Mapenzi yanayoanza kufa

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Penzi huwa halidondoki na kufa ghafla kama mgonjwa wa degedege na beriberi, penzi huwa linakufa kwa process zinazoonekana lakini zinazodharaulika. Dalili za penzi linalotaka kufa huwa ni kama dalili za malaria, utaona tu dalili kichwa kitauma.

Mwili utakuwa mzito na homa ukidharau ukanywa tu panadol ndo watu huzidiwa na kufa ghafla. Usidharau ukiona vimelea vya penzi linaloumwa ukiona penzi lako lina homa litafutie tiba stahiki kabla hali haijawa tete na chronic likalazwa icu na hatimaye kukata roho maana hutaamini macho yako kwamba limekufa kwa ka- homa haka tu.

Dalili za homa ya penzi huwa ziko wazi ila tunazipuuziaga na kuziona oya-oyakama unamjua mpenzi wako utaona tu anavyochange na kuanza kupata vipele vya baridi. Atabadilika anavyoongea na wewe. Attention anayokupa si kama zamani. Visingizio kibao badala ya kuomba msamaha akikosea na communication inayoyumba-yumba kama mlevi wa wanzuki.

Usipotibu penzi lenye homa jiandae kwa mazishi.Simple and clear kama malaria isivyokubalika Africa, usikubali homa ya penzi iue mahaba yako uliyonayo kwa hubby ake.

Tibu homa pale inapotokea usisubiri ulazwe ndo utafute kwinini..

-stunter-
 
Kwa hiyo penzi lako na jje's limekufa kwa style hiyo mkuu?........inaonekana hiyo homa ilikuwa kali sana!
 
kufa kwa mahaba hakuna dawa wala huwezi kuyatibu ni kama sikio la kufa vile
 
Penzi huwa halidondoki na kufa ghafla kama mgonjwa wa degedege na beriberi, penzi huwa linakufa kwa process zinazoonekana lakini zinazodharaulika. Dalili za penzi linalotaka kufa huwa ni kama dalili za malaria, utaona tu dalili kichwa kitauma.

Mwili utakuwa mzito na homa ukidharau ukanywa tu panadol ndo watu huzidiwa na kufa ghafla. Usidharau ukiona vimelea vya penzi linaloumwa ukiona penzi lako lina homa litafutie tiba stahiki kabla hali haijawa tete na chronic likalazwa icu na hatimaye kukata roho maana hutaamini macho yako kwamba limekufa kwa ka- homa haka tu.

Dalili za homa ya penzi huwa ziko wazi ila tunazipuuziaga na kuziona oya-oyakama unamjua mpenzi wako utaona tu anavyochange na kuanza kupata vipele vya baridi. Atabadilika anavyoongea na wewe. Attention anayokupa si kama zamani. Visingizio kibao badala ya kuomba msamaha akikosea na communication inayoyumba-yumba kama mlevi wa wanzuki.

Usipotibu penzi lenye homa jiandae kwa mazishi.Simple and clear kama malaria isivyokubalika Africa, usikubali homa ya penzi iue mahaba yako uliyonayo kwa hubby ake.

Tibu homa pale inapotokea usisubiri ulazwe ndo utafute kwinini..

-stunter-
Kweli mtupu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom