Mapinduzi 2010: Mzizi wa Mabadiliko ya Kweli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapinduzi 2010: Mzizi wa Mabadiliko ya Kweli!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rev. Kishoka, Aug 17, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kubadilisha Chama au Wanasiasa si tija ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini Tanzania.

  Kujipanga upya kupitia Vyama au kutafuta Wanasiasa wapya si njia bora ya kuleta mabadiliko nchini Tanzania.

  Kupigia kelele Ufisadi na hata kuiombea CCM ianguke na kumeguka, hakutaleta mabadiliko ya madendeleo Tanzania.

  Tunahitaji Mapinduzi 2010!

  Tunahitaji mapinduzi ya fikra, utashi, nia na nguvu binafsi ili tulete mabadiliko ya kweli Tanzania.

  Tunapaswa kujijenga kama jamii mpya iliyo huru, yenye kujithamini na kujiamini ili kufanikisha mapinduzi haya.

  Mapinduzi anayoyatamka Rev. Kishoka, si kukatana mapanga, Jeshi au kikundi kuamua kupindua Serikali! La hasha! Bali ni mapinduzi ndani ya mioyo yetu.

  Mapinduzi ya kweli yataanza na Mtanzania kuamua kuachana na Utegemezi na kuanza kujituma, kujiendeleza na Kujitegemea.

  Ndiyo, ni kweli tumeimba nyimbo za kujitegemea kwa miaka mingi, lakini hatukufanya busara na kutafuta njia nyepesi na rahisi kufanikisha azma hiyo ya kuwa Taifa linalojitegemea.

  Mapinduzi ya kweli ya kuleta maendeleo na kujenga Taifa linalojitegemea yatatokana Watanzania kwa umoja kujenga mfumo bora wa kiuchumi ambao si mgumu kama ule wa Adam Smith au John Keynes, bali ni mfumo ambao utamfundisha Mtanzania kuzalisha si cha kujihimu kwa siku mbili tuu, bali ni kuzalisha kwa wingi, kutumia maarifa bora ya Sayansi, Teknolojia na Biashara ambayo si magumu kama Aljebra bali ni mepesi na rahisi kama hesabu za kutoa, kuongeza, kugawanya na kuzidisha.

  Kosa letu Watanzania na hasa sisi Wasomi ni kukimbilia kulijenga Taifa letu kwa mfumo wa Uchumi unaotumia nyenzo za hali ya juu kuliko uwezo wa kawaida wa fikra au utashi kwa Jamii yetu.

  Nikiangalia mkulima, ikiwa atapigwa msasa na kuonyeshwa kuwa akilima heka 20 badala ya heka 2 na kuonyeshwa faida za kulima kwake heka hizo 20 ikiwa ni pamoja na kulima kwa ustadi, kutumia mbolea, umwagiliaji na kujijengea maghala imara ili kuhifadhi mazao yake, basi ni wazi mkulima huyu akiona kipato chake na uwezo wake wa kuzalisha mali unaongezeka, hiyo itakuwa ni kichocheo na motisha wa yeye kuongeza nguvu zake na kujiongezea kipato.

  Lakini maendeleo haya yatapatikana ikiwa Mkuilma huyu atakuwa na Uhuru wa kuuza mazao yake bila kunyanyaswa na Serikali ya kijiji, mtaa, Ushirika au Chama cha Kisiasa.

  Hali kadhalika yule Mangi wa pale Gerezani na Machinga mtaa wa Kongo, akifundishwa mbinu bora za kufanya biashara yake kwa kutumia nyenzo nyepesi na kujiwekea nidhamu ya kazi na hata kufundishwa kujiwekea hifadhi ya mapato yake Benki, basi ni wazi Mangi na Machinga atapiga hatua ya kimaendeleo.

  Pamoja na kuwa Dunia ya leo iko kwenye Teknolojia za Nano, GMO, Digital na nyinginezo ambazo zinaongeza uzalishaji marudufu, ukweli ni kuwa mzalishaji wa Tanzania hawezi kingia katika ushindani wa kimataifa huku akiwa hana umeme, maji au mfumo mzuri wa mawasiliano na ushukuzi ambao unaweza kumfanya ajijenge na kujitosheleza.

  Mkulima niliyemtolea mfano hapo juu, si lazima asafirishe mazao yake Dar Es Salaam, bali anaweza kuuza jirani kabisa na anapoishi au kuwa ndani ya mfumo bora wa kuuza mazao yake ambapo hatatumia gharama nyingi kujipatia kipato cha kufidia jasho lake.

  Kila kitu kinahitaji utashi, nia na nidhamu ya hali ya juu.

  Mtanzania atakapo amka na kuyakubali mapinduzi ya fikra ya kuachana na utegemezi, hiyo itakuwa hatua kubwa ya kwanza na muhimu mno kwa Taifa letu katika kuleta mabadiliko ya kweli, iwe ni kisiasa, kiuchumi au jamii.

  Kinachotushinda kuleta mabadiliko Tanzania si rasilimali, Vyama vya siasa, Katiba, Sheria, Sera, Ilani au Wanasiasa.

  Ni mizizi iliyokomaa ya kutegemea misaada!

  Ndiyo, ni tabia chafu ya kuwa ombaomba, kutegemea kubebwa, kusaidiwa, kupewa, kuhongwa, takrima, baksishi, kidogodogo hata ruzuku.

  Nimetoa mfano hapo juu wa Mkulima, Mchaga na Machinga, na kutamka wazi kuwa inabidi tawe nyenzo nyepesi na kuwafundisha ustadi na umakini katika uzalishaji mali wao na hata kuwafundisha kuwa na mipango bora.

  Hilo ni muhimu ili Mkulima, Mchaga na Machinga wawe huru na kuachana na kutegemea au kuishi kwa kutegemea ndani ya mfumo wa kutegemea.

  Waswahili husema "mtegemea cha ndugu, hufa masikini", sisi kama Tabaka la Wasomi, Wanasiasa na tulioona mengi na kujua mengi, tumeshindwa kumkomboa Mtanzania mwenzetu kwa kumfanya yeye ni mjima, mjinga na kusimika mizizi ya unyonge kwake, hivyo kumfanya yeye "mtegemea cha ndugu" tukimburuza kila kona na kila mtaa na kumtaka afanye tunachotaka na tunachomuamuru.

  Hapa ndipo tulipopotea na tutaendelea kujidanganya kama tutadai kuwa eti tubadilishe kwanza chama, katiba au kuwa na hata wagombea huru.

  Tunachohitaji ni kubadilisha fikra zetu, kama wasomi. Tutumie ujuzi wetu na upeo wetu kurahisisha uzalishaji mali na kuimarisha safari ya Taifa letu na watu wake kwenda katika mfumo wa kujitegemea.

  Ikiwa kama tunashindwa kuishi kama mfano kwa Mtanzania mwenzetu aweze kutuiga kwa yale yaliyo chanya, ni vipi tutegemee yeye ataamka na kuwa na maendeleo?

  Ikiwa Bwana Shamba, Mifugo, Hakimu, Polisi, Muuguzi na wengine, hawaishi maisha na kufanya mambo yanayoendana na elimu zao, tutategemeaje kumfundisha Mzaramo kuwa akikata nyasi na kuondoa uchafu kando ya nyumba atapunguza kwa kiwango kikubwa nafasi ya yeye kupata malaria, huku sisi nyumba zetu zimejaa vichaka na madimbwi ya maji machafu?

  Kule kijijini ikiwa Bwana Shamba ni mhubiri bila vitendo na matunda ya kazi yake kwa manufaa yake yakaonekana kwa Wanakijiji wenzake, tutawezaje basi kudai kuwa Wanakijiji hawaambiliki?

  Hivyo basi ni wajibu wetu kubadilisha fikra zetu, za majirani zetu na familia zetu ziwe ni fikra endelevu kama tunataka mapinduzi ya kweli.

  Jukumu hili ni la kila mmoja wetu na si kusubiri kumsikia Kikwete, Slaa, Maalim Sefu, Bakwata, TEC, Mwanakijiji au Mchungaji waendelee kuyasema haya!

  Ndio kila mtu atakuwa na mvuto wake, na njia yake kuifundisha jamii. Lakini hakutakuwa na mwamko au usahihi kama elimu ya kuleta mapinduzi ya fikra na mwamko mpya wa maendeleo ili kujenga Taifa linalojitegemea kutakuja na masharti ya kijinga, kama kujiunga na chama, kubadili dini, kuletewa huduma kwa utiifu wa Chama, Mtu, Dini au lolote lile!

  Tunapojianda kwa mwaka 2010, basi tujiandae kuleta mapinduzi ya kweli na si kudanganyana! Nasema mwaka 2010 kwa kuwa kila mmoja wetu keshaamua kuwa kazi ya kuleta mabadiliko ni 2010, hivyo nikisema tuanze sasa, sidhani kama utanisikia au kunielewa.

  Wakati ukitafakari mgombea, sera na chama, ambacho unadhani kitaleta mabadiliko na kuimarisha vita dhidi ya Unyonge, Umasikini, Maradhi na Dhuluma, usimsahau Mtanzania mwenzako ambaye kura yake unaitumia kwa manufaa yako binafsi huku yeye akiambulia ahadi nyingi, fulana na ubwabwa na shukrani za kinafiki!

  Mwaka 2010 uwe ni mwaka wa Mapinduzi ya kweli kutuletea maendeleo na kutukomboa katika unyonge na utegemezi.

  Chaguo ni lako, tumia Uhuru na akili zako kwa umakini!
   
 2. S

  Shamu JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Conservative thinking is the best way to live.
   
 3. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,086
  Likes Received: 1,731
  Trophy Points: 280
  Sorry,
  A Partly Utopian discourse of forgotten centuries, though good for preaching. Please think today!
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mchungaji;

  Niemuvutiwa sana na Matamshi: Mapinduzi Ya Fikra, Mapinduzi ndani ya Mioyo yetu, Mapinduzi ya Utashi, Mapinduzi Ya Nidhamu...Katika lugha ya kisasa na kiutandawazi.. Vyote hivyo Vina simamia dhana nzima Ya Emitional Intelligence (EI) VS IQ.

  EI kwa lungha ya nyumbani ni Kiwango cha Utu Na IQ ni Kiwango cha akili.

  Kuana Kueleimika ki AKILI ni tofauti na kuelimika ki UTU.

  Mtu anaweza kuwa ameeleimika na kuwa na afya timamu kiakili lakini akawa na tatizo la kiutu kiafya na kielimu.

  Maendeleo ya kweli ni jumuisho sahihi la Viwango viwlili kwa pamoja.

  Mada ya Mchungaji haijapitwa na wakati. Utu wa mtu haupitwi na wakati.

  Kwa kifupi mada inadai Kujumuisha Kiwango cha UTU kwenye mikakati ya maendeleo na ustawi wa jamii!

  Huwezi kusaliti "Intrinsic Nature" ya Mwanadamu na kutegemea Maendeleo yanye misigi wowote kwa wanadamu na jamii husika husika. Makosa ya kiutu na si kiakili ndio yanoyoigharimu dunia mtikisiko mkubwa wa kiuchumi leo hii. Binadamu wameelimika kwa kiwago cha juu kabisa Kiakili lakini wajinga wa kutisha ki UTU.

  Ni muhimu kukaa chini na kujifunza kinaganaga Dhana nzima Ya UTU kwenye kumstawisha mwanadamu.

  Utu hakuna asiye kuwa nao...AU?

  Kwa mfano tu!

  UZALENDO NI UTU, Kujitegemea ni Utu. Kujituma ni Utu. Kujiheshimu Ni Utu. Nidhamu Ni utu. Utashi Ni Utu. Maadili ya kifamlilia na kiuongozi ni Utu, Kujituma kwa nidhamu na kujali wengine ni Utu. Kukosa ubinafsi wa Kinyama ni Utu. Kujilimbikizia mali kibinafsi Si Utu. Mipango ya kiuchumi na kisiasa inayosimamia utu NI UTU NA MSINGI WA MAENDELEO YA KWELI.

  Mtu mwenye Akili ya kiwango cha Phd au zaidi ya hapo anaweza kuvikosa vyote hivi. Kiongozi wa Taifa ndani ya IKULU anaweza kuwa na kiwango cha sifuri au 1% ya kiwango hiki. Baraza la mawaziri linweza kuwa na kiwango cha chini na cha kutia aibu cha utu..nk. Nyanja zote za kijamii zinaweza kutokuwa na Kiwango sahihi cha Utu Ninaoongelea hapa. Hivyo kupambamabana kwenye vita ya kujenga Utstawi na maendeleo ya jamii kwa Mkono mmoja.

  Mipango na mikakati yote ya kiserekali, kijamii na kichama kama vimesimamia miodoko ya kiakili tu... na kutokutilia maanani Ladha na vionjo vya Ki Utu kama haki, busara, usawa, uvumilivu, uzalendo, kujitolea... sana sana kinachotegemewa hapo ni maanguko kupitia vita vya wenyewe kwa wenyewe au hata majirani, ufisadi, maradhi, matabaka na upuuzi mwingine wowote kijamii...Nafikiri tusiende mbali sana.. Tanzania tunaelekea kuwa mfano mzuri kwa hili...

  Itaendelea...
   
 5. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Kweli kama tunataka mabadiliko ya kweli, as individuals we should be part of the changes we want to see in Tanzania. Kila mtu akiamua kubadilika positively, then tutaweza kuibadilisha Tanzania. Hakuna mjomba wala shangazi ambaye atatusaidia kujipatia yale tunayoyataka kama sisi wenyewe na system zetu tulizozijenga haziko tayari kuyapokea hayo mabadiliko.
   
 6. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa hembu fikiria kwa Mawazo kama haya yanawekwa kwenye Majarida watu wanaenda kuyasoma nafikiri tungekuwa mbali sana watanzania. KUDOS REV
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180

  Enlight us the njia bora which is practical if you do not mind.
   
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakika watanzania lazima tuache uoga na ujinga kwani CCM wanazidi kuifilisi nchi. Wote ni wanafiki na mafisadi. wezi wakubwa wa kura.

  LAZIMA TUWANG'OE 2010
   
 9. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Je tuko tayari kuleta mapinduzi?
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,062
  Trophy Points: 280
  Nilijua tu unakoelekea........ watu wako vitani wanapambana wewe endelea tu kujiuliza utakapomaliza kujiuliza na filosofia zako za kufikirika(theories) njoo utatukuta wengine tayari tuko kwenye uwanja wa mapambano ya kweli(reality), ngoja niishie hapa kwa sasa naona watu hawajakuelewa.
   
 11. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Blah blah nyingi hazileti tija...safari ya mile millioni moja huanza na hatua mmoja........nayo kwa sasa ni kuing'oa CCM kwanza ndio tuanze kujipanga na mfumo tofauti. Huduma ya kwanza ni kuing'oa CCMna matibabu ndio kuweka mifumo inayofaa kuongoza nchi.
   
 12. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Rev Kishoka, Sophists means stop torturing ur brain and join the ulimbukeni wagon that has brought us hapa tulipo....or kuwa mjanja, bongo ni bomba tu, kwa aliyetayari kusurrender mbele ya madhabahu ya mfumo fisadi. Very simple indeed kuliko kuumiza kichwa kama ufanyavyo kaka..
   
 13. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kubadilisha chama na wanasiasa ni tija ya kuleta mabadiliko ya kweli.......

  Wewe ni mchungaji mtu akija kwako unamwombea na unamwambia asali halafu atabadilika na wengine hata kuokoka
  lakini kwenye mabadiliko ya nchi ni tofauti....
  hatuwezi tukamwacha lowasa, karamagi na majambazi wenzake tukategemea wabadilike ili watuongoze

  twende kwenye real issue
  watu tunataka mabadiliko ya uongozi kwa ajili fikra zetu zimebadilika/fikra zetu zimepinduka, kwa hiyo mapinduzi ya fikra tiyari sasa hivi, hatuwezi kuimplement fikra zetu kwa ajili viongozi walio madarakani wanazuia implementation. kwa hiyo sasa hivi ni wakati ni wakati wa mapinduzi ya chama na wanasiasa

  stage 3 za mapinduzi
  1. mapinduzi ya fikra - hapa ni done
  2. mapinduzi ya chama na wanasiasa - sasa hivi tuko hapa
  3. utekelezaji wa fikra - mpaka tumalize stage 2 ndio tunaweza kuingia ya tatu

  ooops mchungaji umeachwa, mapinduzi ya fikra tiyari... sasa hivi tuko stage ya pili, hatukusubiri ila kama unataka tukimbilie

  sasa hivi watu tuko kwenye election mood wakati wa mapinduzi ya chama na wanasiasa
  dr slaa amebadilisha hata akili za wasomi ambao walikuwa hawataki kubadilika, hii ni kitu tofauti kabisa na wakati wa mrema. dr amepambana for 15yrs na watu wamemwona
   
 14. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Hayo mapinduzi yatawezekanaje bila kufuta rushwa? Leo hii wasomi wakifungua kampuni yao na wakawa na vigezo vyote vya kuomba kazi BILA rushwa huo mkataba hautafungwa. Ni ajabu kama maomba ya tenda yanafanyiwa evaluation na watanzania, tenda hiyo hiyo ikifanyiwa evaluation na wageni (ambao siyo watanzania) kitakachotokea ni kuwa evaluation ya watanzania itampa mshindani mwenye uwezo wa kuwapa pesa bila kujali utendaji wakati evaluation ya wageni itampa kazi mtu ambaye ataifanya kazi hiyo katika ukamilifu wake na gharama ndogo.

  Mapinduzi yanatakiwa yaanzie kwenye SIASA maana SIASA Chafu zenye kuendekeza rushwa ndio chanzo cha wajasiliamali wadogo kushindwa kustahimili ushindani toka kwa wafanyabiashara wakubwa ambao mitaji yao wameipata kifisadi hivyo haina gharama yeyote.
   
 15. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,501
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Unaletaje mapinduzi bila ya kufanya mabo hayo (hapo kwenye red)? Labda ungesema kuwa "kufanya hayo peke yake haitoshi" !
   
Loading...