Mapenzi yapo, lakini hakuna kumpenda mtu mwingine

Mapenzi yapo, lakini hakuna kumpenda mtu mwingine

FATHER OF REALITY

Senior Member
Joined
Nov 3, 2014
Posts
123
Reaction score
100
Habari zenu wanajamvi, leo nimewalatea tafakari fupi juu ya kile kiitwacho mapenzi baina ya watu wawili wa jinsia tofauti. Kwa ufupi binadamu ana hisia za za mapenzi, tena zilizo kali sana, ila yale mapenzi au hizo hisia hujengwa juu ya asili ya binadamu ambao ni ubinafsi, kwa sababu hii, megundua kwamba hakuna swala la kumpenda mtu mwingine, yaani mwanmke au mwanaume, bali kila mtu hujipenda mwenyewe kwa kupitia huyo amwitae mpenzi wake, kwa sentesi ya kiujumla wewe ujiitae mpenzi wa mwanume au mwanamke fulani, ukijichunguza vizuri, wewe ni mpenzi wa wewe mwenyewe au kwa lugha rahisi wewe ni mpenzi wa nafsi yako.

Najua mada hii haitawapendeza sana wale wenye wapenzi waliowaambia wamewafia kimoyo,au wale walioingia kwenye mapenzi kwa mara ya kwanza, na kwa sababu hiyo wakapata bubujiko la furaha moyoni, ambayo pia haina dhamana ya kudumu (guarantee), kumbuka wengi wamewaua wale waliodai kuwa wanawapenda na wamewapa mioyo yao.

Nafikiri sasa umeanza kunielewa namaanisha nini. Kila mtu anajipenda mwenyewe ndugu, usidanganyike kuwa kuna kumpenda mtu mwingine, hebu fikiri juu ya yule uliyesema unampenda, mbona ulipomfumania penzi likafa, au ukaingia mgogoro na kipenzi wako, ni nani awezaye kuikorofisha nafsi yake aipendaye, mbona umejikosea maranyingi lakini ukajisamee asilimia 100.

TAZAMA UNAPOMTAFUTA MPENZI KWA MAANA YA MKE AU MUME au vinginevyo, kwa nini unaweka vigezo vyako, na hivyo vigezo ni kwa kumfurahisha nani kama si nafsi yako, na ndio mana kwa kujipenda ukawa na mpenzi ambaye uliamini atakuwa nyenzo ya wewe kijipenda, baadaye ulipogundua yeye si nyenzo sahihi ya wewe kujipenda, ukimtosa, hivi, umeshawahi kujiuliza zile hisia kali za kwanza za mapenzi kwa mwenzi wako uliyemtosa au unayetaka kumtosa zimeenda wapi, na iweje leo ukamtosa mtu umpendaye, huogopi kuutesa moyo wake, jibu, humpendi bali wajipenda mwenyewe, na huyu amehatarisha mpango wa wewe kujipenda kupitia yeye, UNAMUONDOA.

Namalizia, HIVI UMEWAHI KUJIULIZA, KWANINI MPENZI WAKO AKIKWAMBIA NAKUPENDA, NA USIPOMJIBU NAKUPENDA PIA, UWA INALETA MGOGORO? KAMA ANAKUPENDA AKIKWAMBIA WEWE TU SI INATOSHA, KWANINI NAYEYE ANADAI UMWABIE UNAMPENDA, hii ni kuthibitisha kwamba lile neno '' NAKUPENDA'' ni kwa ajili ya asemaye ili kuchokoza kupata neno lile limfurahishalo toka kwako, hivyo si dili maana hilimaanishi kisemwacho. ila mapenzi yapo.

Hujasikia mwanake anatoka nje ya ndoa akisema mume wangu haniridhishi kitandani au hata mwenendo wake, na mwanaume hali kadharika, kule kuridhishwa ndio kujipenda yeye mwenyewe, maana kama mume karidhika nawe kitandani ya nini ustoke au kama mke karidhika nawe ya nini utoke na mpenzi mwingine kama wampenda, jibu ni kwamba kila mmoja hujipenda mwenyewe, humtumia mwenzie kujifurahisha na furaha hiyo ni yake binasi, ndio mana mtu mmoja huwa na wapenzi wengi, ni ubinafsi juu ya kutafuta raha yake.

KARIBUNI, leta hoja, si lazima uamini, ila PIMA.
 
Habari zenu wanajamvi, leo nimewalatea tafakari fupi juu ya kile kiitwacho mapenzi baina ya watu wawili wa jinsia tofauti. Kwa ufupi binadamu ana hisia za za mapenzi, tena zilizo kali sana, ila yale mapenzi au hizo hisia hujengwa juu ya asili ya binadamu ambao ni ubinafsi, kwa sababu hii, megundua kwamba hakuna swala la kumpenda mtu mwingine, yaani mwanmke au mwanaume, bali kila mtu hujipenda mwenyewe kwa kupitia huyo amwitae mpenzi wake, kwa sentesi ya kiujumla wewe ujiitae mpenzi wa mwanume au mwanamke fulani, ukijichunguza vizuri, wewe ni mpenzi wa wewe mwenyewe au kwa lugha rahisi wewe ni mpenzi wa nafsi yako. Najua mada hii haitawapendeza sana wale wenye wapenzi waliowaambia wamewafia kimoyo,au wale walioingia kwenye mapenzi kwa mara ya kwanza, na kwa sababu hiyo wakapata bubujiko la furaha moyoni, ambayo pia haina dhamana ya kudumu (guarantee), kumbuka wengi wamewaua wale waliodai kuwa wanawapenda na wamewapa mioyo yao. Nafikiri sasa umeanza kunielewa namaanisha nini. Kila mtu anajipenda mwenyewe ndugu, usidanganyike kuwa kuna kumpenda mtu mwingine, hebu fikiri juu ya yule uliyesema unampenda, mbona ulipomfumania penzi likafa, au ukaingia mgogoro na kipenzi wako, ni nani awezaye kuikorofisha nafsi yake aipendaye, mbona umejikosea maranyingi lakini ukajisamee asilimia 100. TAZAMA UNAPOMTAFUTA MPENZI KWA MAANA YA MKE AU MUME au vinginevyo, kwa nini unaweka vigezo vyako, na hivyo vigezo ni kwa kumfurahisha nani kama si nafsi yako, na ndio mana kwa kujipenda ukawa na mpenzi ambaye uliamini atakuwa nyenzo ya wewe kijipenda, baadaye ulipogundua yeye si nyenzo sahihi ya wewe kujipenda, ukmtosa, hivi, umeshawahi kujiuliza zile hisia kali za kwanza za mapenzi kwa mwenzi wako uliyemtosa au unayetaka kumtosa zimeenda wapi, na iweje leo ukamtosa mtu umpendaye, huogopi kuutesa moyo wake, jibu, humpendi bali wajipenda mwenyewe, na huyu amehatarisha mpango wa wewe kujipenda kupitia yeye, UNAMUONDOA. Namalizia, HIVI UMEWAHI KUJIULIZA, KWANINI MPENZI WAKO AKIKWAMBIA NAKUPENDA, NA USIPOMJIBU NAKUPENDA PIA, UWA INALETA MGOGORO? KAMA ANAKUPENDA AKIKWAMBIA WEWE TU SI INATOSHA, KWANINI NAYEYE ANADAI UMWABIE UNAMPENDA, hii ni kuthibitisha kwamba lile neno '' NAKUPENDA'' ni kwa ajili ya asemaye ili kuchokoza kupata neno lile limfurahishalo toka kwako, hivyo si dili maana hilimaanishi kisemwacho. ila mapenzi yapo. Hujasikia mwanake anatoka nje ya ndoa akisema mume wangu haniridhishi kitandani au hata mwenendo wake, na mwanaume hali kadharika, kule kuridhishwa ndio kujipenda yeye mwenyewe, maana kama mume karidhika nawe kitandani ya nini ustoke au kama mke karidhika nawe ya nini utoke na mpenzi mwingine kama wampenda, jibu ni kwamba kila mmoja hujipenda mwenyewe, humtumia mwenzie kujifurahisha na furaha hiyo ni yake binasi, ndio mana mtu mmoja huwa na wapenzi wengi, ni ubinafsi juu ya kutafuta raha yake. KARIBUNI, leta hoja, si lazima uamini, ila PIMA.

Dear Asante kwa somo hili na kutukumbusha. Thanks!
 
Nakubaliana na wewe hata waliochukua pesa za escrow ni wabinafsi na wanajipenda wenyewe
 
hii mada ilishaletwa hapa na ikajadiliwa na ikamalizika. ama hii ni part 2?
 
Tafakari njema hii, umenikumbusha mada fikirifu za siku za nyuma MMU
^^
 
Back
Top Bottom