creedfx
Senior Member
- Jun 24, 2022
- 103
- 58
Kuna baadhi ya watu huja kwenye maisha yako kama zawadi... lakini wengine huja kama darasa la maumivu. Na darasa hili lilinifundisha kuwa… mapenzi si ya waliokomaa tu, bali ni ya waliovunjika na wakaamua kupona.
Hii ni hadithi yangu. Ya kweli. Niliipenda kimya, nikaamini ni dua yangu ikijibiwa… kumbe ilikuwa jaribio. Kama unavyoamini kuwa ukimpenda mtu kwa kweli, basi hata Mungu atamfanya awe wako basi utataka kusoma hadithi hii hadi mwisho.
Mapenzi si wakati mzuri, ni moyo sahihi. Na wakati mwingine moyo unaokuja sahihi, huja kwa lengo la kukuvunja ili ukubaliane na wewe kwanza. 💔 Ukweli ni kwamba wengi ambao hatujaoa huwa tunaomba: "Ya Allah, nakuomba mke/mume mwema."
Lakini hatuombi tu mtu mwenye tabia nzuri, bali pia mwenye mvuto, sura ya kichwani, tabia za kidini, busara, akili, na roho nzuri. Tunaamini tutampata tukiwa tayari. Tunajiambia: "Nikishajijenga, nitamtafuta ninayemtaka."
Miaka yangu ya kuwa single niliitumia sana kujijenga kimya kimya. Nikajizuia tamaa, nikatengeneza nidhamu, nikasema: "Nikishapata kazi, kipato na msimamo... nitamtafuta malkia wa maisha yangu."
Sikujua kuwa Allah hamuandai yeye aje kwangu, bali huwa anaandaa mimi kwa kile ninachodhani nakihitaji. Na hapo ndipo majibu ya dua huja kama darasa kabla ya kuwa zawadi.
📍 Ilikuwa mwaka wangu wa mwisho chuoni. Sikuwa na kitu zaidi ya elfu kumi ya kula. Siku moja jioni, nikatoka kutuliza akili. Jua la Dar lilikuwa linazama polepole, mvua ikaanza kunyesha. Sina mwavuli. Nikajibanza kwenye duka lililofungwa.
Ndipo nikamuona...
Msichana mrefu, mwenye macho ya kihistoria, suruali nyeusi nyepesi, akishikilia gauni lake lililodariziwa mithili ya lile la princess Cinderella, nywele simple zimefungwa kitaalamu na kitambaa. Kiukweli Alikuwa picha ya yule niliyemuona kila nikisali.
Sijui ujasiri ulitoka wapi. Nikamwambia: "Samahani... naweza simama chini ya mwavuli wako?"
Akaniangalia kwa macho ya mtu aliyezoea kukataliwa lakini bado na chembe ya upole. Akasema: "Usijali, njoo. Ila naelekea huku, kama nawe unaenda, twende wote."
Hatukuongea sana. Lakini kimya kilisema kila kitu. Tulitembea wote mvua ikidondoka mithili ya baraka. Kabla hajaondoka, nikamuuliza: "Naweza kukupata tena baada ya hapa?"
Akanipa namba yake.
Nilihangaika siku kadhaa nikijiuliza: "Nimtafute au nisisumbue hisia zangu?" Lakini nikajikaza. Nilimtumia ujumbe. Nilishangaa alivyopokea vizuri. Tukawa marafiki. Siku moja alikuja nyumbani, tukapiga stori.
Akanisimulia historia yake ya mapenzi. Alisema:
"Nilimpenda mtu kwa miaka 8. Nikajitoa, nikavumilia. Lakini alinisaliti. Bila huruma."
Nilihisi huzuni nikimsikiliza. Nikamwambia: "Maumivu yako ni yangu sasa. Sitakuruhusu uliumie tena."
Nilitaka kuwa tiba ya historia yake. Nikapenda kwa dhati. Nikamwona kama dua yangu. Nikaanza kupanga maisha, kujijenga kwa ajili yake.
Siku moja alileta chakula, akaniita mpenzi wake, akaniambia ananiona kama mume. Niliona ndoa kwenye ndoto zangu.
Lakini siku zilivyoenda, mambo yakaanza kubadilika. Ukimya, baridi. Nikaamini labda bado anapona vidonda vya zamani.
Mpaka siku moja akaniambia:
"Naumia sana na sijui kwa nini... natamani niwe peke yangu."
Majibu yakawa ya baridi. Sauti ya moyo wake ikawa mbali. Hatimaye akasema:
"Samahani. Nimeshindwa kukupenda. Usinitafute tena. Na wala sitaki Sitaki huruma yako."
Nililia kimya kimya. Sikuweza kula. Niliona dunia inanizonga. Akili yangu ilikuwa kwenye mitihani, lakini moyo ulikuwa umevunjika vipande vipande.
Nikamtumia rafiki yake kumjua hali yake. Lakini akarudi na SMS yenye sumu:
"Najua unachopitia. Naomba usimsumbue tena. Hata mimi naumia. Usinijali. Usinitafute tena. Hutakuwa wa kwanza wala wa mwisho. All the best."
Nilikaa kimya. Sikumjibu. Sikutaka kumkimbilia mtu anayekimbia kivuli chake mwenyewe.
Nikabaki na dua moja:
🕊️ Hasbiyallahu la ilaha illa huwa, alayhi tawakkaltu wa huwa Rabbul Arshil Adheem.
Mwenyezi Mungu ananitosha. Yeye pekee ndiye wa kumtegemea.
Nilijifunza kuwa:
• Mapenzi si zawadi kila mara, mengine huja kama darasa.
• Si kila anayekuja na mvua ni baraka; wengine huleta mafuriko.
• Si kila anayekufanya ucheke leo atakufanya ulie kesho.
Leo siogopi tena kuumizwa. Ila naogopa kumpenda mtu asiye tayari kuwa zawadi , bali kuwa jaribio jingine.
Na sitamani hata kumshauri mtu aoe, hadi ajijue, ajijenge, na ajipende kwanza.
Nimeandika hili si kwa huruma, bali kwa kutupa mzigo moyoni. Maumivu hayaponywi kwa kunyamaza bali kwa kusimulia, ili wengine wajifunze kabla hawajavunjika.