Mapungufu ya Katiba: Tume inataka kufurahisha watu badala ya kutatua matatizo


K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
2,351
Likes
816
Points
280
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
2,351 816 280
Tume ya warioba inajaribu kufurahisha Watanzania zaidi ya kutatua matatizo muhimu ya kiuchumi, kisiasa na hata kiutamaduni. Katiba inatakiwa kujibu swali mmoja tu ambalo ni " Je tutafanya nini ili tuweze kuleta kasi ya maendeleo ya Tanzania tukizingatia utamaduni wetu, usalama na rasilimali?". Kwanini nasema hivi

1. Swala la Muungano: Tume imesema inapendekeza serikali tatu lakini je ni kweli serikali tatu itatatua maswala ya muungano?. Je serikali itakuwa na raisi mmoja na mawaziri wakuu wawili au maraisi watatu. Je Zanzibar itakubali kuendeshwa na waziri mkuu? Kama shughuli zote za kiserikali zitakuwa chini ya maraisi wawili wa chini je raisi wa muungano anaweza kuwa na nguvu ndogo sana kulinganisha na raisi wa Tanzania Bara/Tanganyika!. Je mpango wa tume ni nini kwenye hili. Je tutapunguzaje gharama za serikali wakati tunaona gharama zilivyo kwa sasa.

Ukweli ni kwamba mapendekezo ya serikali tatu si kwasababu ya kutatua matatizo ya wananchi!, si kwamba kuna kazi ambayo hizo serikali zitafanya au kuongeza ufanisi bali serikali tatu zinapendekezwa kwasababu ya kufurahisha pande zote mbili. Sijajua wanamfurahisha nani kwani Watanzania watafurahishwa na maendeleo na sio waheshimiwa.

2. Nishati za madini na Gas: Hakuna hata kipengele za kusema mikataba iwe wazi ingawa Tanzania inaenda kwenye uchumi wa Gas. Sasa kama wakina Warioba hawawezi kufanya hivyo nani atafanya serikali yenyewe au bunge la kisiasa!. Nchi nyingi zinaweka mikataba wazi kwanini wameshidwa hili.

Mifano iko mingi lakini inasikitisha kwamba hawa waheshimiwa wanajaribu kufurahisha zaidi ya kutatua matatizo hata Land haijaongelewa

Hapa inaonyesha hawajali rushwa wala maendeleo ya Tanzania. Hiki kitu kingechukiza mafisadi hivyo wameacha.
 
Bobwe

Bobwe

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2013
Messages
1,241
Likes
10
Points
0
Age
39
Bobwe

Bobwe

JF-Expert Member
Joined May 21, 2013
1,241 10 0
Tatizo watanganyika hamjielewi,kwanza hamjielewi hadi leo kuwa nyie ni watanganyika au watanzania bara?mkifanikiwa kulirejesha taifa lenu la uhuru(tanganyika)basi hakuna mchina wala mzungu atakaeiba rasilimali zenu na mtapiga hatua kimaendeleo,mafisadi wamejificha kwenye chaka la muungano.
 

Forum statistics

Threads 1,274,860
Members 490,833
Posts 30,526,135