Mapenzi ya dhati hupimwa kwa njia zipi?

mr pipa

JF-Expert Member
Jul 26, 2021
2,329
4,852
Je, ni ni pale unapo mnunulia mpenzi wako zawadi na kumtimizia mahitaji yake kwa wakati? Au ni pale anapopatwa na matatizo na mpenzi wako akawa nawe bega kwa bega

Nauliza hili nikiwa na mifano hiyi miwili kuna jamaa zangu walikuwa wanawapenzi. Jamaa yangu wa kwanza yeye alipataga hela za madini akamfungulia mkewe duka la nguo mwanzoni walikuwa wanaishi saafi kabisa ila baadae kidogo jamaa akabadili gia angani

Akaanza kuwa mlevi na kuanza kumnyanyasa mke wake akapata hawala akawa amemjengea nyumba na kuhama kwa mkewe kuhamia huko huko end the day jamaa akawa amefilisika mchepuko ukamtimua

Kumbuka nyumba aliyoishi na mkewe na familia yake. Aliikopea bank na nyumba ikauzwa na benki sababu alishindwa kurejesha deni

Basi jamaa akawa kama kadata ikabidi amtoloke mkewe akabahatishe tena huko machimbo huku nyuma mkewe alimuacha kwenye wakati mgumu sana

Mwaka ukapita jamaa hapigi simu kwa mkewe wala nini ikabidi mke wake atafute kazi za ndani kumbuka alizaanae watoto wa tatu

Mwisho wa siku Mungu si Maxmelo mke akawa amekaa sawa kiuchumi na kufungua biashara na kujenga kabisa hiyo ni baada ya miaka kupita

Kwa upande wa jamaa Khali ilikuwa ngumu zaidi mwisho wa siku ikabidi amcheki mkewe

Mke wake kusikia mmewe alifurahi sana na kumtumia nauli na saizi wanaishi tena wote

Jamaa wa pili yeye mke wake kila anachotaka mkewe anamtimizia tena kwa wakati na mke anamkubali sana jamaa na wanaishi kwa furaha

Sasa turudi kwenye swali la mada hiyi upendo wa dhati hupimwa wakati gani?
 
Uzi mzuri
Nimependa kauli yako Mungu si Maxmelo 😂

Binafsi hadi niamini mwanamke ananipenda ni awe mkweli kwangu kwa kila kitu. Nitammiss sana ex wangu alikua hajui kusema uwongo kwenye mapenz hata kitu kimoja.

Ukiwa mbali unapewa taarifa kabisa ukichelewa zaidi ya wiki nagawa mbususu yako. All in all wena tunajuana i mean wenye mapenz ya dhati tunajuana, Ila uwe na uwezo wa kuweka hisia pembeni na kutumia akili, Akili mtu wang
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom