candymarry
Member
- Aug 4, 2012
- 32
- 8
Habari wana Jf/MMU, ni kwa muda sasa tumekuwa tukipata habari za kusikitisha sana,nyingi zikihusisha wapenzi/wanandoa kuuana mara baada ya migogoro ya muda mrefu kati yao,yote hii ni kutokana na upande mmoja kuto kukubaliana na swala la wapenzi hao kuachana!, hasa hasa ni upande wa wenzetu wanaume kuto kukubali swala zima la kuachwa! kitu ambacho hutokea pia pale wawili wanapoamua kuwa wapenzi...nimejiuliza kwanini mtu anaamua kufikia kufanya maamuzi ya kinyama ya kukatisha uhai wa mpenzi/mke wake kisa ameachwa!? hebu wana Great Thinkers tujadili kuhusu hili..kwanini mtu usikubali matokeo kama alivyokubali matokeo ya mwanzo kwamba umekuwa wapenzi lakini at the end of the day "No one knows what the future holds"