Mapinduzi ya hiyari, nchi haina Dini

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,011
Jambo la kushangaza siwezi kusema zuri au jema bila kuwa na hofu katika visiwa vyetu na Taifa hili la Tanzania siku nyingi tumeambiwa na tuna kumbushwa mara kwa mara kuwa Tanzania haina dini isipokuwa sisi waungwana tunao ishi humu ndani ndio tuna dini,kwa maana hiyo tumepewa uwezo kikatiba kuabudu tunacho amini au kutaka hata ikiwa jiwe au tofali ukilikuta halina kazi {halijajengewa} basi ruhsa kulisjudia hakuna atakae kuuliza au kukukataza kwa sababu sheria za nchi ziko wazi kuwa usiingiliwe katika ibada hiyo,sasa kumezidi nini katika haya MAPINDUZI kuwa lazima iwe ndio dini ya kuabudiwa na sote kwa nguvu peke yake sio kisheria uhuru wa kuchagua hapa umeondolewa lakini kwenye dini umewekwa kisheria na kikatiba?

Hii mitihani inatukuta katika kugawa,kutawala na kuwadhibiti wananchi wasijue nani wa kumuogopa au nani wa kuabudiwa na yupi wa kupuuzwa, utasikia usi changanye siasa na dini kwa kuwa hutaki pilau unawafunga wapishi wa mlo huo gerezani sasa unapita ukikusanya viungo na wapishi huna,muhogo unakudhuru na kooni umesha kwama, wali mweupe huuwezi kumbe pilau haikimbiliki.

Mapinduzi tumeyageza ubaguzi siku nyingi sasa tuna vuna tulichopanda.

mzeekondo.
 
Back
Top Bottom