Mapokezi ya Dr Slaa Morogoro na mkutano mkubwa wa hadhara

G

Greenwhich

JF-Expert Member
1,337
1,195
WanaJF

Ni asubuhi tulivu hapa Morogoro na kinachozungumzwa hapa ni ujio wa Katibu Mkuu CHADEMA Dr Wilbroad Slaa anayetarajiwa kuwasili hapa na kufanya mkutano mkubwa sana wa hadhara jioni.

Watu kadhaa wanaonekana wako katika mavazi maalum ya Chadema ya Tshirts na Kombati.

Pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu huyo anatarajiwa kuzungumzia ufisadi mkubwa uliotokea hapa katika manispaa ya Morogoro.

Fuatana nasi kwa Live updates.....

Karibuni.

Updates zaidi

Ratiba itakavyokuwa..

Dr Slaa Rais mtarajiwa wa awamu ya tano atapokelewa kwa maandamano makubwa eneo La Kilakala na kuwahutubia wananchi uwanja wa shule ya Msingi uwanja ndege kuanzia SAA 9 alasiri.

Katika mkutano huo Mkuu wa Idara ya Bunge na Halmashauri CHADEMA Dr Marcossy Albanie ambaye pia ni mtiania wa ubunge jimbo La Morogoro mjini atafukua ufisadi wa zaidi ya bilioni 10 kwenye miradi ya Ujenzi wa Stendi kuu ya mabasi Msamvu 6.6 bn.

Ujenzi wa soko kuu La manispaa 2.6 bn na ubadhirifu miradi ya Maji 1.9 bn ambayo mfadhili wake Millennium Challenge Corporation wamesusia kutoa 1.01 bn zilizosalia na ufisadi mwengine ambapo pia zitatangazwa hatua za kuchukua kabla ya uchaguzi Mkuu.

Updates 2..

Rais Mtarajiwa wa Awamu ya 5 amelakiwa mnamo saa 8 katika eneo la Kilakala kwa msururu mkubwa wa magari ambayo idadi yake haipungui 200.Pia msururu huo ulitanguliwa na Baiskeli na pikipiki zisizo na idadi.Vijana kadhaa walikuwa wamejipanga na mabango yenye maandishi mbalimbali kama Rais wa Wanyonge,Karibu Morogoro utuokoe Baba,Njoo ufukue Ufisadi Msamvu nk..

Dr Slaa ameingia uwanjani mnamo saa 10 na kukumbana na umati mkubwa wa watu huku vikosi vya ulinzi na Usalama vya Red Brigade vikiwa vimejipanga kila kona ya uwanja na kutoa salaam za kipekee wakati kiongozi huyo akipanda Jukwaani.
View attachment 246724
Dr. Slaa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa morogoro na viunga vyake..
Kikubwa alichokizungumza Dr Slaa ni kutangaza Rasmi kwamba UKAWA itakapoingia madarakani itaanza upya mchakato wa Katiba mpya.

Dr Slaa amesema kwamba hiyo ndiyo ahadi yake kubwa kwa Watanzania kwa sababu mchakato wa Katiba umenajisiwa na CCM na maoni yote ya wananchi yalitupwa kapuni na badala yake yakawekwa maoni ya CCM.

Mara baada ya kutoa ahadi hiyo umati wote ulilipuka kwa shangwe kubwa na kuhanikiza anga kwa maneno Rais....Rais...Rais.....Rais.
 
I

Izu

Senior Member
175
0
Mkuu najiandaa kwenda kumpokea mtuu pekee nitakaempigia kura ya ya Rais mwaka huu.
 
I

Izu

Senior Member
175
0
Daktari wa kweli siyo wanaoamini Urais mpaka utoe kafala za watu kwenye ajari.
 

Forum statistics


Threads
1,424,986

Messages
35,078,036

Members
538,184
Top Bottom