Mapenzi ya kweli au kudangananya

Do santos

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
635
337
Wawili wanaoitwa wapendanao wameoana kwa sherehe na vifijo,sasa mmoja au wote wanatoka nje ya ndoa.Swali kwa nini watoke nje ya ndoa?Wamechokana au kuna tatizo baina yao?Ndo watoke nje ya ndoa?Wenye kutoka nje ya ndoa wanamaanisha ni kwa wenzao?Hawana mapenzi na kwanini wamewaoa/kuolewa nao? Piga picha mume/mke anavua nguo tena kwa khiari yake kwa asiye mume/mke wake,je kweli kuna mapenzi kwa walioona wenye michezo kama hii.Ajabu kuna kesi nyingi za usaliti wa ndoa kwa viongozi dini,serikali za mitaa na mahakama za mwanzo.Ndugu zangu hivi kuna mapenzi ya kweli baina ya mume na mke kwa sasa? Nasubiri michango yenu
 
Swali la kwanza wanatakiwa wajibu hao wahusika..sisi tutaishia kubuni tu!Nwyz sababu zinazowatoa watu nje ya ndoa ni nyingi baadhi zikiwa tamaa..maelewano finyu..mawasiliano hafifu..kutokua na heshima..kutokuridhika na mwenzi..ndoa za kulazimishana unakuta mmoja anataka iwepo mwingine hajali!Nwyz kwasababu hivi vitu vipo haina maana hamna mapenzi tena!Ni kiasi tu chakumpata atakae kupenda na kukuheshimu wewe kama ambavyo utafanya kwake!
 
ni mambo mengi sana na kupata usahihi inategemea na wahusika wenyewe.
ila kwa hao hapo imetokea mapema na i can guess itakuwa wameingia kwenye ndoa bila kuwa na hisia za kupendana na inaonesha kila mmoja hajaridhika na mwenzake.
 
Kutoka nje ya ndo hakumaanishi ni kutopendana, sijui ni ibilisi,tamaa, mfumo, mazoea wanajua wahusika. Ukifutilia hao watu utagundua wanapendana sana tu hata ukijaribu kusema ndoa ivunjike wako tayari kiufa, na hata kutoka kwao ni kwa siri sana. pengine wanavyodai msosi kila siku uleule unachosha. Ila Mungu atusaidie katika hili.
 
Lazima kuna sababu japo sababu zingine hazina msingi wala nini ili mradi tu maisha yanaendelea
 
thread zile zile kila siku...
halaf haya masuali yake hayako katika mpangilio kabisa yaani. anauliza masuali kama anaiuliza GOOGLE bana! aulize masuali kijitu kizima bana! (nimekasirika kweli wakati naandika hii post)
 
Haya mlio wahi kutoka nje ya ndoa tunaomba majibu. Talk from experience and nt hearsay!
 
halaf haya masuali yake hayako katika mpangilio kabisa yaani. anauliza masuali kama anaiuliza GOOGLE bana! aulize masuali kijitu kizima bana! (nimekasirika kweli wakati naandika hii post)

ha ha hah ha
 
Back
Top Bottom