Tumekuwa pamoja kwa miaka miwili sasa plus miaka miwili ya kuzungushwa inakuwa minne. Nampenda sana na ndo mtarajiwa wangu Mungu akijalia. Kwa muda wa mwaka mmoja sasa hivi yuko mbali kabisa nami ila navumilia na sijawahi kumcheat. Lakini kuna tabia imejitokeza kama miezi mitatu hivi simuelewi kwa kweli.
Nikipiga simu muda mwingine hapokei wala hata kunitumia msg kwamba yuko busy hakuna, natuma msg hajibu. Kuna wakati akipokea maongezi yake hata nnavyoongea na dada yangu aliyenizidi miaka 25 huwa nafurahia kwani huwa tunataniana. Majibu yake ni mkato na ukimwambia i love you anakujibu, ok! Hii ni tofauti na mwanzo. Nimezoea kila asubuhi na mapema kumsabahi na kumtakia kazi njema lakini siku hizi anapokea cm na kuniambia ana usingizi hata kama ni muda ambao mfanyakazi anatakiwa aamke. Kuna siku ndo kabisa sauti ilikuwa kama kuna breakfast inaendelea, loh!
Nilikata simu na kwenda kufanya mambo yangu. Jana nimempigia simu akawa anaongea kiuoga nikamuuliza, are you at your home? Akakata simu na mpaka leo hapokei. Kuna wakati huwa ananambia simu ni mbovu lakini bado najiuliza mbo wakati mwingine unampigia na kuongea naye? Nifanyeje ndugu zangu? Yaani hata ibada yangu leo imekuwa sio kama kawaida.
Nyalotsi, you are scared of the obvious! It is as you are thinking, she busy elsewhere, its a fact you have to live with for now, please forgive yourself and pick yourself and keep going at least you are alive! Keep living your life .......The Lord will provide for you!