Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,731
- 218,312
Nimefuatilia Siku ya Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa , kiukweli haikufana kama ilivyotarajiwa , sielewi hasa kilichotokea , lakini kukosekana kwa Haji Manara kunaweza pia kuwa kumechangia kukosekana ama kupunguza Shamra shamra kwa kiasi fulani , Maulid Kitenge na Zembwela hawakutosha kuongoza shughuli ile kubwa , hawana mvuto , hasa baada ya kashfa ya Mkataba wa Bandari , hawaaminiki tena .
Wako wengine waliodai kwamba Ukubwa wa kiingilio ni sababu muhimu ya uwanja kupwaya , hasa ikizingatiwa anguko kubwa la Uchumi wa Wananchi wa Tanzania na hasa Wakazi wa Temeke , hili Yanga wanapaswa kujifunza , si rahisi kwa mtu aliyeshindia mihogo au chai kavu ya Rangi kulipa kiingilio cha tsh elfu 10 .
Jambo lingine lililodororesha siku ya Mwananchi ni Kukosekana kwa burudani bora ya Muziki , hasa baada ya Wasanii Wahuni kupewa nafasi ya kuimba nyimbo zenye matusi , labda kwa faida ya wengi ni kwamba kwenye kadamnasi kama ile , Burudani ni sehemu muhimu mno , uwanja ule ulikuwa umejaa watu wengi wazima sana , kualika Wasanii Wahuni wanaoimba matusi bila kujali walio mbele yao , kulikatisha tamaa wadau wengi waliokuwa wanaangalia kwenye TV na kuwafanya waendelee kubaki nyumbani , hapa ndipo wanamuziki wa Congo wanapowazidi wasanii wa kibongo , watu wengi wanapenda burudani , hawataki matusi na lugha za hovyo , Kwa hili Yanga Mmefeli sana , mbona bado nchi hii ina wasanii wakali wengi tu , kwanini mmetuletea Takataka hizi leo ?
Wakati mwingine mnapoandaa mambo haya chukueni ushauri wa wadau wa burudani , ukichagua msanii kwa sababu ana followers wengi Instagram au Twitter utapotea .