Mapenzi yasipokuwa na Uhuru ni kero

Mapenzi yasipokuwa na Uhuru ni kero

Muuza simu used

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
4,393
Reaction score
7,107
Kwa kifupi huwa napenda uhuru hasa ninapokuwa kwenye mahusiano! Kwenye maongezi ama chating sipendi maswali mengi mengi yasiyokuwa na tija,ama upo wapi? unafanya nini? Na nani? Kwa nini? ili iweje?

Demu anapogeuka askari mpelelezi kwenye maisha yangu kwangu mimi nakereka sana! Mwanamke anayelazimisha mchati usiku kucha bila jambo lolote la msingi na hana hoja yoyote ya muondelezo wa story huwa naboreka sana!

Mwanamke anayekuja gheto mara kwa mara bila taarifa yeyote ni kero iliyotukuka! Nimeshawahi kuacha mwanamke kwa sababu tu alikuwa anakuja ghetto wakati wowote siku yoyote bila taarifa na hata siku moja hajawahi kunipa taarifa kwa muda wa mwaka mzima aisee nilivumilia hata nikaamua kuachia ngazi maana ukimwambia anakuwa Mkali!

Mapenzi yakuchunguzana kwangu ni big No!

N:B, Mchunguze tu endapo ni mkeo ama mumeo ili ujue unaishi na mtu wa namna gani na wale sio mpita njia
 
Hyo n kero haswaa mimi mwenyewe nshamwacha janaume kutwaa kuja kwangu bila taarifa hata sa nane za usiku utafkir kwake hata kodi hanilipii shenzzz n sahihi kero hizo bora uwe single tu

Ni kweli ni kero sana,sometimes mtu huna hata mood ya mapenzi labda unataka ukae utulize akili yako kidogo mara unashangaa mtu huyo ameshafika [emoji17]
 
Mimi kero kuu ni kudai muamala yaani hapo ni magufuli na lissu, hayo mengine tutaelekezana tu jinsi ya kuishi
Mwengine anadai hela kama alikukopesha vile kumbe ni hisani tu.
Juzi nimekutana na mwamba MPesa kibandani. Jamaa analalamika demu anampigia simu mfululizo yani hapumui. Hadi kakasirika badala ya 10k katuma elf 5 tu kumkomesha maana msumbufu sana.
 
Mkipendana hakuna kero. Ila kama haumpendi nikerosana
Hakika, mie kuna GF wangu enzi nipo chuo tulikuwa hatuwezi maliza 3 hours bila kutextiana.

We were at the same class ila mda ambao hatutext ni Lecture ikiwa on session. After sessions lazma demu aje magetoni tunakaa hadi usiku mnene tunakulana mchebwede tu.

Nilikuwa hata prep siendi so wana wakiwa madarasani jioni mie nakula zangu burudani na mlimbwende. Uzuri nilikuwa smart class, pepa zikikaribia nakula vitini na mama tunasongesha.

Kimsingi sijawahi kuchoka ile companionship and that because i was so in love with her.
 
Sasa mbona hizo kero ndio mapenz yenyewe...?

Mi nadhan kero ni pale mtu anapo lazimisha ufanye vitu vilivyo nje ya uwezo wako...

Kama kitu kipo ndan ya uwezo wako na unaona kero kufanyia mwenzi wako basi hapo kero ni upendo hakuna upendo Kati yenu
 
Hakika, mie kuna GF wangu enzi nipo chuo tulikuwa hatuwezi maliza 3 hours bila kutextiana.

We were at the same class ila mda ambao hatutext ni Lecture ikiwa on session. After sessions lazma demu aje magetoni tunakaa hadi usiku mnene tunakulana mchebwede tu.

Nilikuwa hata prep siendi so wana wakiwa madarasani jioni mie nakula zangu burudani na mlimbwende. Uzuri nilikuwa smart class, pepa zikikaribia nakula vitini na mama tunasongesha.

Kimsingi sijawahi kuchoka ile companionship and that because i was so in love with her.
Then after, what happened?
 
Back
Top Bottom