Mapigano kati ya wakulima na wafugaji

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji

simba wa dodoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
930
Reaction score
1,024
habari wa jamvi leo nimekaa nikiwaza kipindi chs nyuma, kile kukicha mapigano yanazuka kati ha wakulia na wafugaji, haipiti miezi mitatu utaskia wanaliamsha dude sasa hali hii naona imetulia hivi sisikii tena wakipigana

hivi ni kweli wametulia hakuna vita tena au tangu mweheshima magu atie mkwala vyombo vya habari kureport matukio hayo na waandishi wametulia na wahariri wao.

Na kama siku hizi hakuna mapigano bhasi inabidi tuipongeze serikali kupitia waziri wake wa ardhi lukuvi kwa kazi kubwa nayofanya maana nchi imetulia nina muda sijaskia hata mitandao watu wakizibuana
 
Nadhani suluhisho litakuwa limepatikan kama sio kudhibitiwa kwa muda, ilikuwa ni aibu kwa nchi ambaye karibu asilimia sabini ni pori watu kugombania ardhi yakilimo na malisho.
 
Siku hizi mambo hufanyika kimya kimya, hamna kuripoti.
 
Wafugaji washanyoshwa. Walikuwa watemi sana, ela zao zimekuwa za moto kila mtu anaziogopa.
 
....nakumbuka wazee wa jadi waliitwa mpakani mwa Tanga na Manyara, wakadhamiria kuheshimianaa.
 
Nadhani suluhisho litakuwa limepatikan kama sio kudhibitiwa kwa muda, ilikuwa ni aibu kwa nchi ambaye karibu asilimia sabini ni pori watu kugombania ardhi yakilimo na malisho.
maana nakumbuka hata kwenye kampeni akisemaga kwamba atakemchagua waziri wa ardhi akishindwa kushughulika swala wakulima na wafugaji atamtimbua ndio maana jamaa mpaka leo kadumu
 
ITV na vyombo vingine vya habari walipigwa marufuku kuripoti habari za mapigano ya Wakulima na Wafugaji. TBC nayo kwao hizo huwa siyo habari. Kwa hiyo usidhani hamna mapigano. Ni kwamba haupati tena fursa ya kupata habari hizo lakini mapigano bado yapo
 
Back
Top Bottom