Dr am 4 real PhD
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 18,336
- 37,122
Cheap energy drink ni mbaya mfano mo energy,Azam energy sio nzurii labda ZILE energy drink expensive kidogo.Nanasi kwenye kikali? Sijawahi ona live.
Mie nachanganyaga na energy japo kuna siku ilitaka kuniletea kashda, kidogo niimbiwe parapanda.
👏👏👏👏👏Mahitaji ya Kupika Biriani
Viambato vya Msingi
Wali (mchele wa Basmati) – Vikombe 3
Nyama ya mbuzi, kuku, au nyama nyingine yoyote – Kilo 1
Vitunguu maji – 3 vikubwa (katwa mviringo na kukaangwa hadi rangi ya dhahabu)
Nyanya – 4 (saga hadi ziwe laini)
Mtindi wa asili – Vikombe ½
Kitunguu saumu na tangawizi ya kusagwa – Vijiko 2 vya supu
Mafuta ya kupikia au samli – Vikombe ½
Chumvi – Kiasi cha ladha
Viungo vya Biriani
Binzari ya pilau (cumin) – Kijiko 1 cha chai
Mdalasini – Vipande 2
Hiliki – Mbegu 5
Karafuu – Mbegu 5
Paprika au pilipili ya unga – Kijiko 1 cha chai
Binzari manjano (turmeric) – Kijiko ½ cha chai
Majani ya mint au coriander – Kiasi cha kupambia
Hatua za Kupika Biriani
1. Kuandaa Nyama
Osha nyama vizuri na uikate vipande vya wastani.
Weka nyama kwenye sufuria, ongeza mtindi, tangawizi na kitunguu saumu, nyanya, na viungo vya biriani (binzari ya pilau, hiliki, mdalasini, karafuu, na paprika).
Changanya vizuri na acha ichemke kwa moto wa wastani hadi nyama iwe laini na mchuzi uwe mzito.
2. Kuandaa Wali
Osha mchele na uuweke kwenye maji safi kwa dakika 30 ili ulainike kidogo.
Chemsha maji mengi kwenye sufuria na ongeza chumvi na binzari manjano kwa ladha na rangi nzuri.
Weka mchele na upike hadi uwe karibu kuiva lakini usiutoe kabisa (unapaswa kuwa na ukoko kidogo).
Chuja maji ya wali na uweke pembeni.
3. Kukaanga Vitunguu
Kwenye sufuria tofauti, kaanga vitunguu hadi viwe vya rangi ya dhahabu. Hii itaongeza ladha na muonekano wa kuvutia kwenye biriani yako.
4. Kupanga Biriani
Katika sufuria kubwa, pakiza tabaka za mchanganyiko wa nyama na wali.
Anza na tabaka ya mchuzi wa nyama, kisha funika na wali, na endelea kupangilia hadi viambato vyote viishe.
Nyunyiza vitunguu vya kukaanga na majani ya mint au coriander juu kwa ajili ya harufu nzuri na ladha.
5. Kukamilisha Kupika Biriani
Funika sufuria vizuri na ipike kwa moto wa chini kwa dakika 20 hadi 30. Hii husaidia viungo na ladha kuchanganyika vizuri.
6. Kuhudumia
Tumikia biriani ikiwa moto na usindikize na kachumbari, mchuzi wa nyama, au maziwa ya mgando.
Vidokezo vya Mafanikio
Chagua mchele wa ubora mzuri: Mchele wa Basmati hutoa biriani yenye muonekano mzuri na ladha ya kipekee.
Epuka wali kupitiliza kuiva: Wali wa biriani unapaswa kuwa na ukoko kidogo ili usikunjike unapochanganywa.
Tumia moto mdogo mwishoni: Hii husaidia wali na mchuzi kuiva vizuri bila kuungua.
Viungo vya biriani ni muhimu: Viungo vinachangia harufu nzuri na ladha tamu ya biriani.
Faida za Biriani
Mlo wa kukaribisha wageni: Biriani ni chakula kinachoheshimiwa kwenye hafla mbalimbali.
Mchanganyiko wa ladha: Inakutanisha ladha ya nyama, wali, na viungo vya asili kwa namna ya kipekee.
Inaweza kubadilishwa kulingana na upendeleo: Unaweza kutumia mboga badala ya nyama kwa biriani ya mboga.
Hitimisho
Kupika biriani ni sanaa ambayo inahitaji uvumilivu na upendo lakini matokeo yake ni mlo wa kipekee na unaofurahisha.
Kwa kufuata hatua hizi rahisi unaweza kupika biriani nyumbani kwa ladha nzuri kama ya mgahawani.
Mdogo angu ukipata muda tuwekee nondo za kulipika😊 ili sisi watu wa uswahilini siku moja tulipikeKabisa birian ni rost
Kabisa.We sema kweli
Hiyo kabichi waipikaje kwani, usikute me naloweka, maana hahahahaMie kabichi huniambii kitu, nile kabichi mwaka mzima na kisamvu sawa tu.
Mie maharage labda nile kijiko kimoja tu.
Ila hapana aisee.
Ila kunde nakula.
Ndio ivo wanaripua tuMwanzo nilihisi hivyo nikaenda kununua pale kwa nino ijumaa morocco hali ikawa ivyo ivyo pilau ina uhafadhari tofauti na birian
Maziwa kwenye pombe kali?Cheap energy drink ni mbaya mfano mo energy,Azam energy sio nzurii labda ZILE energy drink expensive kidogo.
Energy drink sio nzurii Sana naziogopa maana zinakataga usingizi pombe ikiisha kichwani.
Jarib hata nanasi ya AFIYA utaona io cocktail yake.
Kuna ambao huchanganya na maziwa fresh 😀 dunia hii Ina maajabu mengi mengi sanaa
Naiunga na kitunguu, nyanya, vijinyanyq chungu na hata wakati mwingine naweka simbambili ili kunogesha ladha.Hiyo kabichi waipikaje kwani, usikute me naloweka, maana hahahaha
Mbona zanzi 😊Maziwa kwenye pombe kali?
Sijawahi sikia wala ona
Kweli dunia ina maajabu.
Energy inanipaga shida sana sema ndio hivo sina la kufanya.
Na nikinywa inanipelekesha hoi, sema napenda kale ka stimu kake ndio maana wakati mwingine inakuwaga ngumu kuiacha.
Ila ya maziwa sijawahi kuona, mbali ya kusikia pia
Madam B hujaona mkate wa kingazija (mkate wa gudugudu) unavyopikwa wee utablow👏👏👏👏👏
Asante sana kwa maelezo.
Mwachiluwi uje sasa utoe diko kesho.
Sema biriani lina process kama sijui kitu gani!
Yaani unaweza ghahiri kula.
Ila jamaa kasema biriani hajataja bilianiBiliani ni lost sio mchele nikitulia nashusha maelezo
Zanzi na Amarula nilishawahi ila 🤮.Mbona zanzi 😊
Huyo jamaa anachanganya pombekali na maziwa ntaweka ushahidi wa pichaa.
Utakufa ukimix na energy ujue🤔Nanasi kwenye kikali? Sijawahi ona live.
Mie nachanganyaga na energy japo kuna siku ilitaka kuniletea kashda, kidogo niimbiwe parapanda.
Tobaaaa!!!Madam B hujaona mkate wa kingazija (mkate wa gudugudu) unavyopikwa wee utablow
Mkate huo unapikwa siku nzima 😂😂😂
Katika kukua kwangu nimemuona mamaangu kaupika mara 1 tu.
Ila ukishapikwa unaweza kukaa zaidi ya mwezi mmoja upo fresh hauharibiki
Maziwa hayakatiki?Cheap energy drink ni mbaya mfano mo energy,Azam energy sio nzurii labda ZILE energy drink expensive kidogo.
Energy drink sio nzurii Sana naziogopa maana zinakataga usingizi pombe ikiisha kichwani.
Jarib hata nanasi ya AFIYA utaona io cocktail yake.
Kuna ambao huchanganya na maziwa fresh 😀 dunia hii Ina maajabu mengi mengi sanaa
Huu msisitizo maanake nini maana vijana siku hizi mnakua na ndimi mbili 🤔😂😂😂Exactly 💯 tamu sana yaani sana Broccoli nalipenda sana lile😎
Muhimu📌simbambili
Yaani kuna siku ilibaki 🤌 niyaage mashindano.Utakufa ukimix na energy ujue🤔
Kwa sura upo kama mkate wa sembeTobaaaa!!!
Siku nzima unapika mkate?
Gudugudu?
Sijawahi hata kuusikia.
Kweli vyakula na vitafunwa viko vya aina nyingi.
Ni kama mkate wa kawaida au upoje upoje huo?
Kabisaaaaaa!!!Muhimu📌