Mapinduzi ya kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapinduzi ya kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Felixonfellix, May 17, 2010.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  :eyeroll2: Kwa hili pinduzi la kwanza, aidha kuking'oa madarakani chama tawala CCM, ambacho kimehakikisha kushindwa kazi, au kufanyike mapinduzi makubwa ndani ya chama hiki ili kiweze kukidhi matarajio na matakwa ya watanzania. Ni chama gani kingine kitaweza kuchukua nafasi ya CCM, hiki bado ni kitendawili. Kwa nionavyo na hali ilivyo, sijaona chama mbadala kitakachoweza kuleta maendeleo nchini. Ninachoona, ni pilikapilika za kisiasa kukidhi matamanio ya kisiasa. Sioni juhudi na nia thabiti za kisiasa ndani ya vyama vya siasa nchini katika kukuza uchumi wa nchi. Hivyo basi, kunahitajika chama mbadala chenye malengo thabiti ili kuchukua nafasi ya CCM, si hivi vyama vilivyopo sasa. Lah, mapinduzi makubwa yanatakiwa yafanyike katika vyama vilivyopo sasa.

  Ni vipi mabadiliko ndani ya CCM yatafanyika, hili nalo ni swali tete lisilokua na jibu la moja kwa moja. CCM kama chama tawala lazima kibadilike na kujirudi ili kuwatendea haki watanzania. Kikiwa ni chama tawala, CCM ina nafasi ya moja kwa moja katika kuboresha maisha ya watanzania. Wana-CCM ndio viongozi wa nchi hii, wao ndio wakuu wa mikoa, wao ndio wabunge, wao ndio wanakamati za mambo mbalimbali, wao ndio mawaziri, wao ndio kila kitu. Kulegalega kwa maendeleo ya nchi ni athari za moja kwa moja za hawa viongozi ambao ni wana-CCM. Baadhi ya maswali muhimu ya kujibu katika kufanya mapinduzi ndani ya chama tawala ni kama ifuatavyo:

  - Vipi ilani za CCM zinaweza kutekelezwa kivitendo?
  - Utendaji wa viongozi unafuatiliwaje? kwa kiasi gani? hapa kuna mifano mingi tu mmoja ni huu utendaji wa kazi wa wabunge. Kwanza ni zipi kazi ya mbunge? vipi mbunge anawajibika/wajibishwa (kuna ulazima wowote wa kumtaka mbunge atembelee jimbo lake kuchochea shughuli za kimaendeleo? nani anafuatilia kama hili linafanywa? Je wabunge mabubu bungeni wanawajibishwa vipi?),
  - Vipi CCM itaepuka siasa chafu - kwa mfano pale wafanyabiashara wanapokuwa wanasiasa kukidhi matamanio yao, au pale wasomi wanapokimbilia siasa kukidhi tamaa zao huku wakijua taifa linahitaji wasomi, au ubinafsi unapochukua nafasi ya utendaji, au fitna za kisiasa zisizo na maana yoyote zaidi ya tamaa tu, n.k
  - Vipi wananchi wanaweza shirikishwa katika maamuzi ya chama kuhusu maswala ya mustakabali wao?
  - Vipi chama kama chama kitajali watu wake zaidi kuliko siasa?
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mapinduzi yoyote yawe ya kisiasa au vingi nevyo yana anza kwana na mapinduzi ya kifikira ya wananchi wenyewe.
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kuna watu binafsi pia wanaweza kujipanga kuchukua nchi kwani shinikizo la mgombea binafsi limefika juu zaidi naona wananchi wamepata msukumo wa kutosha na majaji wamekuwa huru zaidi nadhani tuanze kufikiria wagombea binafsi pia wataoweza kuleta mabadiliko
   
Loading...