Mapenzi ya mbali yananichanganya!

Mapenzi ya mbali yananichanganya!

yani wewe na akili zako zote unashindwa kujua..manzi kama hakukubali ukimtell i love u anakwambia ok..ama thanks..jombaa..Jipangeeeeeee warembo wote hawa we unakomaa na long distance? amin kwamba kuna mtu anakula mzigo huo...
Mi huwa nawaambia wanaume kuwa kamwe usimuonyeshee mpenzi wako wa kike/mke wako kuwa unampenda sana. Mwanamke akishakusoma hivyo atakushika mapembe na wewe kazi yako itakuwa ni kumfuata yeye atakako. Sasa mwenzetu pamoja na vioja anavyofanyiwa anaomba ushauri. Hivi ukifiwa huwa unahitaji kutafuta ushauri kwa watu, kwamba wakushauri labda uzike au upeleke maiti hospitali? Hapo huwa hakuna ushauri, ukifiwa wewe kazi yako ni kuzika tu, sasa huyu kaona mwanamke kabadilika na anaonyesha dalili zote za kupata mwanamme mwingine yeye yuko nyuma ya keyboard kuomba ushauri. Wewe mpige chini na jifanye kama huna time naye tena. Baada ya muda yeye ndio ataanza kukutafuta. Na kama kweli akili zako hazikutoshi utamrudia.(Ni kama nakuona vile). I never commit to women because doing so is harmful to your health!
 
Pole sana,i can imagine maumivu unayoyapata kwa sasa.Hiyo ilinikuta mm j2 iliyopita aisee nashindwa ht kusimulia yaan kanisan hapakukalika ila nashukru angalau sasa nimeanza kuzoea.
 
Yupo nje ya nchi au?

Wewe mueleze malalamiko yako then majibu atakayokupa ndiyo yatakupa muongozo wa maamuzi sahihi ya kuchukua.
 
kusoma hujui, hata picha tu?????
ukisikia chwii chwiii chwiii ujue keshanasa mtegoni
 
Tumekuwa pamoja kwa miaka miwili sasa plus miaka miwili ya kuzungushwa inakuwa minne. Nampenda sana na ndo mtarajiwa wangu Mungu akijalia. Kwa muda wa mwaka mmoja sasa hivi yuko mbali kabisa nami ila navumilia na sijawahi kumcheat. Lakini kuna tabia imejitokeza kama miezi mitatu hivi simuelewi kwa kweli.

Nikipiga simu muda mwingine hapokei wala hata kunitumia msg kwamba yuko busy hakuna, natuma msg hajibu. Kuna wakati akipokea maongezi yake hata nnavyoongea na dada yangu aliyenizidi miaka 25 huwa nafurahia kwani huwa tunataniana. Majibu yake ni mkato na ukimwambia i love you anakujibu, ok! Hii ni tofauti na mwanzo. Nimezoea kila asubuhi na mapema kumsabahi na kumtakia kazi njema lakini siku hizi anapokea cm na kuniambia ana usingizi hata kama ni muda ambao mfanyakazi anatakiwa aamke. Kuna siku ndo kabisa sauti ilikuwa kama kuna breakfast inaendelea, loh!

Nilikata simu na kwenda kufanya mambo yangu. Jana nimempigia simu akawa anaongea kiuoga nikamuuliza, are you at your home? Akakata simu na mpaka leo hapokei. Kuna wakati huwa ananambia simu ni mbovu lakini bado najiuliza mbo wakati mwingine unampigia na kuongea naye? Nifanyeje ndugu zangu? Yaani hata ibada yangu leo imekuwa sio kama kawaida.

mwe!!!! long distance never work kijana...kamatia hapo hapo ulipo huyo anagegedwa na jamaa mwengine
 
Tumekuwa pamoja kwa miaka miwili sasa plus miaka miwili ya kuzungushwa inakuwa minne. Nampenda sana na ndo mtarajiwa wangu Mungu akijalia. Kwa muda wa mwaka mmoja sasa hivi yuko mbali kabisa nami ila navumilia na sijawahi kumcheat. Lakini kuna tabia imejitokeza kama miezi mitatu hivi simuelewi kwa kweli.

Nikipiga simu muda mwingine hapokei wala hata kunitumia msg kwamba yuko busy hakuna, natuma msg hajibu. Kuna wakati akipokea maongezi yake hata nnavyoongea na UNAWEZA SHINDWA ELEWA MAANDISHI,LAKINI HATA PICHA JAMANI?
 
sasa ndugu kwa kinywa chako yapata mwaka wa nne huu, nini malengo ya hayo mahusiano yenu, maana distance ina chalenge zake ,au ndo bado mnasomana, yawezekana amepunguza upendo coz haelewei mna malengo gani, miaka minne inatosha kupanga mikakati chanya, pia muavoid kukaa kipindi kirefu bila kuonana mawasiliano ya simu pekee hayatoshi kuboresha na kulipalilia penzi
 
hizo ni dalili tosha kuwahuyomtu,ame loose interest na wewe.ila uamuziniwako,jaribu na wewe kumpa mapozi vilevile,usijionyeshe kwake kama unaumia.ingawa unaumia,baada ya muda ukiona mambo ndio hayo hayo,songa mbele na maisha yako.mpotezee for good ingawa ni ngumu
 
Jaribu kumpotezea kwa ghalama za vocha na chupi n.k ulizo kuwa unamghalamia
 
Unadhani wahenga waliosema "fimbo ya mbali haiui nyoka" hawakuwa na akili timamu? Kalagabaho!
 
hapo siyo mapenzi ya mbali ,hapo nimapenzi hakuna mkuu...........kwisha habari yako wewe songa na maisha.
hlf huyo mpenzi wako yupo wapi mpaka unakaa mwaka mzima hamjaonana?

sehemu nilipo na maisha yananifanya kuwa hivyo. Kuna muda alipata likizo nilipomwambia aje akasema kuna kazi anazifanya ko akashindwa kuja. Yaani we acha tu
 
Unadhani wahenga waliosema "fimbo ya mbali haiui nyoka" hawakuwa na akili timamu? Kalagabaho!

sasa na masuala ya kazi itakuwaje. Au ndo tuwe tunaoa wale wanaofanya karibu nasi? Na wale tunaokutana nao vyuoni itakuwaje?
 
Suprise at first tulikuwa karibu kwani alikuwa karibu na nilipo. Ni mwaka huu mmoja tu ndo wenye hizi kashi kashi.
 
Pole sana,i can imagine maumivu unayoyapata kwa sasa.Hiyo ilinikuta mm j2 iliyopita aisee nashindwa ht kusimulia yaan kanisan hapakukalika ila nashukru angalau sasa nimeanza kuzoea.

asante ndugu yangu. Inakuwa ni ishu kumuacha hivi hivi bila ushahidi wa kutosha. Pia ni mtu ambaye najipanga kuishi naye lakini umbali ndo unaleta shida.
 
... Pole sana..
Tafuta mmoja 2 wa kuiba ili mizani ibalance.
Kinachokusumbua ni kwamba unahisi mpenzi wako anahemewa.. Na kamwe huwezi tibu hilo gonjwa mpaka na ww ufanye hicho unachomwazia mpenzi wako.
So nakushaur tafuta ka1 kakupunguzia wivu.
 
Tafuta rafiki aliye karibu naye achunguze.. lkn dalili zote zaonyesha huyo hakupendi.. Jiondoe mapema tafuta atakayekupenda kwa dhati

sehemu alipo hakuna ninayemfahamu na rafiki wa karibu yuko mbali kidogo na eneo anakoishi. Aafu washkaji somtime ukiwatumia ndo wanageuza ishu na kubadili wao. Nawaogopa sana wanaume kwenye mambo ya mapenzi.
 
hizo ni dalili tosha kuwahuyomtu,ame loose interest na wewe.ila uamuziniwako,jaribu na wewe kumpa mapozi vilevile,usijionyeshe kwake kama unaumia.ingawa unaumia,baada ya muda ukiona mambo ndio hayo hayo,songa mbele na maisha yako.mpotezee for good ingawa ni ngumu

...mwenzio kaoza wewe..
Hawezi fanya maigizo
 
Pole maumivu yako ni kutokana na hisia zako. Uwezekano mkubwa ana mtu mwingine tayari.

Kujihakikishia (itasaidia nadhani), nenda kwake utapata ukweli wote na itasaidia kusupport maamuzi yajayo.

Pole sana mpendwa!

asante dada angu. Itabidi nijipange maana yeye kuja ananambia ratiba imemkaba. Lakini unaweza fika kule ukaishia kutambulishwa kwamba huyu ndo mume wangu. Hayo maumivu yake yatakuwa mara nyingi zaidi. Unaweza jikuta unaishia jela kwa kupiga mtu.
 
...mwenzio kaoza wewe..
Hawezi fanya maigizo

kweli aisee, unajua mtu ambaye ulishafunga ukurasa ni tofauti na unayemfukuzia. Huku najiribu kuwa makini ili nisijeamua kujichomeka kwa mtu yeyote kupunguza maumivu.
 
asante dada angu. Itabidi nijipange maana yeye kuja ananambia ratiba imemkaba. Lakini unaweza fika kule ukaishia kutambulishwa kwamba huyu ndo mume wangu. Hayo maumivu yake yatakuwa mara nyingi zaidi. Unaweza jikuta unaishia jela kwa kupiga mtu.

Lakini ni bora kujua ukweli mchungu kuliko kuishi kwa suspense!
 
Back
Top Bottom