Mapigano ya wenyewe -cheche inayoshika kasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapigano ya wenyewe -cheche inayoshika kasi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwiba, Mar 18, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kut.Mwananchi.
  Ambrose Wantaigwa,Tarime

  MBUNGE wa Tarime Charles Mwera amewashutumu polisi kwa kutumia nguvu nyingi katika kukabiliana na mapigano ya koo ambazo zinasababisha vifo ambavyo vingeweza kuepukika.

  Mwera alisema matokeo yake, polisi wamempiga risasi kifuani na kumuua mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Nyamwaga wakati wakikabiliana na wapiganaji kutoka koo za Wairegi na Wanyabasi jana.

  Mbunge huyo alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Marwa chacha (17), ambaye alikuwa mita chache kutoka eneo la oparesheni za polisi hao kujaribu kukabiliana na wapiganaji wa koo hizo.

  Alisema kitendo cha polisi kutumia risasi za moto hata katika vijiji wanavyoishi raia wema wasiohusika na vita ni kibaya.

  ''Unapokwenda katika kijiji na kuanza kupiga risasi ovyo tegemea kuua watu wasiohusika kama ilivyotokea katika mwanafunzi huyu na sidhani kama kisheria adhabu ya mtu anayekamatwa katika mapigano ya koo anahukumiwa kifo tena bila kufikishwa katika vyombo vya dola, " alisema na kuongeza;'
  ''Sababu mojawapo inayokwamisha juhudi za kumaliza kabisa mapigano ya koo ni pamoja na mbinu za zima moto zinazotumiwa na polisi ikiwa ni pamoja na kukamata watu ovyo,''.

  Badala yake alipendekeza jeshi hilo kujikita zaidi kupambana na wezi wa mifugo wanaoiba mchana kweupe tena kwa kutumia silaha za kivita pamoja na kuwakamata watu wanaodaiwa kufanya uvamizi na kuchoma nyumba za wanavijiji.

  Wakati huohuo serikali mkoani mara imeandaa tamasha la amani litakalohusisha washikadau wote wilayani hapa ikiwa ni jitihada za kukomesha mapigano kati ya koo zote za kabila la wakurya.
   
Loading...