Mapigano - Ikwiriri. Ukweli ndio huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapigano - Ikwiriri. Ukweli ndio huu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mokoyo, May 22, 2012.

 1. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,784
  Likes Received: 1,970
  Trophy Points: 280
  Naomba kusema kuwa mgogoro unaoendelea huko Ikwiriri baina ya wafugaji na wakulima ni muendelezo tu wa matukio kama haya ambayo tumekuwa tunayashuhudia katika wilaya nyingine kama vile Kilosa, Kilindi, Hanang, Arumeru, Mbarali na kwingineko. Tatizo hapa si ukwasi walionao wafugaji au umasikini wa wakulima. La hasa ila ni tatizo la kimfumo ambalo limesababishwa na serikali yetu yenyewe. Kuna tatizo la kauli mbovu na za kibaguzi ambazo zimekuwa zinatolewa na viongozi wa serikali kuhusiana na wafugaji. Mfano kama unakumbuka kauli ya PM Pinda kule bungeni ya kuwa wafugaji warudi walikotoka. Hii ni kauli mbaya sana ambayo ina tafsiri nyingi kwa wafugaji ikiwa ya kujihisi kubaguliwa kutokana na kazi yao. Pia kuna suala la uhamishaji wa wafugaji kutoka katika bonde la Ihefu mwaka 2006 pasipo utaratibu maalum na kuwapeleka katika mikoa ya Lindi, Pwani na Morogoro jambo ambalo ndio sasa linalozua maafa haya yote.

  Ombi langu kwa serikali ni kujenga mfumo bora wa kifugaji ambao utakuwa unalinda maslahi ya mifugo na wafugaji wenyewe. Tazama kuna mikakati mingi ya kilimo ambayo kwa mtazamo wa haraka utaona kuwa hakuna nafasi kwa wafugaji kujiendeleza zaidi ya leo kuambiwa ondokeni Kilombero, ondokeni Rufiji, ondokeni Mbarali, ondokeni Arumeru. Sasa wataenda wapi?
   
 2. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,897
  Likes Received: 2,317
  Trophy Points: 280
  Mkuu kati ya watu wavivu sana wa kufikiri wewe unaweza kuchukua nambari wani!
  Una matatizo si ya kufikiri tu, bali hata kushindwa ku-extrapolate matokeo ya yale unayodhania.

  Haihitaji elimu ya sekondari kuelewa kuwa jangwa la huko Shinyanga na sehemu za Arusha limesababishwa na mifugo mingi kupita kiasi.

  Suluhisho?

  Lile suluhisho kama la mtoa posti hapo juu ni kuswaga mifugo na kwenda kwingine regardless of the effects caused huku nyuma.
  That is irresponsible, hatuishi enzi za Nuhu, leo ni karne ya 21.

  Kama mTanzania atataka abembelezwe kupunguza mifugo ili afuge kitaalam, wakati mali anazo-mifugo basi mtoa mada you are being reckless.

  Na ile ardhi iliyoharibika,iliyoachwa nyuma nani wa kuirutubisha?
  Na je nikiwa mchokozi ile ardhi iliyoachwa kule nyuma basi je wakulima kaidai kwa vile wafugaji wanai-disown-wanaikana ili wahamie kule wanakokwenda?

  Tatizo moja la mtu reckless kama mtoa hoja, ni kufikiri tatizo la wafugaji karne hii litatauliwa kwa kuhama hama kama miaka ya ujima.
  Mtu kama huyo hata akielimika na akitumia kompyuta bado ana asili yake tu kimawazao na kutaka kuishi kiujima.
   
 3. L

  Laizer Ole Naibio Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kuna umuhimu wa kuwa na mipango itakayoshirikisha wafugaji. Pia sisi wafugaji lazima tubadilike sasa. Ardhi na maji vinaendelea kuadimika. Wafugaji watafute ardhi ya kudumu waache kuhamahama. Ni vyema mpango wa kugawa maeneo kwa ajili ya wafugaji na Mpango wa Matumizi bora ya ardhi ukatekelezwa.
   
 4. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,724
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Niliwahi kusikia kutoka kwa Mbunge mmoja ya kwamba, Serikali haina Sera ya Mifugo, hivyo suala la ugawaji wa maeneo ya mifugo linakuwa gumu, na kupelekea vurugu baina ya wakulima na wafugaji. Mfano; huko Kilosa, Monduli, n.k hivyo wafugaji kujiamulia kadiri watakavyo.
   
 5. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,724
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Niliwahi kusikia kutoka kwa Mbunge mmoja ya kwamba, Serikali haina Sera ya Mifugo, hivyo suala la ugawaji wa maeneo ya mifugo linakuwa gumu, hivyo kupelekea matamko yasiyoangalia athari za mbali, pia kupelekea vurugu baina ya wakulima na wafugaji. Mfano; huko Kilosa, Monduli, n.k hivyo wafugaji kujiamulia kadiri watakavyo.
   
 6. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,784
  Likes Received: 1,970
  Trophy Points: 280
  sijaona hoja katika haya maneno yako zaidi ya kushindwa kuelewa historia ya chanzo cha migogoro baina ya wafugaji na wakulima Tanzania. Hakuna aliyekuambia kuwa wafugaji wameshindwa ku-settle sehemu moja na kuwa na mifugo michache, ni hisia zako. Suala la mifugo kuharibu ardhi sijui huko Shinyanga na kwingineko ni ukosefu tu wa mipango madhubuti ya kuhakikisha kuwa makundi yanayotumia ardhi yanaheshimu vipi mipaka yake.

  Wewe sio reckless ila una matatizo ya ushabiki pasipo kujua unachoshakia ni sahihi kweli au la. Kuna tatizo kubwa la utekelezaji wa sheria nchi hii ikiwa ni pamoja na sheria za ardhi. Na hili ndilo tatizo kubwa sana, husitizame mambo katika uelewa wa kipunguani kiasi hiki unaweza kuleta shida zaidi ya hiyo huko Ikwiriri.
   
Loading...