrilion mbona hatukuona zikiendelea kutangazwa baada ya uchaguzi shida ilikuwa nini Mkuu? Naomba taarifa ya makusanyo nov. 2020 - march 2021... mkataba wa manunuzi ya ndege... ujenzi wa airport ya chattle...na... na...na... kisha tuendelee kujadili.
Vinginevyo YAMEKWISHA... TANZANIA IPO... RAIS NI SSH. KAZI IENDELEE...
 
Kuhusu Corona mama angejifanya hasikii wala haoni kama ilivyo kwa katiba mpya.
 
Acha kupotosha umma bure, Mhe Raisi Samia Suluhu Hassan a.k.a Mama SASHA hajasema tubembeleze walipa kodi la hasa, amesema sheria za kulipa kodi zipo zitumike vizuri. Hii tabia ya kutumia vikosi kazi sio kwa mujibu wa sheria za kulipa kodi kwa mujibu wa katiba, sheria na kanuni zetu. Tatizo la watu kama wewe ni tatizo la kuibuka kwa watu wenye tabia za kikatili katika nchi yetu. Watanzania kwa hulka sio watu wenye ukatili! Umetoa mfano wa nchi ya Spain na hatua zilizochukulia kwa akina Lionel Messi au C. Ronaldo kuhusu kukwepa kodi. Kilichotumika kule ni sheria za kukwepa kodi sio kwamba walipelekewa vikosi kazi! Na hili ndilo analosisitiza Mhe Raisi Samia Suluhu Hassan a.k.a Mama SASHA. Anawahimiza TRA na taasisi zingine zinazokusanya kodi kufuata sheria zilizopo kukusanya kodi na si kwa kutumia matakwa ya mtumishi wa umma. Kwahiyo tuache kumsingizia Mhe Raisi wetu kuhusu mambo ya kiubinadamu anayosisitiza kwa watumishi wa umma kuwatendea wananchi.
 
"samia yeye anakuja na mbinu ya kuwabembeleza walipa kodi"

Nope Nope No.
Her methods ni kodi ilipwe kwa kufuata sheria. sio kubembeleza mtu.
Utawala uliopita ulikuwa aggressive kwenye kodi kiasi kwamba walikuwa hawaziachi biashara za watu salama.
Yes walifanikiwa lakin walikuwa wanaacha trail of distruction nyuma.
 
Samia unadhan ana akili nzuri yule mama? Akili zKe sio nzuri , ye anataka kuongoza Tanzania kama anaongoza familia yake
umenikumbusha rais aliepita aliongoza hivyo hivyo.
lakin hamkusema.

Awe na akil au hana. your views haziwez badilisha chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…