Mapenzi ya jinsia moja yadaiwa kushamiri Morogoro

Philip Dominick

JF-Expert Member
May 26, 2013
1,021
189
JUMAPILI, JUNI 16, 2013 05:50 NA
MERINA ROBERT, MOROGORO
HALMASHAURI ya Manispaa ya
Morogoro inakabiliwa na
changamoto ya kukua kwa
maambukizi ya Ukimwi, baada ya
kushamiri kwa biashara ya mapenzi
ya jinsia moja. Akizungumza na
waandishi wa habari mjini hapa,
Naibu Meya Manispaa ya
Morogoro, Lidya Mbiaji, alisema
kuwa kumekuwa na tatizo kubwa la
kushamiri kwa vichocheo vya
ngono, hali inayochangia kukua kwa
kiwango cha maambukizi ya Ukimwi
katika mkoa huo.
Pia alisema ongezeko la nyumba za
kulala wageni nalo limekuwa
kichocheo kikubwa cha kushamiri
kwa biashara ya ngono zembe.
Aliionya jamii kuepukana na mila
na desturi zinazochangia kuleta
vichocheo vya kuongezeka kwa
maambukizi ya ukimwi, ikiwemo
ngoma za unyago zijulikanazo kwa
jina maarufu la kunemwa pamoja
na mabanda ya kuonyesha video
ambayo nje yamekuwa yakionyesha
mechi za soka, lakini ndani ya
mabanda hayo huonyesha picha za
ngono na kusababisha kuleta
hamasa ya watu kufanya ngono.
Pia aliviomba vyombo vya habari
kusaidia kuelimisha jamii namna ya
kujiepusha vitendo vinavyochangia
maambukizi ya ukimwi, kwani hali
si shwari kutokana na makundi ya
watu wanaofanya biashara ya
ngono kuvamia Manispaa ya
Morogoro.
Alisema hata kwa wasomi wa vyuo
vikuu, hali pia si shwari, kutokana
tafiti kuonyesha kuwa wana
kiwango cha juu cha kufanya ngono
zembe, hivyo kulitisha taifa
kupoteza wasomi wake mara baada
ya kumaliza masomo yao.
“Kumekuwa na makundi makubwa
ya jamii yanayoingia katika hatari
ya kupata maambukizi…ukiangalia
kundi la wanafunzi, watu masikini
na wanawake, hasa wajane
changamoto hii inawagusa moja
kwa moja,” alisema Mbiaji.

soure:mtanzania
 
Je waandishi wa habari nao walikuwepo,,,maana huwa sielewi habar zao zinachochea ngono au zinahamasisha kuachana na ngono
 
Back
Top Bottom