Mapokezi ya CHADEMA Kigoma Yamshangaza Lema

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, alisema kuwa juzi walipata mapokezi makubwa mjini Kigoma na kwamba kila mtu akiwa katika chama afanye kazi ya kukijenga badala ya kukibomoa.

Alisema licha ya kuwapo na madai kuwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, ana umaarufu mkubwa mkoani humo, jambo hilo halina ukweli.

Alidai mwaka 2010 walitegemea kupata ushindi katika Jimbo la Mpanda, lakini Zitto aliandika barua akieleza kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, awe mgombea pekee.

Alisema baada ya chama kupata taaarifa na kutaka kumwajibisha Zitto, Mwenyekiti Mbowe, aliingilia kati na kusitisha uamuzi huo.

Alisema kutokana na waraka walioukamata aliodai uliokuwa na malengo ya kukisambaratisha chama, waliona hawana sababu za kuendelea na Zitto na kumvua nyadhifa zake na kwamba kitendo cha kuweka pingamizi mahakamani asijadiliwe kinamfanya awe mbunge wa Mahakama.

Alisema mwaka 2000 walikuwapo madiwani 11 katika jimbo la Zitto la Kigoma Kaskazini, lakini mwaka 2005 alipogombea walipungua na kubakia sita na kwamba mwaka 2010 walipungua zaidi na kubakia wawili, hivyo hakuna ukweli kuwa amekijenga chama katika jimbo lake.

Katika hatua nyingine na mwendelezo wa M4C OPD Umati mkubwa wa wakazi wa Manispaa ya Bukoba jana walimiminika kwa wingi katika uwanja wa Uhuru kuwasikiliza Viongozi wa Chadema waliohutubia mkutano wa hadhara.

Kabla ya mkutano huo, yalifanyika maandamano makubwa yaliyokuwa yakiongozwa na vijana waendesha pikipiki.

Source: Nipashe Jumatatu.
 
'''Alisema mwaka 2000 walikuwapo madiwani 11 katika jimbo la Zitto la Kigoma Kaskazini, lakini mwaka 2005 alipogombea walipungua na kubakia sita(6) na kwamba mwaka 2010 walipungua zaidi na kubakia wawili(2), hivyo hakuna ukweli kuwa amekijenga chama katika jimbo lake.'''

Nimenukuu kipengere hiki na kimenivutia kweli kwa maana halisi ZITTO tangu awe Mbunge katika Jimbo hilo CDM imeshuka kwa kasi ya ajabu. na ni vema kwa sasa CDM wakafanya kazi ya ziada kuwarudisha wanachama wake ambao wameondoka CDM kwa sababu ya ZITTO kuwa Mbunge na hili lifanyike kwa kutafuta Mgombea anayefaa na ni chaguo la wanakigoma Kaskazini.
 
Kwa hiyo kumbe Zitto Kabwe naye alikua ni MZIGO!!
 
Mtu mzima anapozungumza inatia hasira huyu molemo haoni aibu kuongea uongo?

'''Alisema mwaka 2000 walikuwapo madiwani 11 katika jimbo la Zitto la Kigoma Kaskazini, lakini mwaka 2005 alipogombea walipungua na kubakia sita(6) na kwamba mwaka 2010 walipungua zaidi na kubakia wawili(2), hivyo hakuna ukweli kuwa amekijenga chama katika jimbo lake.'''

Ebu tupe ufafanuzi juu ya hiki kilichoandikwa hapo juu ni kweli au ni uongo, na kama ni kweli hii kauli yako ya kusema mtu anasema uongo tuieleweje? kwa hiyo wewe ndio utakuwa muongo kwa kutokubaliana na ukweli.
 
'''Alisema mwaka 2000 walikuwapo madiwani 11 katika jimbo la Zitto la Kigoma Kaskazini, lakini mwaka 2005 alipogombea walipungua na kubakia sita(6) na kwamba mwaka 2010 walipungua zaidi na kubakia wawili(2), hivyo hakuna ukweli kuwa amekijenga chama katika jimbo lake.'''

Nimenukuu kipengere hiki na kimenivutia kweli kwa maana halisi ZITTO tangu awe Mbunge katika Jimbo hilo CDM imeshuka kwa kasi ya ajabu. na ni vema kwa sasa CDM wakafanya kazi ya ziada kuwarudisha wanachama wake ambao wameondoka CDM kwa sababu ya ZITTO kuwa Mbunge na hili lifanyike kwa kutafuta Mgombea anayefaa na ni chaguo la wanakigoma Kaskazini.

Usihofu kibogo CDM itasimamisha watu makini na watetezi wa wananchi katika ngazi za Udiwani na Ubunge jimbo la Kigoma kaskazini mwakani.
 
Last edited by a moderator:
huyu mini kabang kaingia ndani ya chama majuzi tu kusaka ubunge leo hii anajiona yeye ndo kakijenga chama kuliko hata wale aliowakuta!!
anasahau kwamba alipokuwa huko alikokuwa hakuna aliyekuwa anamjua zaidi ya wanaAR wachache tu.
vurugu zooote za lema ndani ya chama ni kwa sababu ya kubebwa na mbowe tu vinginevyo hana HADHI ya kuwa mjumbe kamati kuu ya chama, na zaidi angeshaadhibiwa kwa tabia yake ya kuropoka nje ya vikao halali vya chama kama katiba ya chama ibara ya 10 inavyosema!!
 
Alisema mwaka 2000 walikuwapo madiwani 11 katika jimbo la Zitto la Kigoma Kaskazini, lakini mwaka 2005 alipogombea walipungua na kubakia sita na kwamba mwaka 2010 walipungua zaidi na kubakia wawili, hivyo hakuna ukweli kuwa amekijenga chama katika jimbo lake
yeye si anasema ni mbunge wa kitaifa inamaana amekataliwa na wana kigoma kaskazini basi tu kujitutumua kwingi
 
'''Alisema mwaka 2000 walikuwapo madiwani 11 katika jimbo la Zitto la Kigoma Kaskazini, lakini mwaka 2005 alipogombea walipungua na kubakia sita(6) na kwamba mwaka 2010 walipungua zaidi na kubakia wawili(2), hivyo hakuna ukweli kuwa amekijenga chama katika jimbo lake.'''

Hivi mwaka 2000 na mwaka 2005 Huyu ndugu Godbless J Lema. alikuwa yuko chama gani???
 
Last edited by a moderator:
aisee,kumbe huyu kabwe amehujumu hadi kigoma,kutoka madiwani 11 hadi 2!!!
 
Back
Top Bottom