Mapokezi makubwa yamsubiri Dk. Slaa Katavi, Polisi waanza

Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
2,620
1,500
Katika mwendelezo wa mwitikio mkubwa ambao ziara ya Katibu Mkuu Dk. Slaa imeendelea kupata tangu siku ya kwanza alipoanza mkoani Mbeya katika mji wa Vwawa wilayani Mbozi, kisha mji wa Tunduma uliozizima kwa mkutano wa kihistoria na jana mji wa Sumbawanga ukasimama kwa muda wakati wa mkutano na baada wakati wananchi walipomsindikiza kwa maelfu, leo ni zamu ya watu wa Katavi kupata neno la hamasa kuiondoa CCM mwaka huu.

Katibu Mkuu akapofika Mjini Katavi atakwenda moja kwa moja ofisini kupata briefing ya utendaji wa chama na mwenendo wa maandalizi ya chama kwa kushirikiana na vyama washirika wa UKAWA kwenda kushinda uchaguzi Mkuu wa mwaka huu na kuongoza dola.

Baada ya hapo atapita katika vituo vya uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa BVR Kama ambavyo ambavyo amefanya maeneo yote alikopita katika ziara hii na ile aliyofanya mkoani Kagera.

Baada ya hapo Katibu Mkuu atakwenda kuzungumza na wananchi wa Katavi katika Uwanja wa Kashaulili Mjini hapo ambao maandalizi yake yamekamilika ukitarajiwa kuwa mkutano mkubwa watu wa Katavi wakidhamiria kuvunja rekodi za Tunduma na Sumbawanga.

Tayari watu wa Mji wa Katavi wanamsubiri Katibu Mkuu ambapo kutokana na uwingi wa magari na pikipiki na waenda kwa miguu ambao hadi sasa wako tayari ofisi ya chama mjini hapo, polisi wamewauliza viongozi wetu wa chama kama wanaweza kupunguza idadi ya Pikipiki na magari.

Viongozi wamewaambia polisi hakuna namna ya kuweza kupunguza watu wenye shauku kubwa ya kumpokea na kumsikiliza kiongozi wao. Wamewaambia wazi kuwa wanapaswa kuzoea mwamko wa siasa nchini na kiu ya wananchi kutaka mabadiliko wakiwa tayari kukiondoa CCM madarakani mwaka huu ifikapo mwezi Oktoba.

Wamewaambia mapokezi hayo ndiyo hadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA na wananchi wanatambua umuhimu wa kumpatia heshima inayomstahili Katibu Mkuu Dk. Slaa ndiyo maana wamejiandaa tangu jana.

Wamewaambia polisi wajiandae kusaidiana na vijana wa CHADEMA katika kutoa ulinzi kwa msafara wa Katibu Mkuu Dk. Slaa kuanzia atakapofika hadi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara unaotarajiwa kufanyika Uwanja wa Kashaulili.

Hii ni siku ya nne ya ziara ya Katibu Mkuu Dk. Slaa aliyoanza siku ya Jumamosi katika mji wa Vwawa, kisha Jumapili akawa Tunduma jana alikuwa Sumbawanga.

Kote huko Daktari Slaa amepeleka ujumbe mmoja mkubwa; watu kujitokeza na kuhamasishana kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu hapo Oktoba.

Aidha ameendelea kukagua maandalizi ya chama kinavyojiandaa kwenda kushinda uchaguzi kwa kushirikiana na vyama wenza wa UKAWA na kuongoza serikali.

Makene..
.


 

Attachments

Kinjekitile junior

Kinjekitile junior

JF-Expert Member
4,406
1,250
Makene ujumbe wako kuhusu polisi naona haujakamilika rudi tena ufafanue vizuri hapa ili tuanze mjadala rasmi!
 
Jile79

Jile79

JF-Expert Member
13,827
2,000
Tunamsubiri rais wetu kwa hamu kubwaaa
 
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
2,620
1,500
Nani ataichagua CCM kuongoza kupitia kwa wagombea wake wanaoendelea kuufanya urahisi kuwa 'bidhaa' rahisi kiasi kwamba hadi sasa tumekwama kwenye hali kama hii;
 

Attachments

Mwakaboko King

Mwakaboko King

JF-Expert Member
1,099
1,225
Nani ataichagua CCM kuongoza kupitia kwa wagombea wake wanaoendelea kuufanya urahisi kuwa 'bidhaa' rahisi kiasi kwamba hadi sasa tumekwama kwenye hali kama hii;
Usilazimishe hoja na kutafuta uhalali sema hiyo shule ni ya wapi na wewe umechangia nini
 
Mwakaboko King

Mwakaboko King

JF-Expert Member
1,099
1,225
Tena za njombe kwa makinda. Huwezi ona coz ww ni kipofu....bahati mbaya hivyohivyo ulivyo unawaongoza wenzako.
Jibu swali wewe unayeleta dharau kwa kudanganya umma,huyo rais wenu mmemwapishia wapi??au chini ya mwembe?
 
Mwakaboko King

Mwakaboko King

JF-Expert Member
1,099
1,225
Kumbe avatar ndo inasaidia kwenye ushindi?
Embu jicheki tena proceesor yako ya kichwani.
Endelea kuload na RAM yako ya kimagumagushi,hujui unachochangia sijui umekunywa viroba asubuhi hii?
 
Mwakaboko King

Mwakaboko King

JF-Expert Member
1,099
1,225
Halafu mwakaboko kwa lugha ya kisambaa ni mwanamke aliyejaaliwa makalio
Endelea tu kuongea uharo na kumfurahia huyo rais wako mliyemwapisha chini ya mwembe!muulize kilichomtokea mwaka 2010 na mkewe mwenye sifa ulizozitaja hapo, teh teh yaani vichwa vyenu ni mizigo!
 
zumbemkuu

zumbemkuu

JF-Expert Member
10,066
2,000
Endelea kuload na RAM yako ya kimagumagushi,hujui unachochangia sijui umekunywa viroba asubuhi hii?
Kwa masikitiko makubwa sana naomba nikupatie majibu yako kuwa vipimo vinaonyesha umeathirika huko kunako tigo, hivyo wewe ni bwabwa. Kwaheri na nakutakia maisha mema ya kuwa mke
 
mdetichia

mdetichia

JF-Expert Member
5,302
2,000
....

.....Hakika sakuminambili na nusu asubuhi Oktoba hiyo... Taifa litazizima !!!!
Mwambie bi mkubwa afunge kichau kula hukohuko manake hawa jamaa nasikia wamejipanga ukishapiga kura urudi nyumbani majibu utayapata huko huko kama sio wizi ni nini.
 

Forum statistics


Threads
1,424,986

Messages
35,078,036

Members
538,184
Top Bottom