Emmado
JF-Expert Member
- Dec 2, 2010
- 225
- 278
Unayempenda kwa dhati Sinza huna uhakika kama kwake uko peke yako au ana ki-branch cha LOVE SACCOSS Temeke na huwa anakopesha penzi kwa riba nafuu ya asilimia 10 halafu anajazilizia kipato kwenye akaunti yenu ya pamoja ya Benki ya Mapenzi makao makuu ya Home Branch.
Na kwa kumhisi ana ki-branch,na wewe unatafuta tawi la VICOBA Mlandizi unaanza kutumbukiza mafao yako huko na kuzungusha hakuna kitu kibaya kama kuhisi-hisi vitu,uko kwenye uhusiano na mtu lakini una wasiwasi kama unaoga bafu la nje la makuti..kila anachokwambia unahisi-hisi tu,akisema amelala unahisi-hisi,akisema anatoka na rafiki zake unahisi-hisi.
Hisia-hasi ni dalili za KUTOM-TRUST and There is no Love without Trust, wote mtageuka waigizaji wa Bongo-Movie,Director wewe,Script writer wewe,Costume Designer wewe,na kushoot wewe,lazima Muvi ya penzi lenu iwe mbaya tu.
Penzi tamu ni lile mnaloaminiana na kuheshimiana huku ukijua unapendwa wewe na unampenda yeye tu, kama humuamini umpendaye kwanini umkabidhi moyo wako wa thamani aulinde?
Wote mtajikuta mnahamisha akiba yenu kutoka Benki yenu ya pamoja na kwenda kupanda mbegu DECI.