Mapokezi makubwa yamsubiri Dk. Slaa Katavi, Polisi waanza

Achana na huyo kalume kenge rud kwenye hoja mkuu! Hao wapo tangu enz za nabii musa! Ila mungu aliwaangamiza!

Hawa mara moja moja unawapa nzima ili wakwaambie jamaa zao na wazazi wao.Hakuna shida mkuu ni kweli I have to go back to the TOPIC.................Asante
 
Katika mwendelezo wa mwitikio mkubwa ambao ziara ya Katibu Mkuu Dk. Slaa imeendelea kupata tangu siku ya kwanza alipoanza mkoani Mbeya katika mji wa Vwawa wilayani Mbozi, kisha mji wa Tunduma uliozizima kwa mkutano wa kihistoria na jana mji wa Sumbawanga ukasimama kwa muda wakati wa mkutano na baada wakati wananchi walipomsindikiza kwa maelfu, leo ni zamu ya watu wa Katavi kupata neno la hamasa kuiondoa CCM mwaka huu.

Katibu Mkuu akapofika Mjini Katavi atakwenda moja kwa moja ofisini kupata briefing ya utendaji wa chama na mwenendo wa maandalizi ya chama kwa kushirikiana na vyama washirika wa UKAWA kwenda kushinda uchaguzi Mkuu wa mwaka huu na kuongoza dola.

Baada ya hapo atapita katika vituo vya uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa BVR Kama ambavyo ambavyo amefanya maeneo yote alikopita katika ziara hii na ile aliyofanya mkoani Kagera.

Baada ya hapo Katibu Mkuu atakwenda kuzungumza na wananchi wa Katavi katika Uwanja wa Kashaulili Mjini hapo ambao maandalizi yake yamekamilika ukitarajiwa kuwa mkutano mkubwa watu wa Katavi wakidhamiria kuvunja rekodi za Tunduma na Sumbawanga.

Tayari watu wa Mji wa Katavi wanamsubiri Katibu Mkuu ambapo kutokana na uwingi wa magari na pikipiki na waenda kwa miguu ambao hadi sasa wako tayari ofisi ya chama mjini hapo, polisi wamewauliza viongozi wetu wa chama kama wanaweza kupunguza idadi ya Pikipiki na magari.

Viongozi wamewaambia polisi hakuna namna ya kuweza kupunguza watu wenye shauku kubwa ya kumpokea na kumsikiliza kiongozi wao. Wamewaambia wazi kuwa wanapaswa kuzoea mwamko wa siasa nchini na kiu ya wananchi kutaka mabadiliko wakiwa tayari kukiondoa CCM madarakani mwaka huu ifikapo mwezi Oktoba.

Wamewaambia mapokezi hayo ndiyo hadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA na wananchi wanatambua umuhimu wa kumpatia heshima inayomstahili Katibu Mkuu Dk. Slaa ndiyo maana wamejiandaa tangu jana.

Wamewaambia polisi wajiandae kusaidiana na vijana wa CHADEMA katika kutoa ulinzi kwa msafara wa Katibu Mkuu Dk. Slaa kuanzia atakapofika hadi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara unaotarajiwa kufanyika Uwanja wa Kashaulili.

Hii ni siku ya nne ya ziara ya Katibu Mkuu Dk. Slaa aliyoanza siku ya Jumamosi katika mji wa Vwawa, kisha Jumapili akawa Tunduma jana alikuwa Sumbawanga.

Kote huko Daktari Slaa amepeleka ujumbe mmoja mkubwa; watu kujitokeza na kuhamasishana kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu hapo Oktoba.

Aidha ameendelea kukagua maandalizi ya chama kinavyojiandaa kwenda kushinda uchaguzi kwa kushirikiana na vyama wenza wa UKAWA na kuongoza serikali.

Makene..
.
attachment.php

attachment.php


Napata raha sana.
 
Back
Top Bottom