Mapokezi ya Dr Slaa kutetemesha Karatu leo

Mapokezi ya Dr Slaa kutetemesha Karatu leo

THE BEST HON DR SLAA akipita mahali lazima vumbi litimke !
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa leo ataanza ziara ya kichama kwenye jimbo la Karatu.

Ziara ya Dr Slaa ni ya kawaida ya kuimarisha chama na kuwanadi wagombea wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji.

Kama inavyokuwa siku zote kiongozi huyo anapozuru Karatu ni kwamba mapokezi makubwa sana yameandaliwa na inatarajiwa shughuli katika mji wa Karatu na viunga vyake kusimama walau kwa masaa 6 kupisha ujio wa kiongozi huyo maarufu zaidi Tanzania.

Katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Jumapili Chadema inatarajiwa kushinda mitaa,vijiji na vitongoji vyote jimboni Karatu kutokana na jimbo hilo kuwa ngome kuu ya Chadema kwa kipindi cha miaka 20 sasa.

Dr Slaa ni mzaliwa wa Karatu na ameongoza jimbo hilo kwa miaka 15 akiwa mbunge hivyo anaporejea nyumbani wanaKaratu wanasema ni mtoto amerudi nyumbani huku vijiji kadhaa vikitoa mbuzi na ngombe kuchinja na kufanya sherehe kwa heshima ya Kiongozi huyo wa kipekee.

Mapokezi katika picha:
10433937_595043210597777_9119763100152042000_n.jpg

10858600_595091103926321_3170641238429547717_n.jpg
10730993_595040857264679_1481196891995176623_n.jpg
10850045_595029290599169_1596058076531025311_n.jpg

Huyu mzee mbona anazidi kuchoka sana!
 
..... Duuh, Wadau Hizo Picha Ni Kweli Au Mume Edit? Daaah, Sijawahi Ona Mapokezi Makubwa Kama Haya.
 
Saa ya ukombozi wa watanzania kutoka ukoloni wa maccm umewadia
2015 ccm itakwenda na maji. Wakaendelee na siasa zao za maji taka
 
..... Duuh, Wadau Hizo Picha Ni Kweli Au Mume Edit? Daaah, Sijawahi Ona Mapokezi Makubwa Kama Haya.

Mkuu hiyo ni sehemu ya mapokezi...Picha nyingine nimeshindwa kuweka hakika ni umati uliotikisa Karatu nzima.
 
Mkuu hiyo ni sehemu ya mapokezi...Picha nyingine nimeshindwa kuweka hakika ni umati uliotikisa Karatu nzima.

Ahsante mkuu kwa picha, itamsaidie Juliana na Mwigulu kujiandaa kisaikolojia.
 
Jamaa kawaingiza kingi akina mwigulu na jamii yake wakaamini kuwa wamempokea katibu wa cdm Karatu! Kapiga hela na amesepa!!!!

kwahiyo jamaa alikuwa mtu wa kawaida?duh hi kali
 
Back
Top Bottom