WIMBO: Chura
ALBUM: sina hakika
KUNDI: JKT Taarab
Chura nakuulizia unipe jibu makini,
kwa kila inyapo mvua wakimbilia bwawani
Huna nguo za kufua na wala huna sabuni,
nijibu yapate tua maji utayafanyani
Chorus
Chura punguza vituko na wako uhayawani,
umezua sokomoko watu hawaeleni
Ukivunjika mgongo, dawa atakupa nani?
2.
Mwenzenu nilikisia ni mlinzi kisimani,
mtu utamzuia maji akiyatamani
Akaja dada Rukia na ndooye mkononi,
chura ukajing`atua ukajitosa pembeni
Chura punguza vituko ………………………
3.
Chura bora kuamua wende kulima shambani,
mazao kujipatia wende kuuza sokoni
Nguo kujinunulia isitiri maungoni,
au ukitaka ndoa nenda kaoe nyumbani.
Chura punguza vituko ………………………
wapendwa,
nimeweka wimbo wa CHURA wa JKT Taarab kwenye lik hii hapo chini:
https://www.jamiiforums.com/entertainment/208761-chura-jkt-taarab-walitisha-sana-enzi-hizo.html
naomba tujadili usahihi wa maneno hayoo yaliyokolezwa rangi nyekundu
1.
mimi nafikiri badala ya kusema nilikisia, ilipaswa kusemwa nilidhania au nilifikiria, manake makisio ninayoyajua mimi ni "estimates" kwa kiingereza na haiwezekani kwa vyovyote vile kuwa dhana iliyoko kwenye hilo shairi ni "estimate"
2.
na hapo kujing'atua, ukiachilia mbali msuala ya vina na mizani, tusema mwalimu nyerere aling'atuka au naye alijing'atua madarakani??
3.
kuhusu "kujitosa pembeni", hapo pembeni ni wapi, ni kisimani au nje ya kisima, na kama ni nje ya kisima, inawezekana kitu au mtu kujitosa nchi kavu? au kujitosa lazima iwe majini (kisimani/mtoni/ziwani/baharini nk)?
4.hiyo sentensi nadhani iko sawa kisarufi, ila kimantiki ni suala la tafsiri ya neno nyumbani na wakati tu kwamba kwa wakati wa sasa, haisisitizwi kuwenda kuoa nyumbani na kwa wakati huu mtu aweza kuoa popote hata nchi za ng'ambo.
pia baadhi ya mila haziruhusu kuona nyumbani (close relatives). japo kishairi inaeleweka kuwa ililenga kubalance vina na mizani, isipokuwa kama dhana ya neno nyumbani kama inavyotumika, imelenga dhana sawa na "home town/city/country" nk vinginevyo kama ni close relative itakuwa jambo lisilowezekana kwa mila nyingi za kiafrika
nyie mnaonaje wapendwa?
mbarikiwe sana
Glory to God
Lugha ya kishairi mara nyingi hainyooki la ujumbe hufika kama inavyotakiwa, pamoja na yote umemwelewa Chura?
Chama
Gongo la Mboto DSM
Hii ni fasihi. Na katika fasihi watunzi hutumia maneno anuai hata ya lugha za kigeni ili mradi wapate vina muafaka katika mpangilio wake. Na katika muktadha huo inafika wakati wanaweka maneno kimakosa, sasa hapo hunabudi msomaji ufahamu nini maudhui ya Mtunzi au Mwandishi. Lugha ni Fasihi . Lakini umelielewa Shairi maana yake?
Lugha ya kishairi mara nyingi hainyooki la ujumbe hufika kama inavyotakiwa, pamoja na yote umemwelewa Chura?
Chama
Gongo la Mboto DSM
Mkuu chama wa Gongs,
Hebu fanya maarifa hapo, huyu chura ni nani? mi mpaka leo bado kumjua
Natanguliza shukrani
Asprin
Boko Basihaya, DSM.
Mkuu mtemiwaWandamba,
Tafadhali saidia mimi kujua maana ya huu ushairi. Huyu chura ni nani anazungumziwa?