Mapenzi yanatesa kuliko kitu chochote

Hendisamu

JF-Expert Member
May 9, 2019
319
500
Habari za wakati huu wakuu, bila shaka hamjambo na kheri ya sikukuu ndugu zetu Islamic members over the World.

Moja kwa moja kwenye mada. Aisee tusichukulie poa kabisa kuna watu wanateseka sana zaidi ya maumivu ya kuungua moto sababu ya mapenzi.

Unakuta girl au boy kakata tamaa kabisa hana matumaini ya kumpata ubavu wake, age inasonga, maisha magumu, hana wa kumfariji, mateso mateso mateso kwa moyo yanachoma yanaunguza.

Mbaya zaidi na cha kushangaza hawa ndiyo watu ambao akitongozwa au akipendwa huwa ni wagumu sana kutoa support eti kwa kigezo cha kuwa MAKINI asije kuachwa hovyo hovyo.

Kumbe sometimes anazidisha umakini hadi anaamfukuzisha ambae angekuwa ubavu wake wa kweli.

Hapo sasa wengine wanakata tamaa kabisa tena kwa kitu kikali wanajijeruhi upendo wao unatoweka kabisa maana anajiona hawana bahati.

Ngoja niwape moyo, ukitafuta mpenzi ukiwa na pressure yaani ukiwa bado hujatuliza moyo wako kwa kulidhika na hali ya kuwa single, nakwambia utapishana sana na watu sahihi.

Wasalaaam!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom