The Icebreaker
Platinum Member
- Apr 24, 2014
- 38,116
- 117,902
Okay πWanaopigana vita dhidi yao wao wenyewe ni watu wasiojitambua na ni watu wasiojua wanataka nini kwenye maisha yao,
Ni watu wanaoendeshwa zaidi kwa hisia kuliko akili,
Sijawahi kupigana vita dhidi yangu na wala haitatokea,kila ninachokifanya ni maamuzi yangu mimi kama mimi,sijawahi kujuta na wala sitakuja kujuta coz kila jambo hua na thamani kwa wakati wake,
Live the life you love,
Love the life you live.
Okay!Kumbe hujasoma mada uwii
Nguvu πͺwell done gentleman
Ipi hiyo?Kichwani mwako mbona kuna battle kubwa tu, malizana nayo kwanzaπ€£
Umemshauri vyema sana Madam, labda niongezee jambo hapa.Ni kwasababu unahofia atakuona je baada ya kumwambia kua huwezi hilo jambo lake
Lakini ukweli ni kwamba kusema hapana ni bora zaidi kuliko kutoa matumaini fake
Akikujia mtu anahitaji umsaidie jambo fulani ni kwasababu amekuamini na anadhani atasaidika
Lakini hiyo haina maana lazima umsaidie kwa namna anayotaka hapana badala yake unaweza kumpa mawazo au njia ya kutatua hata kama wewe umeshindwa kumsaidia lakini huo ni msaada tosha
CC: Marcostilone
Mkuu sio kwamba wewe hauna msimamo.shukran mkuu nitalifanyia kaz maana huwa najilaumu mfano mwaka jana kunandu gungu anaishi mwanza alinipigia simu akanieleza anashida ya lak 2 na nusu nikashinda kukataa ikanibid nimutumie hela ambayo ni ya mtaji wa biashara yangu mpak ikapelekea kuyumba kwa biashara mpaka leo huwa najilaumu kwa kukosa msimamo
Mkuu, kitu cha kwanza ni kujikubali mwenyewekwenye mazingira au matukio ya userious mathalani kwenye vikao vya ofisini au sehemu yoyote utakayohitajika utoe mawazo yako huku watu wakiwa attention kukusikiliza wewe.
KaribuAsante
Asante ndege Mdinya ππOkay!
Cognitive dissonance ni hali ya msuguano unaotokea kwenye akili yako pale unapokuwa na, (a) Imani mbili zinazopingana, (b)unachoamini hakifanani na tabia yako. Kwa mfano unajua JF inakupotezea muda lakini wewe bado unaendelea kuingia tu JF (inakuuma lakini huachi).
Unaoata stress. Katika kupunguza hizi stress akili inafanya mambo yafuatayo:
1. Unabadi imani juu ya jambo husika, kwa mfano unajisemea, "labda JF hainipotezei muda". Akili inatulia.
2. Kujihalalishia. Unajisemea, "mbona wengine wako tu JF masaa yote, nami naendelea tu kuperuzi". Akili inatulia.
3. Unapunguza uzito wa tatizo. Unajisemea, "hata hivyo sikai sana jukwaani". Akili inatulia.
4. Kuachana mazima na kile unavhoona hakikufai. Hii ni njia ngumu lakini ni muhimu sana. Unaacha kabisa kuingia JF unakwenda kulika mpunga majarubami na unapata manufaa makubwa.
NB: Akili ya binadamu hupendelea zaidi comfort zone ndiyo maana haitaki kuona unabadilika. Jaribio la kutaka kubadika ni tishio kwa akili yako, so yakupasa ujikaze sana.
Msome Leon festinger kwa mengi zaidi.
Sawa mkuuNakumbuka mwaka 2000 niliitwa na bibi yangu kijijini aliniambia mambo mengi sana ila maneno ninayoyakumbuka hadi leo aliniambia "mjukuu wangu ipo siku moja watu wengi watapoteza mda wao kusoma comment yako"
Thank you πUmemshauri vyema sana Madam, labda niongezee jambo hapa.
Ndugu shilaa hiyo ni vita ambayo watu wengi wanapambana nayo kimya kimya, wengi huwa wanaishia kusema ndiyo ili wasiwaudhi wengine, lakini mwisho wa siku huwa wanaishia kujiudhi wenyewe.
Kumbuka, kusema hapana pale ambapo huna uwezo ni self respect. Ukikubali kila ombi kwa kuogopa watu watakuchukuliaje, utaanza kubeba mizigo ambayo si yako, halafu mwisho wake stress na majuto vinakuwa sehemu ya maisha yako.
Sometimes, the most powerful word is simply No, watu wanaokuheshimu kweli wataelewa mipaka yako na wasiokuelewa, huenda walikuwa wanathamini manufaa wanayoyapata kwako kuliko ustawi wako.
Jifunze kusema, "Ningependa kukusaidia, lakini kwa sasa siwezi." Huu sio ubinafsi, ni wisdom. Ukijifunza hilo utaona amani ya moyo wako inaongezeka kuliko ulivyowahi kufikiria.
Kwanza kabisa ishi vile unavyopenda.Natoa angalizo kwa wale wa unashinda JF full-time
Huu ni kama ushauri tu kwamba hii mada inakuhusu isome yote ili uanze leo kupigana na hiyo tabia isiyopendeza ya kufatilia ni nani anaingia online sa ngapi na anatoka saa ngapi
Sisi wengine kuandika ni moja wapo ya enjoyment π
Na hii platform sio kama hizo zingine za kupost makalio au kutafuta attention hapa tulio wengi hatufahamiani
na hii inatupa uhuru wa ku share kujifunza kupiga story na kufurahia maisha kwa mtindo huo
kwa wale wote wanaovutiwa na nyuzi zangu guys nipo in love kwenu π₯° nawapenda sanaππ
Twende zetu sasa π
Mapigano yapo ya aina nyingi Umewahi kusikia nchi fulani ikiwa vitani?
Watu husema nchi A inapigana na nchi B. Hayo huitwa mapigano
Pia kuna mapigano kati ya watu wawili, mtu A na mtu B, kama vile yanavyotokea ulingoni( mtu anapigwa hata kwa TKO)
Hata wanyama nao hupigana mfano kuku, mbuzi na wengine
Lakini je, umewahi kujiuliza kama inawezekana mtu kupigana dhidi ya yeye mwenyewe?
Jibu ni ndiyo, inawezekana kuwa na vita au mapigano dhidi yako mwenyewe
Haya ni mapigano ambayo hayapiganwi kwa ngumi wala silaha, bali ni mapambano ya ndani ya nafsi
Ni pale unapogundua kuna kitu ndani yako ambacho hakikufanyi kuwa mtu unayetaka kuwa, hivyo unaamua kukikabili
Mfano unaweza kujijua kabisa una tabia fulani kama wivu, hasira au kutokuwa na subira
Baada ya muda unagundua tabia hiyo haikusaidii wewe wala jamii inayokuzunguka
Hapo ndipo vita vinaanza siyo dhidi ya mtu mwingine, bali dhidi ya hiyo tabia iliyopo ndani yako
Unaanza kujifunza kujizuia kujirekebisha na kuikataa ile hali ambayo haikupi thamani
Kwa mfano, kama zamani ulikuwa huwezi kukaa nyumbani na kila mara ulitamani kutoka, siku moja hamu hiyo inapokuja unaweza kujikuta ukisema
Hapana, siendi leo(unakaza)
Hapo unakuwa umeanza kupigana dhidi yako mwenyewe unayashinda matamanio yako kwa ajili ya lengo kubwa zaidi
Sasa swali la mjadalaπ
Wewe umewahi kuwa na vita au mapigano dhidi yako mwenyewe?
Ni nini kilishinda wewe au kile ulichokuwa unapambana nacho?
Ulipigana kwa muda gani, na ulitumia njia gani kushinda?
Nyongezaπ
Kabla hujaanza mapambano hayo, ni muhimu kujifanyia utafiti wa nafsi yako Jifahamu, tambua tabia zako, haiba yako na vitu vinavyokufanya uwe wewe
Baada ya hapo utaweza kuona kama kuna mambo ndani yako unayoyapenda au kuna mengine ambayo yanahitaji kubadilishwa
Kwa sababu wakati mwingine ushindi mkubwa wa mtu siyo kumshinda mwingine, bali ni kujishinda mwenyewe na kuwa yule mtu ambaye anatamani kuwa
Happy weekend π₯
ShesRise_1 βοΈ
kweli mkuu kwanza nimejihisi mwenye furaha baada ya kupata mawazo yenu hapa nimeajifunza kitu kiufupi mmenifundisha mbinu za kushinda vita vyangu kuliko ningepipana kimoyo moyoUmemshauri vyema sana Madam, labda niongezee jambo hapa.
Kumbuka, kusema hapana pale ambapo huna uwezo ni self respect. Ukikubali kila ombi kwa kuogopa watu watakuchukuliaje, utaanza kubeba mizigo ambayo si yako, halafu mwisho wake stress na majuto vinakuwa sehemu ya maisha yako.
Sometimes, the most powerful word is simply No, watu wanaokuheshimu kweli wataelewa mipaka yako na wasiokuelewa, huenda walikuwa wanathamini manufaa wanayoyapata kwako kuliko ustawi wako.
Jifunze kusema, "Ningependa kukusaidia, lakini kwa sasa siwezi." Huu sio ubinafsi, ni wisdom. Ukijifunza hilo utaona amani ya moyo wako inaongezeka kuliko ulivyowahi kufikiria.
π€£π€£π€£ wewe weekend leo upo wapKwanza kabisa ishi vile unavyopenda.
Amejuaje kama uko full time kama na yeye hayuko hivo.
Kila mtu afanye anachokipenda.
Watuache.
Yes π₯π₯π₯π₯π₯π₯π₯π₯π₯π₯Argentina Bingwa
Full time Argentina 2 Spain 1
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...hiyo tabia isiyopendeza ya kufatilia ni nani anaingia online sa ngapi na anatoka saa ngapi
Mfano unaweza kujijua kabisa una tabia fulani kama wivu, hasira au kutokuwa na subira
Baada ya muda unagundua tabia hiyo haikusaidii wewe wala jamii inayokuzunguka