Mapenzi ya Jinsia moja Sekondari Bagamoyo

Mapenzi ya Jinsia moja Sekondari Bagamoyo

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
14,481
Reaction score
10,234
Nimekutana na habari hii hapa chini kwenye Gazeti la Nipashe la tarehe 25/01/2014.Nimechelea kuileta hii habari kwenu kwa muktadha wa kujadiliana ili kuweza kutanabaisha chimbuko la mparanganyiko huu usio na bukheri katika jamii yetu ya Watanzania.

[h=2]Mapenzi ya jinsia moja yalalamikiwa sekondari wasichana[/h]


Na Beatrice Shayo



25th January 2014


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa






Shule moja ya sekondari ya wasichana iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, imelalamikiwa na wanafunzi pamoja na wazazi kuwa mabinti wanajihusisha na vitendo vya ngono vya jinsia moja (usagaji).

Akizungumza na NIPASHE mmoja wa wazazi (jina linahifadhiwa) alisema shule hiyo imepoteza sifa kwa kuwa kuna wimbi kubwa la wanafunzi wanaojihusisha na vitendo hivyo vya usagaji.

Alisema mtoto wake alikuwa ameanza kidato cha kwanza mwaka jana na baada ya kumuandikisha ndipo baadhi ya watu walipomueleza kuwa shule hiyo kwa sasa ina sifa mbaya ya mchezo ‘huo mchafu.’

"Baada ya kuelezwa nikasema nitalifanyia kazi jambo hilo hivi karibuni katika kupekua madaftari ya mwanangu nakutana na kibarua cha mapenzi alichoandikiwa na msichana mwenzake niliumia sana na nilitumia nguvu kumbana bila hivyo asingeniambia," alisema

Alisema ilimbidi amhamishe binti yake na kujiunga na shule moja ya sekondari iliyopo mkoani Tanga kwa ajili ya kuendelea na masomo ya kidato cha pili mwaka huu.

Mzazi huyo alisema anashangazwa ni kwa nini hatua hazichukuliwi wakati suala hilo ni la hatari kwani watoto wao wataharibika kiakili pamoja na kimwili na wanaweza kuambukizana VVU na Ukimwi..

Alisema wakati mwanaye akisoma katika shule hiyo alikuwa akihudhuria vikao vya wazazi mara kwa mara na kwamba kila kikao walikuwa wakifukuzwa wanafunzi kutokana na mwenendo huo.

"Hili tatizo ni kubwa na kufukuzwa kwa mwanafunzi sidhani kuwa wanatatua tatizo nadhani hakuna usimamizi mzuri kwani wangeweza kudhibiti kwa haraka tatizo hilo kabla ya kuwa kubwa," alisema

Pia alisema ndugu yake imembidi amhamishe mwanae na kumtafutia shule nyingine kwa kuhofia binti yake kurubuniwa kwani wanakuwa ni wadogo na hawaelewi chochote, hivyo inaweza kuwa rahisi kudanganywa na kuingia kwenye vitendo hivyo viovu.

Alisema kuwa hata kiwango cha ufaulu kwa sasa shule hiyo imeshuka kutokana na tatizo hilo kwa wanafunzi .

Hata hivyo, NIPASHE ilizungumza na mwanafunzi mmoja ambaye anasoma katika shule hiyo kuhusiana na suala hilo ambapo alikiri kuwepo kwa jambo hilo na kueleza kuwa wanaofanya mchezo huo ni wa kidato cha tano na cha sita.

"Mimi hawajanifanyia ila najua wanaofanya mchezo huo ni wale walioko kidato cha tano na cha sita," alisema Pia kuna baadhi ya wazazi wengine wamekuwa wakilalamikia jambo hilo na kueleza kuwa ndugu zao imewalazimu kuwahamisha watoto wao kutokana na vitendo hivyo vinavyofanyika shuleni hapo.




CHANZO: NIPASHE

MY TAKE
Tatizo la msingi hapa ni nini katika jamii yetu? nini inapelekea mambo haya kukua kwa kasi?



Karibuni kwa mjadala mujarabu.
 
Wanasema uhuru wa kupendaa bila kuvunjaa sheriaa hata uamue mbwaa awe mpezi wako ni sawaaa
 
Ndo tunamaliza tamaduni za kwetu TZ/Afrika na kwenda na mambo ya kimagharibi. Na mambo tunayoangalia kwenye tamthilia na movie zetu na watoto yanachangia haya kwa kiwango kikubwa.
 
Leo baada ya kurudi nyumbani mwanangu 8yrs old wa kiume wa std three ananiambia; wakati akila sausage alizopewa na mama yake, eti mwanafunzi mwenzake wa kike kamwambia kuwa; nanukuu, "Dadii Larisa kaniambia eti mdudu wa mwanamke yuko kama sambusa halafu wa mwanaume yuko kama sausage."

nimemwacha na mama yake aanze naye, mi nitarudi baadaye kuzungumza naye. acha nipate kinana yangu kwanza huku nikitafuta namna ya kumweka Sawa.

wazazi tujipange we've got work to do.
 
Leo baada ya kurudi nyumbani mwanangu 8yrs old wa kiume wa std three ananiambia; wakati akila sausage alizopewa na mama yake, eti mwanafunzi mwenzake wa kike kamwambia kuwa; nanukuu, "Dadii Larisa kaniambia eti mdudu wa mwanamke yuko kama sambusa halafu wa mwanaume yuko kama sausage."

nimemwacha na mama yake aanze naye, mi nitarudi baadaye kuzungumza naye. acha nipate kinana yangu kwanza huku nikitafuta namna ya kumweka Sawa.

wazazi tujipange we've got work to do.

Kuna mmomonyoko mkubwa sana wa maadili...10 Years to come we will be talking of different society
 
Hii yote imesababishwa na kufuta michezo mashuleni hivyo wanafunzi wanajikuta wakimaliza vipindi mchana wanalala tu na shule za bweni ni balaa kwani nyege zikipanda hapo lazima atamshika mwenziye tu,
Kitu kingine ni matumizi ya simu za window mashuleni wanafunzi wanakuwa wanaagalia ngono kwenye simu zao badala ya kufikiria masomo, wakati mimi nasoma shule ya boys kipindi hicho mkitaka ilikuwa mkitaka kuangalia movie ya pilau kwenye tv ya shule ilikuwa ni siri na kwa watu wakubwa ie wa vidato vya juu na ilikuwa labda mara 1 kwa wk 2 au mwezi.


Wanasema uhuru wa kupendaa bila kuvunjaa sheriaa hata uamue mbwaa awe mpezi wako ni sawaaa
 
Waliopotea ni vigumu kuwarudisha labda mola peke yake ajuae kila ya mmoja wetu.kila kitokeacho si kigeni kwake mwokoz yeye ,mwachie yeye atakavyo yeye...................... HIZI NI SIKU ZA HATARI HATA MAISHA YAMEKUWA MAFUPI.


USISHANGAEEEEEEEE
 
Mbona huu mchezo kwa girls ni wasiku nyingi nakumbuka mm nimesoma girls tupu 2000 yalikuwepo so jamii itafute mbinu ya kuyazuia haya au shule za jinsia moja siziwepo tu
 
Back
Top Bottom