Elly B
JF-Expert Member
- Jan 11, 2011
- 1,194
- 906
Ndugu Zangu,
Wakati nafikiria kwa makini maana ya Mapinduzi, nikajiwa ghafla na hii picha yenye utata ya jinsi sherehe ya mapinduzi itakavyokuwa.
Kwanza nikaona ni siku ya kihistoria kwa sababu kuna wajukuu waliozaliwa katika mapinduzi hayo ambao wengi hawajui hata ukweli kuhusu mapinduzi hayo. Wajukuu ambao hawatajua mapinduzi yana uzito gani hasa. Mapinduzi ambayo yataona aibu kuwataja watu kama kina John Okello. Nabaki najiuliza kwani hasa tunachoogopa kusema ukweli ni kipi? Kuna nini tusema ukweli?
Lakini la pili, ni siku ya aina yake kwa sababu leo tena dunia itapata kushuhudia matukio ya ajabu ajabu. Leo Rais wa Jamhuri atahudhuria sherehe hizo na atapokelewa kama mgeni wa kawaida tu. Hamtasikia walau wimbo wa Taifa alilotokea (maana taifa hilo siyo Zanzibari). Halafu atatakiwa kuwahi uwanjani ili Mwenye nchi afunge ugeni kama Mkuu wa nchi. Halafu itabidi asimame kwa heshima wakati Mkuu wa nchi ya Zanzibar anapokea heshima ya majeshi yake. Na Mwisho kabisa itabidi asubiri Rais wa Zanzibar atoke uwanjani ndiyo yeye pamoja na other members of the floor watoke!
Kwa haraka leo ni siku ya wale waiotaka kuona kasoro za Muungano kupata fursa ya kujionea kwa macho kasoro hizo. Shangaa utasikia wengine hawaoni kama kuna kasoro hata kidogo, na wengine walipoweka hilo mpaka kwenye katiba kwamba Zanzibar itambuliwe rasmi na katiba, sambamba na Tanganyika kurudi, hao hao wagonjwa walikuwa wa kwanza kupinga. Halafu bila shida wanakwenda kumdhalilisha Mwenyekiti wao leo!
Lakini haya! hii ndiyo Tanzania. Nchi ya aina yake ambapo chochote kisichowezekana kutokea popote duniani, kinaweza kutokea na watu wakaona ni OK. Na tukiendelea hivi nitaomba mnisamehe pale nitakapoi-nominate nchi yangu iongezwe katika maajabu ya Dunia!