Mashabiki ni watu wa hovyo sana katika ulimwengu wa soka hasa hapa bongo

mr kipengele

JF-Expert Member
Oct 5, 2022
206
607
Habari za muda huu.

Bila kupoteza muda ngoja niende moja kwa moja kwenye mada , mashabiki wa bongo ni tatizo sana. Jana mnyama kapiga mtu saba kwa moja shangwe limetapakaa kila mahali ,kila mtu anasema Simba ni timu bora makocha wanajua kupanga kikosi.Lakini kesho au kesho kutwa Simba au Yanga zikipigwa magoli ya kufa mtu utasikia hatumkati matola mara Nabi ni kocha wa mchongo lakin akiwapa matokeo huwa mnasahau mapungu ya timu zenu kabisa.

Kuna swala la umri wa wachezaji limezungumzwa hasa kwa upande wa Simba ambao inaonekana ndio kikosi chenye wazee wengi kuliko Yanga lakin baada ya ushindi huu hakuna mwanasimba yeyote aliye laumu uzee wa wachezaji ngoja makundi yaanze kuna matusi ya kila aina hawa wachezaji watatukanwa na hata makocha wataonekana wametoka vichochoroni

Ukija kwa upande wa Yanga nao ni majanga sana timu inacheza kawaida sana lakin mashabiki zake wanavyo vimba mtaani utazani kunakikosi cha maana ,Yanga akifungwa mara moja tu utasikia Kaze hamna kitu Hersi anazingua

Mashabiki hamubebeki kabisa .
 
Hivi ile Kauli kwamba "Tunaoumia Ni Sisi Mashabiki" unadhani kwa muktadha huo atakuwa anapenda timu yake ifanye vibaya?
 
Ulitakiwa unyooshe maelezo. Watu wenye tabia hizo ni mashabiki wa simba! Mashabiki wa Yanga tunasubiria makombe tu.
 
Ulitakiwa unyooshe maelezo. Watu wenye tabia hizo ni mashabiki wa simba! Mashabiki wa Yanga tunasubiria makombe tu.
Mashabiki wa Utopolo mna mambo ya kishetani sana tukianzia na show ya Mama J na hii ya juzi mlipokuwa mnacheza Kangamoko,nyie watu ni chukizo mbele ya Mungu
 
Hivi ile Kauli kwamba "Tunaoumia Ni Sisi Mashabiki" unadhani kwa muktadha huo atakuwa anapenda timu yake ifanye vibaya?
Basi Kama ndio hivyo kwanini hamtaki kusimamia ukweli kwa mfano pale msimbazi ,Simba ikishinda hakuna shabiki hata mmoja utamsikia akisema Mgunda ni chekecheo ,lakin siku Simba ikifululiza ku droo na kupigwa aiseee Mgunda atarudi coastal union asubuh tu mashabiki makanjanja sana sio wachambuzi tu.
 
Kwa hiyo mkuu hata timu ikishinda unataka mashabiki walalamike tu? Hilo litakuwa tatizo, tena ugonjwa wa akili kabisa.
 
Ulitakiwa unyooshe maelezo. Watu wenye tabia hizo ni mashabiki wa simba! Mashabiki wa Yanga tunasubiria makombe tu.
Hapa ni Jambo tu la kusema ukweli sio Simba wala Yanga ,ile siku Yanga imetoka 1-1 na Alhilah afu wakaja Club Africain wakatoka 0-0 aisee matusi yote yalikawa kwa nabimara ooh! Nabi sio professor atoke tu

Mashabiki miyeyusho sana
 
Kwa hiyo mkuu hata timu ikishinda unataka mashabiki walalamike tu? Hilo litakuwa tatizo, tena ugonjwa wa akili kabisa.
Kwann isiwe Kama mbele tu ,Kama timu inahitaji mchezaji Basi atafutwe mchezaji wa kueleweka lakin kwa bongo ni tofauti
 
Nataka niwape Simba wa MSIMBAZI basi hili
1672211135942.jpg
 
Back
Top Bottom