MTAZAMO
Platinum Member
- Feb 8, 2011
- 20,212
- 35,865
Mapigano ya Lepanto yalifanyika baharini tarehe 7 Oktoba 1571 kati ya Wakristo na Waislamu, meli zao zilipokutana katika Ghuba ya Patras (karibu na Ugiriki).
Lepanto ni jina la bandari zilipoondoka meli za Dola la Osmani, wakati zile za mshikamano wa Kikristo zilitokea Messina(Italia).
Ni kwamba mwaka 1571 Papa PiusV aliunganisha nchi za Kikatoliki katika "Liga Sancta" ili kuzuia Waturuki wa dola hilo wasiteke Ulaya nzima.
Waislam wa Kituruki miaka ya 1500 waliamua kutumia mwanya wa vuguvugu la kujitenga kwa Waprotestanti kutoka Kanisa Katoliki. Hivyo waliamua kuvamia nchi za Ulaya ili kueneza dini yao kwa nguvu ya upanga na vita kwa kuwalazimisha Wakristo kuwa Waislam.
Oktoba 7, 1571 Waislam wa Kituruki waliamua kuivamia Italy kwa kuanzisha vita ya baharini iliyojulikana kama Vita vya Lepanto (Ugiriki). Baba Mtakatifu wa wakati huo alikuwa Pius V. Papa Pius V alijua wazi kuwa Waislam walikuwa ni wengi kwa idadi kuliko Wakristo na ya kuwa Waislam walikuwa na meli nyingi za kivita kuliko Wakristo.
Hata hivyo Baba Mtakatifu aliamuru jeshi lake likisaidiwa na wanajeshi kutoka Spain kwenda baharini kupambana na Waislam.
Baba Mtakatifu aliamuru kila askari abebe Rozari na kuisali wanapokuwa vitani majini; pia aliamuru wananchi wa Italia waliobaki majumbani wafanye maandamo makubwa huku wakisali Rozari kuomba msaada wa Bikira Maria ili Wakristo washinde vita. Yeye mwenyewe alisali Rozari siku hiyo ya Oktoba 7.
Muda si mrefu habari zilimfikia Baba Mtakatifu kuwa Wakristo wameshinda vita na kati ya meli 242 za Waislam zimesalia meli 12 tu huku jumla ya Waislam 30,000 wakiwa wameuwa, takribani 8,000 wamejeruhiwa au kutekwa.
Kwa upande wa Wakristo ni watu 7,500 tu waliokuwa ama wameuawa au wamejeruhiwa au kutekwa ambao baadaye wengi wao walifanikiwa kutoroka.
Papa Pius V alitamka kuwa ushindi huo haujatokana na weledi wa askari wala ubora wa vifaa vya kivita bali ni ushindi uliotokana na maombezi ya Bikira Maria wa Rozari.
My take;
Tuombe Mungu tuendelee na ushawishi wa hizi dini zetu bila kushikiana mapanga. Amani na mshikamano wa kidini ni muhimu mno ili kuheshimiana kila mtu na imani yake. Amani ni tunu tuliyorithi kwa waasisi wa taifa letu tuitunze na kuendelea kutofautiana na kushawishiana bila chuki na vita.
Sent using Jamii Forums mobile app