Mapenzi yakivunjika huwa unafanya nini?

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Kwa sisi wanawake tulio wengi kama umeachwa au umemfumania umpendae tunahisi maumivu makali hadi kutamani kuzimia

Mawazo, maumivu ya kichwa, mwili kuwa na joto na uchovu, hapa sitaki niongee kuhusu mahusiano tena,hata kama mwanaume ataninitongoza naweza kumjibu vibaya

Baada ya siku kadhaa hivi nachukua simu naingia WhatsApp, insta au fb au kwenye orodha ya majina ya simu halafu naanza kuangalia kati ya wanaume waliowahi kunitongoza nikamkatalia ni nani handsome na alikuwa serious na mimi

Nitaselect jina nitamtumia sms "Mambo" akinijibu atajiongeza mwenyewe kwa nini leo nimemtafuta

Sasa wale wanaume mnaokataliwa wakati mnatutongoza halafu mnaishia kutoa mabango na lugha za kashfa hii nafasi huwa inawakosa
 
Nilishawahi kumuacha mwanamke huyo kumbe sipo tayari nilikoma kenge Mimi!!
Nilifuta namba zake zote! Mbona nilianza kuzitafuta😜

Uzuri akanitafuta tukarudiana hapo ndo nikaanza kujiandaa kumuacha! Nashukuru nilifauru kumuacha nikajua na mapenzi ni nini..!! Na hapo ndo nikaelewa kwanini baadhi ya vitu vimeandikwa "SHAKE BEFORE USE!".

Ushauli Kama mtu umempenda usimuache kwa pupa utakufa kikenge na ukiona haeleweki Anza kukaa mguu nje mguu ndani.. wachache watanielewa.
 
mi nikiona dalili tu najihami namwambia hivi wewe ndo wakunifanyia maringo hvo akat nshakugalagaza mara kibao, unakipi kipya mbele yangu? then namtumia nakuckilizia majibu
 
Kwa mwanaume anayejibiidisha,au anayejisimamia mwenyewe kwa mahitaji na kila kitu, mara nyingi ni ngumu kuachwa hata akiachwa wapo wanawake watakaojileta,kwa sababu wanawake wengi wanataka mteremko
 
Mimi jana nimeacha mtu jana afu sielewi nimemuachaje...
Akalia wee...
Leo ndio mimi naanza kupata maumivu. Dah!
 
Kwa mwanaume anayejibiidisha,au anayejisimamia mwenyewe kwa mahitaji na kila kitu, mara nyingi ni ngumu kuachwa hata akiachwa wapo wanawake watakaojileta,kwa sababu wanawake wengi wanataka mteremko
upo nje beat(mada)
 
Nilishawahi kumuacha mwanamke huyo kumbe sipo tayari nilikoma kenge Mimi!!
Nilifuta namba zake zote! Mbona nilianza kuzitafuta😜

Uzuri akanitafuta tukarudiana hapo ndo nikaanza kujiandaa kumuacha! Nashukuru nilifauru kumuacha nikajua na mapenzi ni nini..!! Na hapo ndo nikaelewa kwanini baadhi ya vitu vimeandikwa "SHAKE BEFORE USE!".

Ushauli Kama mtu umempenda usimuache kwa pupa utakufa kikenge na ukiona haeleweki Anza kukaa mguu nje mguu ndani.. wachache watanielewa.

Hii ilinitokea nikiwa najiandaa kufanya pepa la financila Report.

Basi tukazinguana kidogo nikakimbilia kusema ka vipi tuachane..
Mama yangu weweee.. nilipata matatizo ya dunia, consolidation statement iligoma kukalilika. Niliomba msamaha kama tahira lakini mchumba alikataa kata kata. Eti nimezoea😂😂

Ikanibidi nimuambie nipo kwenye pepa, fanya ata kuniigizia kuwa umenisamehe. Bado akagoma..

Jamani mapenzi yanauma nyie. Maana nilikuwa mweu gafla. Nikaanza na kuongea peke angu..

Japo miaka imepita, ila popote ulipo we mwanamke nakuombea upate corona maana unaroho mbaya sana boya wewe..

Yani kakosa kenyewe ata akaeleweki et na msamaha ninyimwe😂😂 dah
 
Mkuu inaonekana ulishindwa bembeleza!
Unatakiwa unatia vokali mpaka kushinda neno msamaha wenyewe!
Usipende kuwaambia hao viumbe kuwa asipokukubalia utazurika ndo atataka uzurike sasa akuone😂😂

mi ndo nilijulia hapo kuwa mapenzi yanauma nikarudi nyuma nikapanga majeshi nikaamua sasa.. mpk leo sikuwahi kumtafuta
Kama mtu hujajipanga usiache bora ukakaanae huku unajiandaa kumuacha alasivyo unaweza tangazwa hata TBC mtu kajitia kamba😎

Mapenzi kiboko ukipenda ile kupenda😜
 
Back
Top Bottom